Back

ⓘ Zumbe
                                     

ⓘ Zumbe

Zumbe ni neno la kisambaa linaloonyesha heshima na uthamani wa mtu, maana yake halisi kwa kisambaa ni Mfalme. Kiongozi wa wasambaa aliitwa Zumbe kama cheo chenye sifa kubwa kwa jamii hiyo. Huko usambaani neno Zumbe pia hutumika kama salamu tangulizi unapogonga kwenye nyumba ya mtu kwa ajili ya kusalimia, yaani lazima utangulize zumbe kwa ajili ya heshima ya baba mwenye nyumba. Katika siku za karibuni huko Usambaani, neno zumbe linatumika kumuonyesha mtu aliye na hali nzuri kimaisha au kimapato. Mfano mtu anapokuwa na hali zuri kimaisha wasambaa kumuita zumbe, yaani wakimaanisha mtu mwenye heshima au anayethaminika katika jamii.

Asili ya neno no cheo cha "jumbe" kwa Kiswahili kinachomtaja mkuu au mtawala wa kieneo.