Back

ⓘ Jamii:Mungu




                                               

Huruma ya Mungu

Huruma ya Mungu ni sifa kubwa ya Mwenyezi Mungu ambayo inatangazwa katika dini mbalimbali, hususan Uyahudi, Ukristo na Uislamu. Biblia na Kurani zinalingana katika kusisitiza ubora wa sifa hiyo.

                                               

Trimurti

Trimurti ni fundisho katika dini ya Uhindu linaloonyesha miungu mikuu mitatu kama nguvu moja ya kimungu au kwa lugha nyingine miungu mikuu kama maumbo tofauti ya nguvu moja ya kimungu. Jina latokana na maneno ya Kisanskrit "tri" maana yake "tatu" na "murti".

                                               

YHWH

YHWH ni herufi nne ambazo kwa Kiebrania zinaandikwa יהוה. Ni konsonanti zinazounda jina la Mungu lililo muhimu kuliko yote linalopatikana mara 6.828 hivi katika Biblia ya Kiebrania kuanzia Mwa 2:4. Jina hilo halipatikani kabisa katika vitabu vya Wimbo Ulio Bora, Kitabu cha Mhubiri na Kitabu cha Esta.

Allah
                                               

Allah

Allah ni neno la Kiarabu linalorejea Mungu pekee., muumba wa mbingu, dunia na vyote vilivyomo. Hasa linatumika katika dini ya Uislamu, lakini pia Wayahudi wanaoongea Kiarabu na Wakristo Waarabu na wa nchi nyingine kama vile Malaysia wanamwita Mungu "Allah" tangu kabla ya Mtume Muhammad. Hata dini za Bahai na Kalasinga zinamuita Mungu hivyo.

Yohana 3: 16
                                               

Yohana 3: 16

Yohana 3:16 ni mstari ule wa Injili ilivyoandikwa na Yohana Mtakatifu unaodondolewa mara nyingi kabisa. Wakristo wengi wanauangalia kama muhtasari wa ujumbe wa Injili kuhusu Mungu na Yesu Kristo. Katika tafsiri ya Habari Njema, mstari huo unasema: "Maana Mungu aliupenda ulimwengu hivi hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele".