Back

ⓘ Lagos
Lagos
                                     

ⓘ Lagos

Lagos ni mji mkubwa wa Nigeria. Ilikuwa mji mkuu wa nchi hadi mwaka 1991.

Ikiwa na wakazi takriban milioni 12 katika eneo la jiji na milioni 15 - 22 katika rundiko la mji ni kati ya miji mikubwa zaidi ya Afrika; inawezekana kwamba idadi ya watu imeshapita ya Kairo, hivyo kuwa jiji lenye watu wengi barani Afrika.

Lagos ilianzishwa kama mji wa bandari uliokua juu ya visiwa vidogo karibu na mdomo wa wangwa wa Lagos unapounganika na Bahari ya Atlantiki.

Bandari ya Lagos iko kati ya bandari muhimu zaidi Afrika.

                                     

1. Jiografia

Lagos iko mwambaoni mwa Ghuba ya Guinea; wenyeji hutofautiana sehemu mbili kuu ambazo ni "kisiwani" The Island na "barani" Mainland.

Lagos kisiwani

Lagos kisiwani ni zaidi ya kisiwa kimoja, jina hili linajumlisha pande zote zilizotengwa na bara kwa mfereji ambao ni mlango wa wangwa wa Lagos kwenda baharini.

Visiwa vikubwa ni Lagos Island, Ikoyi, na Viktoria pamoja na visiwa vidogo mbalimbali, mara nyingi mifereji midogo kati yake imeshafunikwa kwa majengo na madaraja mengi au kujazwa. Sehemu hii ni kitovu cha biashara na maofisi pamoja na makazi yenye bei za juu.

Madaraja matatu makubwa huunganisha sehemu ya kisiwani na bara ambazo ni madaraja ya Carter, Eko na daraja la tatu la bara.

Lagos bara

Wakazi wengi wa Lagos huishi barani, ngambo ya wangwa. Huko viko viwanda vingi.

                                     

2. Utawala

Hadi mwaka 2006 kulikuwa na manisipaa ya Lagos iliyojumlisha Lagos Visiwani pamoja na maeneo machache barani. Mwaka ule manisipaa ilivunjika na kugawiwa kwa halmashauri mbalimbali. Hali halisi jiji likaendelea kukua barani. Tangu siku zile serikali inalenga kuimarisha utawala kwenye ngazi za chini.

Ndani ya eneo la Lagos hakuna muundo wa manisipaa au jiji moja bali kuna halmashauri 16 zinazoitwa Local Government Area LGA na kuunganishwa katika "Metropolitan Lagos". Idadi za wakazi hapa chini zinarejea sensa ya 21 Machi 2006.

                                     

3. Tabianchi

Lagos huwa na tabianchi ya savana tropiki Aw kufuatana na upambanuzi wa Koeppen. Kiwango cha mvua kinatofautiana sana baina ya majira ya mvua na ya ukame. Masika yenye mvua yaanza mwezi Aprili na kuishia Oktoba. Ya ukame yako kati ya Novemba hadi Machi. Mwezi wenye mvua nyingi ni Juni yenye usimbishaji wa mm 315.5, ilhali Januari ina milimita 13.2 pekee.

Lagos iko karibu na ikweta, tena kwenye uwiano wa bahari, hivyo hakuna tofauti kubwa katika halijoto kati ya miezi ya mwaka. Wakati wa Machi wastani uko kwenye sentigredi 28.5 na Agosti huwa na 25.

                                     

4. Historia

Kiasili eneo la Lagos lilikaliwa na kabila la Waawori ambao ni sehemu ya Wayoruba. Katika karne ya 15 ikaitwa "Oko".

Chini ya chifu wao Olofin hao Waawori wakahamia kwenye visiwa ndani ya wangwa pamoja na Kisiwa cha Lagos

Katika karne ya 16 eneo lilitwaliwa na milki ya Benin na kisiwa cha Lagos kilikuwa kambi la kijeshi la Benin kilichoitwa "Eko". Jina hili linatumiwa hadi leo na wenyeji wa Lagos.

Jina la Lagos lilitumiwa na mabaharia Wareno waliojenga huko kituo cha biashara na kukiita kwa heshima ya mji wa Lagos huko Ureno.

Mwaka 1472 baharia Mreno Ruy de Sequeira alifika Eko akaanzisha kituo cha "Lagos" - kwa Kireno neno hili lamaanisha "maziwa": ni pia jina la mji wa Ureno ya kusini.

Katika karne zilizofuata Lagos ilikuwa ufalme mdogo wa Kiyoruba. Mtawala wake alistawi na kutajiriki kutokana na biashara na wafanyabiashara kutoka Ulaya. Sehemu kubwa ilikuwa biashara ya watumwa.

Katika karne ya 19 Uingereza ilibadilisha msimamo wake kuhusu utumwa wakijaribu kukandamiza biashara hiyo katika Afrika ya Mashariki. Mwaka 1841 Oba mpya aliyeitwa Akitoye alipiga marufuku biashara ya watumwa lakini alipinduliwa kwa sababu ya upinzani wa wafanyabiashara wenyeji. Akitoye aliomba usaidizi wa Uingereza. Manowari za Kiingereza zilishambulia Lagos tarehe 26 na 27 Desemba 1852 na kumrudisha mfalme.

Matatizo ya biashara ya watumwa yaliendelea na Waingereza walichukua kisiwa cha Lagos na kuifanya kwanza eneo lindwa halafu koloni. Oba alibaki na madaraka machache.                                     

5. Uchumi

Lagos ni kitovu cha uchumi wa Nigeria. Kiasi kikubwa cha pato la taifa kinazalishwa hapa. Makao makuu ya makampuni makubwa na benki yako Lagos Kisiwani.

Lagos ni pia moyo wa tasnia ya mawasiliano ICT ya Afrika ya Magharibi.

Sehemu za Lagos zina hali ya juu, hata hivyo theluthi mbili za wakazi huishi katika mitaa ya vibanda pasipo maji ya bomba na vyoo vya kutosha.

Bandari ya Lagos ni bandari kubwa ya Nigeria iko pia kati ya mabandari makubwa ya Afrika. Ina pande tatu ambazo ni kando la kisiwa cha Lagos chenyewe halafu sehemu za Apapa penye kituo cha kontena na Tin Can. Bandari imeunganishwa na mfumo wa reli ya Nigeria.

Sehemu muhimu ya biashara ya bandari ni petroliamu inayosafirishwa hapa kwenda kote duniani. Mafuta ya petroli na bidhaa zilizotengenezwa kutoka mafuta hayo ni sawa na asilimia 14 za Jumla ya Pato la Taifa GDP na 90% za mapato ya fedha za kigeni.

                                     
 • Lagos ni jimbo la Nigeria.
 • Los Lagos Kihispania: X Región de Los Lagos ni jina la kutaja mkoa ulioko nchini Chile. Mji mkuu wake ni Puerto Montt. Wilaya ya Llanquihue Wilaya ya
 • Wangwa wa Lagos uko nchini Nigeria ukiwa mmojawapo kati ya nyangwa kubwa kwenye pwani ya ghuba ya Guinea. Eneo lake ni takriban km² 6, 354.7 Ni gimba la
 • a Lagos Girl Movie starring Alexx Ekubo, Dolapo Oni, Liz Benson premieres in Lagos en - US IBAKATV - NOLLYWOOD 2017 - 12 - 27 Diary Of A Lagos Girl
 • Brila FM - Lagos Lagos 89.75 - Eko FM Ikeja, Lagos 90.90 - Top Radio Lagos 92.3 - Inspiration FM Lagos 93.7 - Rhythm FM - Lagos Lagos 94.8 - Altitude
 • Dar 2 Lagos ni jina la filamu iliyotoka mwaka 2006 kutoka nchini Tanzania. Ndani yake anakuja Mercy Johnson, Steven Kanumba, Bimbo Akintola, David Manento
 • mbalimbali katika idara ya sheria ya Jimbo la Lagos anakotoka. Yemi Osinbajo alizaliwa mwaka 1957 mjini Lagos Alimwoa Dolapo Soyode Osinbajo aliye mjukuu
 • uko katika sehemu ya Ikeja, nchi ya Lagos nchini Nigeria, na uwanja huu wa ndege ndio ambao unahudumia mji wa Lagos kusini magharibi mwa Nigeria na taifa
 • aliipata katika shule ya St. Finbarr s College, Lagos Alisoma pia chuo chuo kikuu cha lagos University of Lagos ambapo alisoma mawasiliano ya uma. Kazi ya
 • Imepakana na Benin, Niger, Chad na Kamerun. Mji mkuu ni Abuja ikitanguliwa na Lagos hadi mwaka 1991. Nigeria imepata uhuru wake tarehe 1 Oktoba 1960, ikiunganisha
 • Ayo Yusuf Oyejide amezaliwa tar. 19 Julai 1988 mjini Lagos ni mwanamuziki wa afro kutoka nchini Nigeria.