Back

ⓘ Liturujia ya Milano
Liturujia ya Milano
                                     

ⓘ Liturujia ya Milano

Liturujia ya Milano ni liturujia maalumu ambayo inatumika katika sehemu kubwa ya jimbo kuu la Milano na katika parokia kadhaa za majimbo ya kandokando nchini Italia hadi baadhi ya zile za jimbo la Lugano.

Kesi ya pekee ni parokia ya Pescocostanzo iliyopo katika Italia ya kati inapotumika kwa ibada ya ubatizo.

Kama asili yake anatajwa babu wa Kanisa Ambrosi, aliyekuwa askofu wa jimbo hilo katika sehemu ya mwisho wa karne ya 4. Ndiyo sababu inaitwa pia Liturujia ya Ambrosi.

Baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano liturujia hiyo imeshughulikiwa sana na wachungaji na wataalamu mbalimbali hata kupata uhai mpya.

Ingawa Wakatoliki wa maeneo hayo milioni 5 hivi wanafuata liturujia hiyo, upande wa sheria za Kanisa hawatofautiani na wenzao wote wa Kanisa la Kilatini.

                                     

1. Marejeo

 • Messale Ambrosiano secondo il rito della santa Chiese di Milano. Riformato a norma dei decreti del Concilio Vaticano II. Promulgato dal Signor Cardinale Giovanno Colombo, arcivescovo di Milano, Milano 1976
 • Missale Ambrosianum iuxta ritum Sanctae Ecclesiae Mediolanensis, ex decreto Sacrosancto OEcumenici Concilii Vaticani II instauratum, auctoritate Ioannis Colombo Sanctae Romanae Ecclesiae Presbyter Cardinalis Archiepiscopi Mediolanensis promulgatum, Mediolani 1981
 • 1996 Dizionario di Liturgia Ambrosiana, Marco Navoni. ISBN 88-7023-219-0.
 • Griffiths, Alan 1999. We Give You Thanks and Praise. Canterbury Press. ISBN 1-58051-069-8.
 • 1986 Messale ambrosiano festivo. Piemme. ISBN 88-384-1421-1.
 • A. Ratti / M. Magistretti, Missale Ambrosianum Duplex, Mediolani 1913
                                     
 • yaliendelea zaidi ya miaka 200. Hivyo baadhi ya liturujia nyingine za Kilatini zimedumu mpaka leo, kama vile liturujia ya Ambrosi kandokando ya Milano Italia
 • Liturujia ya Toledo au liturujia ya Kimozarabu, yaani ya kati ya Waarabu ni liturujia ya pekee inayotumika hasa katika jimbo la Toledo Hispania pamoja
 • Liturujia ya Roma ni liturujia iliyoenea katika sehemu kubwa ya Kanisa Katoliki, kutoka makao yake makuu, Roma Italia Kwa asili yake ni liturujia ya
 • Liturujia ya Braga ni liturujia maalumu inayotumika tangu karne ya 6 hasa katika jimbo kuu la Braga Ureno Inahusiana na aina nyingine za liturujia
 • Jumatano ya Majivu, katika kalenda ya mwaka wa Kanisa la Magharibi, ni siku ya kwanza ya kwaresima, walau kwa madhehebu mengi katika liturujia ya Milano Kwaresima
 • Agostino wa Hippo Kati ya mambo ya pekee aliyoacha ni urithi wa tenzi na liturujia ya pekee inayoendelea kutumika Milano na sehemu nyingine kadhaa za Italia
 • upande wa liturujia wengi wa waamini wake wanafuata mapokeo ya Kanisa la Roma, lakini wengine wanafuata mapokeo ya Ambrosi wa Milano au yale ya Lyon, Braga
 • Liturujia ya Roma isiyo ya kawaida ni taratibu za ibada zinavyotumika katika Kanisa Katoliki kufuatana na mapokeo ya Roma jinsi yalivyokuwa mwaka 1962
 • Liturujia ya Lyon kwa Kilatini: ritus Lugdunensis ni liturujia mojawapo ya Kanisa la Kilatini ambayo imeendelea kutumika katika jimbo kuu la Lyon Ufaransa
 • Liturujia ya Vipindi ni sala rasmi ya Kanisa kama inavyoadhimishwa katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo, lakini ni jina hasa la mpangilio unaofuatwa
 • liturujia ni mpangilio wa maadhimisho au kalenda inayoratibu majira na sikukuu za Ukristo katika muda wa mwaka mmoja. Kalenda hii inataja nafasi ya vipindi