Back

ⓘ Nishati mbadala
Nishati mbadala
                                     

ⓘ Nishati mbadala

Nishati mbadala ni aina za nishati kutoka vyanzo asilia kama vile mwanga wa jua, nguvu ya upepo, mvua, joto kutoka ardhi, mwendo wa kupwakujaa, kuni au aina nyingine za biomasi na mengine.

Kwa jumla ni vyanzo vya nishati visivyokwisha kutokana na matumizi au kupoa haraka, tofauti na fueli za kisukuku ambazo zinatoka kwenye vyanzo kama makaa mawe, gesi asilia au mafuta ya petroli zinazoendelea kupungua kadiri zinazotumiwa.

Uwekezaji kwenye miradi ya nishati mbadala duniani ulifikia kiasi cha dola za Marekani bilioni 286 mwaka 2015, huku nchi za China na Marekani zikiongoza kwa uwekezaji. Kazi zinazohusiana na nishati mbadala duniani zinakadiriwa kufikia milioni 7.7. Nchi kama Iceland inatumia asilimia 85 ya mahitaji yake ya nishati kutoka nishati mbadala na hivyo kuwa nchi ya kwanza duniani kwa matumizi makubwa ya aina hii ya nishati. Kutokana na ripoti iliyotolewa na REN21 (Renewable Energy Policy Network for the 21st Century, mwaka 2015 nishati mbadala ilichangia asilimia 19.2 ya matumizi ya nishati duniani.

                                     

1. Matumizi ya nishati mbadala

Mwaka 2008 takriban 19-20% ya matumizi ya nishati duniani yametokea kwenye nishati mbadala; wakati ule sehemu kubwa ya takriban asilimia 13 kutoka biomasi hasa kuni na 3.2% kutoka nguvu ya umememaji.

Mwaka 2016/17 kiasi hiki kilibadilika tayari. Biomasi ya kawaida kuni ilichangia asilimia 8.9, joto kuoka biomasi, jotoardhi na jotojua 4.2 %, umememaji 3.9 na umemejua pamoja na umeme wa upepo ilikuwa 2.2%. Vyanzo vya kisasa vya nishati mbadala inaogezeka haraka.

Hali halisi manufaa kutoka nishati ya jua ni kubwa zaidi sana kwa sababu matumizi yote ya mimea, mazao na matunda yana nishati ya jua kama msingi wake; pia kiwango cha joto la mazingira kinasababishwa na jua lakini katika takwimu hizi zinataja viwango tu vinavotumiwa na jitihada za binadamu kubadilisha mazingira asilia kama kupasha moto nyumbani, kupika vyakula, uzalishaji umeme, kuendesha usafiri na kadhalika.

Katika uzalishaji wa umeme duniani asilimia ya nguvu ya umememaji ilikuwa takriban 15%.

                                     

2. Kuongezeka kwa nguvu ya upepo

Teknolojia ya kuzalisha umeme wa upepo imepanuka sana katika miaka iliyopita. Mwisho wa mwaka 2009 ujazifu wa umeme kutoka chanzo hiki ulikuwa megawati 157.900 ambazo ni ongezeko la 31% tangu mwanzo wa mwaka uleule.

Maendeleo hayo mwanzoni yalitokea Ulaya, hasa Ujerumani, Udani na Uingereza lakini baadaye Marekani na China ziliongeza pia jitihada zao kupanua chanzo hicho cha umeme.

Katika nchi ya Denmark umeme kutoka nguvu ya upepo ni tayari asilimia 19 ya matumizi yote ya kitaifa.

                                     

3. Umemejua

Seli za umemejua zinabadilisha mwanga wa jua kuwa umeme. Teknolojia hiyo inaendelea haraka sana na gharama za seli hizi zinashuka. Kuna vituo vingi, hasa Ulaya, ambako serikali zimetoa misaada kwa ajili ya kutegeneza vituo hivyo na matumizi ya teknolojia hiyo.

Mwisho wa mwaka 2010 vituo vikubwa duniani vilikuwa:

 • Rovigo Photovoltaic Power Plant Italia, 70 MW,
 • Finsterwalde Solar Park Ujerumani, 80.7 MW,
 • Sarnia Photovoltaic Power Plant Kanada, 97 MW,
 • Olmedilla Photovoltaic Park Hispania, 60 MW,
 • Lieberose Photovoltaic Park Ujerumani, 53 MW.
 • Montalto di Castro Photovoltaic Power Station Italia, 84.2 MW
 • Strasskirchen Solar Park Ujerumani, 54 MW

Vituo vikubwa zaidi hutengenezwa.

                                     

4. Viungo vya nje

 • Nchi 11 zinazoongoza kwa nishati mbadala duniani
 • EPA uses onsite renewable technologies
 • Renewable Energy Nishati Mbadala, muswada ya kipindi cha Sauti ya Ujerumani, Huduma ya Kiswahili, kuhusu nishati mbadala. Tovuti ya dw.com, iliangaliwa Juni 2017
 • New World Record achieved in solar cell technology Archived Julai 12, 2009 at the Wayback Machine.
 • Mfuko wa Nishati Mbadala wa Afrika Mradi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya
 • Kuhusu nishati mbadala nchini China Kiswahili Archived Mei 18, 2013 at the Wayback Machine.
 • Vyanzo 10 vikuu vya nishati mbadala
 • US National Renewable Energy Laboratory NREL.
 • Energy conservation at home in Simple Wikibooks Archived Mei 29, 2008 at the Wayback Machine.