Back

ⓘ Mkaapweke
                                               

Dominiko wa Calzada

Dominiko wa Calzada alikuwa padri mkaapweke aliyehudumia hadi kifo chake waumini walioelekea Santiago de Compostela kwa hija. Kabla ya hapo alijaribu kujiunga na monasteri mbalimbali akakataliwa kwa sababu ya ulemavu wa viungo vyake na udogo wa akili yake. Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 12 Mei.

Mkaapweke
                                     

ⓘ Mkaapweke

Katika Ukristo asili ya maisha hayo ni jangwa la Misri katika karne ya 3 na hasa ya 4. Paulo Mthebani + 250 hivi ni wa kwanza kujulikana.

Antoni Abati, mmoja kati ya wale waliovutiwa naye, alijivutia umati wa wafuasi kusini mwa Misri: kutoka huko wakaapweke walienea kote mashariki mwa Dola la Roma, hasa Palestina Ilarioni, Kapadokia Basili Mkuu na Gregori wa Nazianzo.

Wengi kati ya hao wa kwanza wanajulikana kati ya mababu wa jangwani.

Baada ya Pakomi + 318 hivi kuanzisha maisha ya kijumuia kwa watawa na kuwatungia kanuni ya kwanza, mtindo huo ulizidi kuenea usifute kabisa ukaapweke.

Ukaapweke ulienea pia magharibi hasa kutokana na kitabu cha Atanasi wa Aleksandria juu ya Antoni na kile cha Jeromu juu ya Paulo; kuanzia karne ya 4 Africa kaskazini magharibi na Ulaya pia walipatikana wakaapweke, hasa Gallia, Britain na Ireland.