Back

ⓘ AmiriAmiri
                                     

ⓘ Amiri

Amiri au Emir ni cheo cha mtawala mwislamu anayesimamia emirati. Kiasili maana yake ni "mwenye amri" kama cheo cha kijeshi au kiserikali.

Katika miaka ya kwanza ya Uislamu amiri alikuwa mkuu wa jeshi au sehemu ya jeshi. Baada ya kutwaa nchi alikuwa na nafasi kama gavana ya khalifa. Kutokana na upanuzi wa himaya ya kiislamu na ushaifu wa serikali kuu amiri aliweza kutawala mara nyingi kama mfalme mdogo lakini kwa kawaida alitafuta kibali cha khalifa.

                                     

1. Cheo cha kihistoria

Cheo hiki kilipatikana kwa maumbo mbalimbali kama

  • amir al-bahr ‏امير البحر‎, "amiri wa bahari" ilikuwa cheo cha kiongozi wa jeshi la maji ikaingia katika lugha za Kiulaya kama "admiral".
  • amir al-umara’ "amiri wa maamiri" ilikuwa cheo cha jemadari mkuu wa jeshi la Waabasiya. Baadaye katika Milki ya Osmani ilikuwa cheo cha gavana wa jimbo kubwa.
  • amir al-mu’minin "mkuu wa waumini" ilikuwa cheo cha heshima kwa makhalifa tangu Umar. Hadi leo ni cheo kimoja cha sultani wa Moroko.
                                     

2. Cheo cha mtawala wa emirati

Nchi kadhaa zinazotumia jina "emirati" na cheo cha amiri kama mkuu wa dola ziko kwenye Bara Arabu. Mfano ni Kuwait na Qatar. Pia nchi zilinazojulikana kwa Kiswahili kama Falme za Kiarabu zinajiita emirati chini ya maamiri.

Amiri wa Bahrain alijiita mfalme tangu 2002.

Free and no ads
no need to download or install

Pino - logical board game which is based on tactics and strategy. In general this is a remix of chess, checkers and corners. The game develops imagination, concentration, teaches how to solve tasks, plan their own actions and of course to think logically. It does not matter how much pieces you have, the main thing is how they are placement!

online intellectual game →