Back

ⓘ Koypu
Koypu
                                     

ⓘ Koypu

Koypu au panya-mito ni mnyama mgugunaji mkubwa kiasi na spishi pekee ya familia Myocastoridae. Kinyume na jina lake" panya-mito” mnyama huyu si panya wa kweli, kwa sababu panya ni wana wa familia Muridae. Koypu wanatokea Amerika ya Kusini kwa asili lakini wamewasilishwa sasa katika Amerika ya Kaskazini, Ulaya, Asia na Afrika, na wafugaji wa wanyama-sufu hasa. Sikuhizi Kenya ni nchi pekee katika Afrika ambapo wanaendelea kuishi porini. Hata kama wanaendelea kutathminiwa kwa ajili ya sufu yao, katika nchi nyingi wanafikiriwa kama spishi mvamizi kwa sababu ya mwenendo wake mharibifu wa kula na kuchimba.

Koypu anafanana na biva mdogo lakini mkia wake si mpana. Urefu wake ni sm 40-60 na mkia wa sm 30-45. Uzito ni kg 5-9. Wana meno ya mbele makubwa yenye rangi ya machungwa. Manyoya yake ni mazito na magumu yenye rangi ya kahawia lakini malaika yake meupe ni laini. Ana doa jeupe puani. Miguu ya nyuma ina ngozi kati ya vidole. Chuchu za jike zipo mbavuni ili kunyonyesha watoto wakati jike yupo majini. Wanyama hawa huishi katika matundu kando ya maji na hula mimea ya maji. Humeza chakula sawa na 25% ya uzito wao lakini hupoteza takriban 90% ya uoto wakila.

                                     

1. Soma pia

  • Sandro Bertolino, Aurelio Perrone, and Laura Gola 2005 Effectiveness of coypu control in small Italian wetland areas. Wildlife Society Bulletin 33 2: 714–72.
  • Lauren E. Nolfo-Clements 2006 Seasonal variations in habitat availability, habitat selection, and movement patterns of Myocastor coypus on a subtropical freshwater floating marsh. Dissertation Tulane University. New Orleans. ISBN 0-542-60916-9
  • Carter, J., A.L. Foote, and L.A. Johnson-Randall 1999 Modeling the effects of nutria Myocastor coypus on wetland loss. Wetlands 19 1: 209-219.
  • Sheffels, Trevor and Mark Systma 2007 Report on Nutria Management and Research in the Pacific Northwest Center for Lakes and Reservoir Environmental Sciences and Resources, Portland State University. Available on-line: Archived Juni 5, 2010 at the Wayback Machine.
  • Carter, Jacoby and Billy P. Leonard 2002 A Review of the Literature on the Worldwide Distribution, Spread of, and Efforts to Eradicate the Coypu Myocastor coypus. Wildlife Society Bulletin 30 1: 162–175.
                                     

2. Viungo vya nje

  • Athari ya koypu juu ya upotezaji wa vinamasi katika pwaa ya mashariki ya chini ya Maryland ripoti ya USGS bila tarehe
  • Maelezo mafupi ya spishi - Koypu Myocastor coypus Kituo cha Taifa cha Maelezo kuhusu Spishi Wavamizi Maktaba ya Taifa ya Kilimo ya Muungano ya Madola ya Amerika. Maelezo ya ujumla na habari kuhusu koypu.
  • Historia, usambazaji na chamko ya uwasilisho wa koypu ulimwenguni; jitihada za kumkomesha yenye viungo kuelekea tovuti nyingine za koypu
  • Chuo Kikuu cha Dola la Portland Archived Mei 5, 2010 at the Wayback Machine. Ripoti kuhusu koypu katika Magharibi-kaskazi ya Pasifiki ya Amerika ya Kaskazini.