Back

ⓘ Maadili ya utafiti
Maadili ya utafiti
                                     

ⓘ Maadili ya utafiti

Maadili ya utafiti yanahusu msingi wa kanuni za kimaadili kwa mada mbalimbali yanayohusiana na utafiti wa kisayansi, hivyo matumizi ya kanuni adilifu katika mada mbalimbali zinazohusu binadamu. Hizi ni pamoja na kubuni na kutekeleza utafiti juu ya binadamu na wanyama, nyanja mbalimbali za kashfa za kielimu pamoja na makosa ya kisayansi, kujulisha makosa; udhibiti wa utafiti, nk.

Maadili ya utafiti yaliendelea pakubwa kama dhana katika utafiti wa tiba. Mkataba muhimu hapa ni Tamko la 1974 la Helsinki. Nurenberg Code ni mkataba wa awali, lakini bado una mipasho ya maana. Utafiti katika sayansi ya jamii unawakilisha masuala kadhaa tofauti na yale ya utafiti wa matibabu.

Nyanja ya utafiti wote wa kisayansi umejengwa kwenye msingi wa uaminifu. Wanasayansi huwa na imani kuwa matokeo yaliyoripotiwa na wengine ni halali. Jamii huamini kwamba matokeo ya utafiti huonyesha jaribio lenye uaminifu la wanasayansi kueleza dunia kwa usahihi na bila upendeleo. Lakini uaminifu huu utaendelea tu kama jamii ya kisayansi itajitolea yenyewe kueneza maadili ya kisayansi yanayohusiana na vitendo vya kimaadili.

Kuna masuala mengi ya kimaadili ambayo yanafaa yatiliwe maanani kwa utafiti. Wasomi wa jamii wanahitaji kufahamu kuwa wana jukumu la kulinda usalama wa kupatiana ruhusa halisi na kujua malengo ya wale wote wanaoshiriki katika utafiti. Hawapaswi kutumia vibaya taarifa wanazopata, na kunafaa kuwe na jukumu la kimaadili fulani linalofaa kuchukuliwa kwa washiriki. Kuna wajibu wa kulinda haki za watu katika masomo hayo na vilevile siri na usikivu. Usiri wa wale wanaohusika katika uchunguzi lazima ufanyike, kuweka siri zao na kutokujulikana salama. Kama inavyodokezwa katika BSA for Sociology, maadili haya yote lazima yaheshimiwe isipokuwa kama kuna sababu nyingine kuu za kutofanya hivyo - kwa mfano, shughuli za kigaidi au zilizopigwa marufuku.

Maadili ya utafiti katika muktadha wa matibabu yamejaa principalism, mbinu ambayo imekosolewa kuwa nje ya muktadha.

                                     

1. Masuala muhimu

Matokeo ya utafiti katika machapisho, idadi ya masuala muhimu ni pamoja na:

 • Viwango vya kimaadili. Majarida ya karibuni ya tahariri yaliashiria uzoefu wa shughuli zisizofaa.
 • Uandishi. Nani anaweza kudai haki ya uandishi? Ni mpangilio upi unafaa waandishi kutajwa?
 • Mchakato wa Mapitio. Mapitio ya mchakato huchangia kudhibiti ubora na ni hatua muhimu kujua uhalali wa utafiti
 • Uaminifu. Uaminifu na uadilifu ni wajibu wa kila mwandishi na mtu, mtaalam na mwanachama wa bodi la kuhariri.
                                     

2. Viungo vya nje

 • Archived Novemba 16, 2007 at the Wayback Machine.
 • Johns Hopkins Program katika maadili ya Utafiti Archived Julai 16, 2011 at the Wayback Machine.
 • Shughuli za Kimaadili: Kanuni na Miongozo ya Utafiti na Watu walio hatarini na Familia Archived Desemba 8, 2008 at the Wayback Machine. Itifaki yenye maadili kwa utafiti wa sayansi ya jamii iliyotengenezwa na Kituo cha Watoto na Familia katika Mfumo System
 • TRREE-kwa Afrika inapatia rasilimali kwa lugha kadhaa na mpango wa mafunzo ya bure kuhusu maadili ya utafiti na kanuni ikilenga sana Afrika Kusini kwa Sahara.
 • Scientists Global Responsibility UK
 • Tamko la Sera la Tri-Council Kanada Archived Septemba 19, 2008 at the Wayback Machine.
 • Mitaala ya mafunzo kuhusu Maadili ya utafiti umeandaliwa na, Family Health International FHI, ikilenga majaribio kutumiabinadamu
 • INES Global
 • ics/research.htm Maadili ya utafiti sehemu ya tovuti ya SHiPS S Sociology, Historia na F alsafa S ya Sayansi inapatiana baadhi ya rasilimali muhimu, pamoja na tafiti zinazohusiana na makosa kadhaa ya kisayansi
 • Archived Novemba 7, 2009 at the Wayback Machine.
 • ResearchEthics.ca
 • UNESCO - Maadili ya Sayansi na Teknolojia
 • Mkusanyiko wa majarida yaliyopitiwa upya na walio kwenye taaluma moja kuhusu historia ya matumizi ya udanganyifu katika utafiti, vilevile juu ya historia ya majaribio ya maadili.
 • The Hinxton Group: Kongamano la kimataifa kuhusu seli za Stem, Maadili & Sheria