Back

ⓘ Mashauri ya Kiinjili
Mashauri ya Kiinjili
                                     

ⓘ Mashauri ya Kiinjili

Mashauri ya Kiinjili ni maelekezo ambayo yanapatikana katika Injili lakini hayamlazimishi mfuasi wa Yesu kuyafuata.

Yanategemea maisha na mafundisho yake kadiri ya Agano Jipya.

Yanatolewa kwa hiari ya mtu atakayevutiwa nayo moyoni mwake kutokana na Roho Mtakatifu kumjalia karama ya namna hiyo.

Maarufu zaidi ni yale matatu ambayo ni kiini cha maisha ya utawa hasa katika Kanisa Katoliki: useja mtakatifu, ufukara na utiifu ufafanuzi wake kwa mashirika yote unatolewa katika Mkusanyo wa Sheria za Kanisa la Kilatini, kanuni 599–601.

                                     

1. Viungo vya nje

  • Mashauri ya Kiinjili katika Catholic Encyclopedia.
  • Sehemu juu ya Maisha ya wakfu katika Mkusanyo wa Sheria za Kanisa la Kilatini, 1983, ikiwa pamoja na kanuni 599-601 kuhusu Mashauri ya Kiinjili.