Back

ⓘ Uongo
Uongo
                                     

ⓘ Uongo

Kwa neno la kutaja kipindi cha miaka 10 tazama: mwongo

Uongo ni tamko lisilo kweli lanalotolewa kwa makusudi. Mtu anayesema uwongo anajua au anahisi ya kwamba maneno yake si ya kweli lakini anataka msikilizaji wa maneno yake ayaamini kuwa kweli.

Mara nyingi uwongo hutumiwa kwa kusudi la kuficha kosa, aibu au tendo haramu. Kusudi lingine ni kujipatia faida au kuzuia hasara.

Uwongo hutazamwa kuwa tofauti na maneno yasiyo kweli lakini msemaji hajui kwamba si kweli au alikosea mwenyewe.

                                     

1. Aina za uwongo

Augustino wa Hippo alikuwa kati ya wataalamu wa kwanza waliofanyia uwongo utafiti. Katika kitabu chake "Kuhusu uwongo" "De Mendacio" aliorodhesha aina nane za uwongo kama vile

  • Uwongo usiomwudhi mtu na kumsaidia mtu
  • Uwongo unaotolewa kwa kumfurahisha mtu wakati wa maongezi
  • Uwongo unaosimuliwa kwa furaha ya uwongo au kama mzaha
  • Uwongo unaosababisha hasara kwa watu kadhaa na kuwasaidia wengine
  • Uwongo usiomwudhi mtu na unaokoa heshima ya mtu
  • Uwongo kuhusu mafundisho ya dini
  • Uwongo usiomwudhi mtu lakini unaokoa uhai wa mtu
  • Uwongo unaoleta hasara kwa mtu bila kumsaidia yeyote

Hapa alitofautisha kati ya uwongo mzito unaoleta hasara kwa mtu au uzima wa milele na uwongo mwepesi unaoleta faida kwa mtu bila kumwudhi yeyote. Lakini aliona kila aina ya uwongo kuwa dhambi kwa sababu unafanya watu wasiweze kuaminiana.