Back

ⓘ Khalifa
                                               

Almas Tower

Almas Tower Diamond Tower) ni jumba refu sana mjini Dubai, United Arab Emirates. Ujenzi wa jengo hili la ofisi ilianza mapema mwaka 2005 na kukamilika mwaka 2009. Jengo hili lilifika urefu wake kamili mwaka 2008, na kuwa jengo ja pili refu zaidi Dubai, baada ya Burj Khalifa. Jumba hili lina ghorofa 74, 70 ambazo ni za kutumika kwa biashara sambamba na ghorofa nne za huduma. Jumba hili liko kwenye kisiwa bandia chake mwenyewe katikati mwa mfuko wa Jumeirah Lake Towers, jumba hili ndilo refu zaidi katika majumba yote yatakayojengwa katika mfuko huo baada ya ujenzi kukamilika. Ilibuniwa na ka ...

Khalifa
                                     

ⓘ Khalifa

Khalifa ni cheo cha kihistoria kwa ajili ya kiongozi wa ummah. Ni neno la Kiarabu خليفة khalīfah linalomaanisha "makamu". Khalifa ni kifupi chake cha خليفة رسول الله "khalifatu-rasul-i-llah" kinachomaanisha "Makamu wa mtume wa Allah/Mungu". Hivyo mana yake ni makamu au mfuasi wa Mtume Muhammad katika nafasi yake kama kiongozi wa Waislamu.

Cheo cha khalifa kilitumiwa pamoja na cheo cha amīr-al-muminīn أمير المؤمنين "Jemadari Mkuu wa wenye Imani =Waislamu".

Utaratibu wa uongozi wa khalifa ulianzishwa baada ya kifo cha Muhammad mw. 632 na kuishia 3 Machi 1924 katika mapinduzi ya Atatürk.

                                     

1. Makhalifa wanne wa kwanza

Mtu wa kwanza aliyetumia cheo hiki alikuwa Abu Bakr aliyeongoza ummah ya Waislamu baada ya kifo cha Muhammad mwaka 632. Alichaguliwa na viongozi wa Waislamu kwa sababu Muhammad hakumwacha mrithi wala maagizo kuhusu atakayemfuata kama kiongozi.

Abu Bakr alifuatwa na Umar ibn al-Khattab, Uthman ibn Affan na Ali ibn Abi Talib.

Hawa wanne ni viongozi katika historia wanaokubaliwa na mikondo karibu yote ya Uislamu kwa sababu walichaguliwa na wafuasi wa Mtume Muhammad wenyewe. Isipokuwa kikundi kidogo cha Wakhariji wanaokubali makhalifa wawili wa kwanza pekee. Washia wanafundisha ya kwamba Ali angepaswa kuwa khalifa tangu mwanzo.

Baada ya kifo cha Ali lilitokea farakano kati ya Waislamu: wachache waliwataka wana wa Ali kundelea kuongoza lakini walio wengi walimfuata Muawiya mkuu wa jeshi la Waislamu huko Dameski aliyepigana na Ali na mwanawe Hussain kijeshi na kushinda.

                                     

2.1. Wamuawiya, Waabbasi na Waosmani Wamuawiya

Muawiya kama jemadari ya Waislamu wa Dameski alikuwa khalifa mwaka 661 baada ya kifo cha Ali. Tangu Muawiya hakuna khalifa tena aliyechaguliwa; Muawiya alimteua mwanawe Yazid amfuate. Tangu siku zile cheo cha Khalifa kiliendela ama kwa mfuasi aliyeteuliwa na mwenye cheo au kilinyanganywa kwa njia ya kijeshi.

Wafuasi wa Muawiya waliendelea kutawala hadi 750 walipopinduliwa na wafuasi wa Abbas mjomba wa mtume Muhammad. Mmuawiya mmoja tu aliweza kukimbia hadi sehemu ya Hispania iliyotekwa na Waarabu alipopokelewa kwa heshima na kuanzisha Ukhalifa wa Wamuawiya wa Cordoba uliodumu katika Hispania hadi 1031.

                                     

2.2. Wamuawiya, Waabbasi na Waosmani Waosmani

Watawala Waosmani hawakujali sana cheo cha khalifa. Walijiita hasa "Sultani" pamoja na vyeo vingine. Walitumia cheo cha khalifa hasa katika uhusiano na Waislamu nje ya dola lao. Kwa mafano wakishambulia nchi za Kiislamu kama Uajemi walijiita Khalifa wakidai utii kama wakuu wa Waislamu wote. Au wakishambuliwa na Austria au Urusi walitumia cheo cha khalifa kuita Waislamu wote kujiunga na jihad ya kivita.

Safari ya mwisho ya kutumia cheo cha khalifa kwa wito la jihad ya kivita ilitokea wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ambako Sultani Mehmed V alitumia tena cheo chake cha khalifa kuita waislamu wote wa dunia kujiunga na vita dhidi ya Uingereza.

                                     

2.3. Wamuawiya, Waabbasi na Waosmani Mwisho wa ukhalifa

Baada ya vita cheo kilifutwa na bunge la Uturuki kwa mapendekezo ya Atatürk mwaka 1924.

                                     

2.4. Wamuawiya, Waabbasi na Waosmani Khalifa mbalimbali wa kihistoria

Nje ya ufuatano rasmi ya makhalifa kulitokea pia cheo cha khalifa katika maeneo mbalimbali kwa kushhindana na khalifa rasmi ni nani mwenye cheo cha kweli.

Mifano ni:

  • Makhalifa Wafatima wa Shia katika Misri na Afrika ya Kaskazini 909-1171.
  • makhalifa wa Sudan: viongozi waliomfuata Muhammad Ahmad ibn Abd Allah Al-Mahdi waliitwa kwa cheo "khalifa".
  • Khalifa wa Sokoto alikuwa kiongozi wa milki iliyoundwa na Uthman dan Fodio mnamo mwaka 1804 katika kaskazini ya Nigeria ya leo
  • Makhalifa wa Muwahidun katika Afrika ya Kaskazini na Hispania ya Kiislamu 1145-1269.
  • Makhalifa wa Ahmadiyya - waliomfuata Hazrat Mirza Ghulam Ahmad kama kiongozi wa Ahmadiyya huitwa "khalifa". Tangu 22 Aprili 2003 Hazrat Mirza Masroor Ahmad amekuwa "khalifatul masih V) khalifa wa tano wa Messia.
                                     

3. Majaribio ya kukufusha ukhalifa

Tangu mwaka huu walijitokeza viongozi wa vikundi mbalimbali waliodai cheo cha khalifa lakini bila kukubaliwa na Waislamu wengi.

  • Mfano mmojawapo ni kundi la Mturuki Cemaleddin Kaplan alijejitangaza kuwa khalifa. Alikuwa na wafuasi maelfu kadhaa kati ya Waturuki nchini Ujerumani. Baada kifo chake mashindano juu ya cheo kilisababisha kuuawa kwa mfuasi mmoja na kikundi kilipigwa marufuku na serikali ya Ujerumani.
  • Tarehe 29 Juni 2014 kiongozi wa kundi la Daish Dola la Kiislamu katika Iraqi na Shamu alijitangaza kuwa khalifa akidai Waislamu wote duniani kumtii. Tangazo la ukhalifa lilikuwa sababu kwa vikundi vingine vikali kama vile Al Qaida kuwa adui zake.
  • Kati ya Waislamu wenye mwelekeo mkali kuna mafundisho ya kwamba cheo cha khalifa kinapaswa kurudishwa kama utaratibu wa kisiasa cha kufaa. Mfano wake ni chama cha Hizb ut-Tahrir kilichopigwa marufu katika nchi zote.