Back

ⓘ Maana ya maisha
Maana ya maisha
                                     

ⓘ Maana ya maisha

Maana ya maisha ni mojawapo kati ya masuala makuu kuhusu thamani, madhumuni na umuhimu wa binadamu kuwepo duniani na wa maisha kwa jumla. Suala hilo linaweza kujitokeza katika maswali mengi tofauti yanayohusiana, kama vile Mbona tumekuwepo?, Maisha yanahusu nini? na Ni nini maana ya haya yote?

Binadamu anajiuliza maswali kama hayo hasa anapokabiliana na kifo, kwa mfano msiba wa ndugu au rafiki.

Limekuwa suala kuu la udadisi wa sayansi, falsafa na teolojia tangu zamani. Kumekuwa na idadi kubwa ya majibu kwa maswali hayo kutoka asili mbalimbali kiitikadi na kiutamaduni.

Maana ya maisha imechanganyikana kwa undani na dhana za falsafa na imani za dini na hugusia masuala mengine mengi, kama vile ontolojia, tunu, kusudi, maadili, hiari, uwepo wa Mungu, roho, na kinachoendelea baada ya maisha haya kwisha.

Michango ya sayansi kawaida ni ya moja kwa moja na inaeleza uhalisia kutokana na mambo yanayopimika kuhusu ulimwengu; sayansi inatoa muktadha na mipaka kwa mazungumzo kuhusu mada zinazohusika.

Mbadala ni mtazamo wa kifalsafa unaokabili swali: "Ni nini maana ya maisha yangu?" Thamani ya swali linalohusu kusudi la maisha huweza kuwiana na kuupata ukweli wa mwisho, au hisia za umoja na utakatifu.

                                     

1. Maswali na marejeo yake

Maswali kuhusu maana ya maisha yameulizwa kwa njia mbalimbali zenye upana, yakiwemo yafuatayo:

 • Maana ya maisha ni nini? Nini maana ya haya yote? Sisi ni nani?
 • Kwa nini tumekuwepo? Sababu ya sisi kuwa hapa ni nini?
 • Asili ya uhai ni nini?
 • Hali ya maisha ni nini? Ukweli ni nini?
 • Madhumuni ya maisha ya mtu ni nini?
 • Maana ya maisha ni nini?
 • Cha maana na cha thamani maishani ni nini?
 • Thamani ya maisha ni nini?
 • Sababu ya kuishi ni nini? Kwa nini tunaishi?
                                     

2. Uchunguzi wa kisayansi

Kwamba sayansi inaweza kutusaidia kuelewa zaidi masuala ya msingi kama vile maana ya maisha inazua mabishano mengi katika jamii za sayansi na falsafa ya sayansi.

Hata hivyo, sayansi inaweza kutupa muktadha fulani na huyaweka mipaka kadhaa mazungumzo kuhusu mada kama hizo.

                                     

2.1. Uchunguzi wa kisayansi Umuhimu wa kisaikolojia na thamani katika maisha

Sayansi huenda ikashindwa kutuambia nini ni cha thamani maishani, lakini baadhi ya fani zake hugusia maswali yanayohusiana: watafiti katika saikolojia chanya hutafuta sababu zinazoleta hali ya ndani ya kuridhika na maisha, kujihusisha kikamilifu katika shughuli, kutoa mchango mkubwa zaidi kwa kutumia vipawa vya binafsi,n.k.

Aina moja ya mfumo wa thamani iliyopendekezwa na wataalamu wa elimunafsia ya jamii, iitwayo kwa upana "Nadharia ya Kupambana na Mambo ya Kutisha", inasema kwamba maana yote ya binadamu inatokana na hofu ya msingi ya kifo, ambapo maadili yanachaguliwa yanapotusaidia kuepukana na kumbukumbu ya kifo.

Sayansi ya nyurolojia imetunga nadharia ya malipo, raha na msukumo katika masuala ya kimwili kama shughuli za kupitisha ujumbe za kinyuro. Ikiwa mtu anaamini kwamba maana ya maisha ni kufanya raha ziwe nyingi iwezekanavyo, basi nadharia zinatoa utabiri unaozidi kuongezeka, kuhusu jinsi ya kufanya ili kufanikisha hilo.

Somo la kijamii linapima thamani katika ngazi ya kijamii kwa kubuni nadharia kama vile nadharia ya thamani kanuni n.k.                                     

2.2. Uchunguzi wa kisayansi Asili na hali ya maisha kibiolojia

Nadharia ya mageuko ya spishi haijaribu kuelezea asili ya uhai, bali mchakato ambao viumbe tofauti vimepitia katika kipindi chote cha historia ya dunia kupitia mabadiliko ya ghafla ya kijenetikia na uteuzi wa kiasili Mwishoni mwa karne ya 20, kwa kuzingatia ufahamu wa mabadiliko ya viumbehai unaotegemea jeni hasa, wanabiolojia George C. Williams, Richard Dawkins, David Haig na wengineo, walihitimisha kwamba ikiwa kuna kazi msingi ya maisha, ni kujinakilisha kwa DNA na kuendelea kuwa hai kwa jeni za mtu.

Ingawa wanasayansi wameyachunguza maisha yalivyo duniani, kuyafafanua bayana bado ni changamoto.

Wanabiolojia kwa jumla wanakubaliana kwamba viumbe mbalimbali ni mifumo inayojipanga inayosimamia mazingira ya ndani ili kudumisha hali hii ya mpango, shughuli za kimetaboli hutumika kutoa nishati, na uzazi unaruhusu uhai kuendelea kwa vizazi vingi. Kwa kawaida, umbile huwa sikivu kwa uchochezi na habari za kijenetikia, hivyo huelekea kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi ili kuruhusu marekebisho kupitia mabadiliko ya mwili. Sifa hizo huongeza nafasi ya kuishi ya kiumbe binafsi na wazao wake kwa mtiririko huo.

Viwakala visivyokuwa vya seli vinavyozaana, hasa virusi, kwa jumla havitazamwi kama viumbehai kwa sababu haviwezi kuzaana kwa "kujitegemea" au kuendesha shughuli za kimetaboliki. Pambano hilo ni tatizo, ingawa baadhi ya vimelea na visimbayonti vya ndani ya mwili pia vinaweza kuishi kwa kujitegemea.

Astrobiolojia inajihusisha na uwezekano wa kuwa na aina tofauti ya viumbe hai katika ulimwengu mwingine, kama vile miundo ya kujinakilisha kutoka vifaa vingine visivyo DNA.

                                     

2.3. Uchunguzi wa kisayansi Asili na hatima ya ulimwengu

Ingawa dhana ya Mlipuko mkuu ilipotolewa mara ya kwanza ilipambana na shaka kwa wingi, pia kutokana na uhusiano na imani ya dini ya uumbaji, baadaye imekuja kuungwa mkono na uchunguzi kadhaa wa kujitegemea. Hata hivyo, fizikia ya sasa inaweza kuelezea tu ulimwengu ulivyokuwa mapema, sekunde 10 baada ya kutokea. Wanafizikia wengi wamedadisi nini inaweza kuwa imetangulia, na jinsi ulimwengu ulivyoanza. Baadhi ya wanafizikia hudhani kuwa Mlipuko mkuu ulitokea kwa bahati tu, pamoja na uwepo wa ulimwengu maridhawa.

Hata hivyo, haijalishi jinsi ulimwengu ulivyokuja kuwepo, hatima ya binadamu katika ulimwengu huu ni maangamizi kwani - hata kama ubinadamu utaishi muda mrefu - uhai wa kibiolojia hatimaye yatashindwa kujiendeleza.

                                     

2.4. Uchunguzi wa kisayansi Maswali ya sayansi kuhusu akili

Hali ya kweli na asili ya fahamu na akili yenyewe pia vinajadiliwa sana katika sayansi. Suala la hiari pia linaonekana kuwa na umuhimu wa msingi. Masuala hayo hupatikana zaidi katika nyanja za sayansi koginitivu, nyurolojia na falsafa ya akili, ingawa baadhi ya wanabiolojia wa maendeleo ya uhai na wanafizikia wa kinadharia pia wameliashiria sana suala hilo. mara nyingi zikijumuisha idadi kubwa ya mitazamo ya ziada.

Mbinu nyingine, kwa vile Mfano wa Rasimu Nyingi, hudai kwamba fahamu inaweza kuelezwa kikamilifu na nyurolojia, kupitia utendaji kazi wa ubongo na nyuroni zake.

Nadharia za sumakuumeme za fahamu zinasema eneo la sumakuumeme linalotokana na ubongo ndilo hasa linalobeba fahamu zoefu. Hata hivyo kuna kutokubaliana kuhusu kutekelezwa kwa nadharia kama hiyo inayohusu utendaji kazi kwingine kwa akili.

Nadharia za akili za kikwontamu hutumia nadharia ya kwontamu kuelezea baadhi ya sifa za akili.

Ikitegemea hoja ya maelezo ya akili yasiyoweza kugusika, baadhi ya watu wamependekeza uwepo wa fahamu ya kikosmiki, wakidai kwamba fahamu kwa kweli ndiyo "msingi wa yote kuwepo". Wanaounga mkono mtazamo huo wanaelezea matukio yasiyo ya kawaida, hasa uwezo wa kuhisi usio wa kawaida na uwezo wa kuyasoma mawazo, kama ushahidi wa uwepo wa fahamu ya juu isiyoeleweka. Ili kuthibitisha uwepo wa mambo hayo yasiyo ya kawaida, wanaelimunafsia wa mambo yasiyo ya kawaida wamefanya majaribio mbalimbali. Uchambuzi unaoangalia mambo yote yaliyopo unaonyesha kuwa asilimia ya wenye nguvu zisizo za kawaida ingawa ndogo sana imebaki thabiti. Ingawa baadhi ya wachambuzi wakosoaji wanahisi somo la elimunafsia isiyo ya kawaida kuwa sayansi, hawaridhishwi na matokeo ya majaribio yake. Wanaochunguza mambo haya upya, wanabaki na wasiwasi kwamba matokeo yanayoonekana kuwa na mafanikio huenda yakawa yanatokana na utaratibu mbaya, na watafiti wasiokuwa na mafunzo ya kutosha, au mbinu hafifu.                                     

3. Mitazamo ya kifalsafa

Mitazamo ya falsafa kuhusu maana ya maisha ni itikadi ambazo huelezea maisha kupitia suala la maadili au dhana zinazofafanuliwa na binadamu.

Upanthei wa kiasilia

Kulingana na upanthei wa kiasilia, maana ya maisha ni kutunza viumbe na mazingira.

                                     

3.1. Mitazamo ya kifalsafa Uplato

Plato alikuwa mmoja wa wanafalsafa wa mwanzo, na mwenye ushawishi mwingi hadi leo, hasa kwa uhalisia kuhusu uwepo wa malimwengu. Katika Nadharia ya Maumbo, malimwengu hayapo kimwili, lakini yapo katika maumbo ya kimbingu. Katika Jamhuri mazungumzo ya mhusika wa mwalimu wake Sokrates yanaelezea Umbo la Zuri, jambo la kimaadili, hali kamili ya uzuri, hivyo basi kipimo cha ujumla cha haki. Katika falsafa ya Plato, maana ya maisha ni kufikia umbo la juu zaidi la elimu, ambalo ni Umbo la Zuri, ambapo mambo yote mema na ya haki yanatoa umuhimu na thamani. Binadamu wana wajibu wa kuyatekeleza mazuri, lakini hakuna yeyote anayeweza kufanikiwa katika harakati hiyo bila fikira za kifalsafa, ambazo zinaruhusu elimu ya kweli.

                                     

3.2. Mitazamo ya kifalsafa Uaristoteli

Aristotle, mwanafunzi wa Plato, alikuwa mwanafalsafa mwingine wa mapema, mwenye ushawishi mkubwa, ambaye alisema kuwa maarifa ya maadili si ya hakika kama metafizikia na somo la maarifa, lakini ni maarifa ya kijumla. Kwa sababu si fani ya kinadharia, inambidi mtu asome na afanye mazoezi ili awe mzuri, kwa hiyo mtu angekuwa mwema, hangeweza kusoma tu fadhila ni nini, ingembidi awe na fadhila, kupitia juhudi za kiadili. Kufanya hili, Aristotle alifafanua kitendo kilicho cha fadhila: "Kila tajriba na kila swali, na vilevile kila tendo na chaguo la tendo, linadhaniwa kuwa na uzuri fulani kama lengo lake. Ndiyo sababu lile zuri limefafanuliwa ifaavyo kama lengo la bidii yote cha kiumbe cha kibiolojia kinachoendesha shughuli zake katika muktadha wa kijamii na wa kiutamaduni."

Watu huamua kusudi la binadamu, bila ya ushawishi wa Kimungu; ni tabia ya binadamu, hisia ya kijumla, ambayo ni lengo la maisha ya binadamu. Utu wa Kidunia unataka kuendeleza na kutimiza ubinadamu: "Utu husisitiza uwezo wetu, na uwajibikaji wetu, kuishi maisha adili yenye utimilifu wa binafsi yanayolenga mema makuu ya ubinadamu". Wanautu huendeleza kufunguliwa kifikra ili kuyashughulikia maslahi ya binafsi na yenye manufaa kwa watu wote. Furaha ya mtu binafsi inahusishwa kwa njia isiyoweza kubadilishwa na ustawi wa binadamu wengine, kwa sababu sisi ni wanyama wanaolazimika kuishi katika jamii, ambayo hupata maana kutokana na uhusiano wa karibu, na kwa sababu maendeleo ya kiutamaduni humnufaisha kila mtu katika utamaduni.

Falsafa ndogo za Utu wa Baadaye na Utu Unaopita Yote ambazo wakati mwingine hutumiwa kimbadala ni upanuzi wa maadili ya kiutu. Mtu anapaswa kutafuta maendeleo ya ubinadamu na ya maisha yote kwa kiasi kikubwa iwezekanavyo ili kupatanisha Utu wa Kirainasansi na utamaduni wa karne ya 20 wa sayasansi na teknolojia. Hivyo, kila kiumbe hai ana haki ya kuamua "maana ya maisha binafsi" kwa mtazamo wa kijamii na kibinafsi. Kutoka mtazamo wa kiutu na kielimunafsia ya kupunguza maumivu, suala la maana ya maisha pia linaweza kutafsiriwa tena kama "Ni nini maana ya maisha "yangu"?"

Badala ya kujifunga na swali la kidini au la kikozmiki kuhusu madhumuni makuu, mbinu hii inapendekeza kwamba swali hili ni la binafsi sana. Kuna majibu mengi ya kimatibabu ya kupunguza maumivu kwa swali hili, kwa mfano Viktor Frankl anadokeza kuwa dhana ya "Kutowaza", ambayo kwa kiasi kikubwa hutafsiriwa kama kukoma kutafakari bila mwisho juu ya ubinafsi, badala ya kujishughulisha na maisha. Kwa ujumla, mwitikio wa matibabu ya kuyapunguza maumivu ni kwamba swali la maana ya maisha huvukiza ikiwa mtu anajishughulisha kikamilifu na maisha. Swali kisha linabadilika kuwa wasiwasi maalum zaidi kama vile "Ni upotovu upi unaonisumbua?", "Ni nini kinachozuia uwezo wangu kufurahia vitu?", "Mbona mimi huwasahau wapendwa wangu?". Angalia pia Matibabu ya Kupunguza Maumivu ya Kidhanaishi kadiri ya Irvin Yalom.

                                     

3.3. Mitazamo ya kifalsafa Baada ya Usasa

Falsafa ya Baada ya Usasa - tukizungumza kwa upana- inaona hali ya binadamu ikiwa kama iliyojengwa na lugha, au na miundo na taasisi za jamii ya kibinadamu. Ikitofautiana na aina nyingine za falsafa, ni nadra kwa falsafa ya Baada ya Usasa kutafuta maana zinazopatikana kabla ya tendo au zilizojikita kwa undani katika uwepo wa binadamu. Badala yake inalenga kuchunguza au kukosoa maana zilizopewa ili kuzitafakari au kuzirekebisha upya. Chochote kinachofana na maana ya maisha, katika maana ya falsafa hiyo, kinaweza kueleweka tu ndani ya muundo wa kijamii na wa kilugha, na lazima ufuatwe kama kimbilio kutoka miundo ya nguvu ambayo tayari imejikita katika aina zote za hotuba na mwingiliano.

Kama kanuni, wanafalsafa wa Baada ya Usasa wanatazama mwamko wa vikwazo vya lugha kama muhimu kuvikwepa vikwazo vivyo, lakini wananadharia tofauti wana maoni mbalimbali kuhusu asili ya mchakato huu: kutoka ujenzi wa dharura wa maana na watu binafsi kama katika falsafa ya Kuharibu Yaliyojengwa hadi kwa nadharia ambamo watu ni upanuzi wa kimsingi wa lugha na jamii, bila uhuru halisi kama katika falsafa ya Baada ya Muundo. Kiujumla, falsafa ya Baada ya Usasa inatafuta maana kwa kuangalia miundo ya msingi ambayo inaunda au kulazimisha maana, kuliko yale yanayoonekana kiepifenomenali duniani.                                     

3.4. Mitazamo ya kifalsafa Dhana ya Uhisia

Kulingana na dhana ya kihisia, maana kuu ya maisha ni kupata kutosheleza hisia za kibinadamu. Wafuasi wa falsafa hiyo wanaamini kuwa vitendo vyote maishani ni matokeo ya hisia na hasa haja ya kuzaa. Uwepo wa mtu binafsi huwa chanzo cha kuzaa na unamfanya binadamu kutafuta lengo la kuzaa maishani kwa kuufuata mzunguko. Haraka inasisitiza kuwa watu wanapofikiria kwa kina, watapata kuwa lengo kuu la matendo yote wafanyayo ni kuvutia watu wa jinsia nyingine. Dhana kuu ya uhisia inaweza kufuatwa hivi:

Kama inayokubalika kuwa watu hufunzwa kujifunza shuleni. Kwa nini tusome kwa bidii? Ili tufuzu mitihani. Kwa nini tufuzu mitihani? Ili tuweze kuenda chuo kikuu? Kwa nini tuweze kuenda chuo kikuu? Ili tuweze kupata kazi nzuri? Kwa nini tupate kazi nzuri? Ili tuwe na mali. Kwa nini tuwe na mali? Ili tununue magari mazuri; ili tununue nyumba nzuri; ili tununue bidhaa nzuri. Kwa nini vitu vyote vizuri kumfanya mtu aonekana mzuri? Mwishowe kuvutia watu wa jinsia nyingine, kutosheleza haja ya msingi ya kuzaa na kuendeleza familia ya kibinadamu.

Wanahisia hutumia mawazo hayo kuendeleza dhana kuwa matukio yote ya kibinadamu yanaweza kuelezwa kwa kutumia lengo letu la kuzaa: Kwa nini watu wanapinga sana ndoa baina ya watu wa jinsia moja? Kwa sababu watu katika jozi la namna hiyo hawawezi kuzaa Kwa nini watu hupendana? Kwa sababu upendo husababisha ngono, ambayo huchangia ustawi wa spishi ya binadamu Kwa nini akina mama hupenda watoto hata kama hawajazaliwa bado? Kwa sababu inachangia kutunza na kuongeza idadi ya binadamu Kwa nini watu wengi hupinga utoaji mimba? Kwa sababu inazuia uzazi Kwa nini madaktari wengi sana na matibabu mengi? Ili kutunza idadi ya watu Kwa nini uuaji ni hatia kubwa sana? Kwa sababu kuua kunapunguza idadi ya watu

                                     

3.5. Mitazamo ya kifalsafa Upanthei wa kiasilia

Kulingana na upanthei wa kiasilia, maana ya maisha ni kutunza viumbe na mazingira.

                                     

4.1. Mitazamo ya kidini Falsafa za Kihindu

Uhindu ni jamii ya kidini inayojumuisha itikadi na desturi nyingi. Kwa sababu Uhindu ulikuwa njia ya kuonyesha maisha yenye maana tangu jadi, wakati ambapo hapakuwa na haja ya kutaja Uhindi kama dini tofauti, mafundisho ya Uhindu ni nyongeza na yanayowiana kiasili, kiujumla yasiyo ya kipekee, yenye kudokeza tu na yenye maudhui ya kuvumiliana.

Wengi wanaamini kwamba ātman roho, nafsi, nafsi ya kweli ya mtu, ni ya milele. Kwa sehemu, hili linatokana na imani ya Kihindu kwamba maendeleo ya kiroho hufanyika katika maisha mengi, na malengo yanafaa kuwiana na hali ya maendeleo ya mtu binafsi. Kuna malengo manne ya maisha ya binadamu, yanayojulikana kama purusharthas yamepangwa kuanzia lile dogo zaidi hadi lile kuu: Kama kazi, upendo na radhi ya kingono, Artha mali, Dharma haki, maadili, na Moksha ukombozi kutoka mzunguko wa kuzaliwa upya.

Katika shule zote za Uhindu, maana ya maisha imefungwa ndani ya dhana za karma kitendo chenye matokeo, samsara mzunguko wa kuzaliwa na kuzaliwa upya, na moksha ukombozi. Kuwepo kunaaminika kuwa maendeleo ya atman kupitia vipindi vingi vya maisha, na maendeleo yake ya mwisho kuelekea ukombozi kutoka karma. Malengo hasa ya maisha kwa jumla husongeshwa chini ya mazoea pana ya yoga au dharma kuishi kisahihi ambayo yanakusudiwa kujenga kuzaliwa kupya kuzuri zaidi, ingawa hayo pia kwa ujumla ni matendo chanya katika maisha haya. Shule za jadi za Uhindu mara nyingi huabudu Madeva ambao ni dhihirisho ya Ishvara Mungu wa kibinafsi au wa kuchaguliwa.

                                     

4.2. Mitazamo ya kidini Uhindu wa Advaita na Dvaita

Shule za baadaye zilizitafsiri upya veda kuzingatia Brahman, "Yule Asiye na Wa Pili", kama kielelezo muhimu kinachomfanana Mungu.

Katika Advaita Vedanta ya kimoni, atman hatimaye haitofautishwi na brahman, na lengo la maisha ni kujua au kutambua kwamba nafsi ya mtu ya atman inafanana na Brahman.

Kwa Maupanishadi, yeyote anayefahamu kikamilifu atman, kama msingi wa ubinafsi, anajitambua na Brahman, na hivyo, anapata Mokasha ukombozi, uhuru.

Dvaita Vedanta yenye pande mbili na shule zingine za bhakti zina tafsiri yenye pande mbili. Brahaman anaonekana kama kiumbe kikuu chenye tabia na sifa wazi. Atman inategemea Brahman kwa kuwepo kwake; maana ya maisha ni kupata Moksha kupitia upendo wa Mungu na neema yake.

                                     

4.3. Mitazamo ya kidini Uvaishnavi

Tawi lingine la Uhindu ni Uvaishnavi, ambapo Vishnu ndiye Mungu mkuu. Si shule zote za Uvaishnavi hufunza maana ya maisha, lakini Gaudiya Vaishnavism, kwa mfano, hufunza Achintya Abheda inayomaanisha Kumuabudu Mungu tofauti na Mungu pekee wa kweli na wakati huo ikitambua umoja muhimu wa nafsi zote, huku viumbe vyote hai ni sehemu za milele za Mungu mkuu aitwaye Krsna.

Mtazamo wa kikatiba wa kiumbe hai ni kumtumikia Mungu na upendo na kujali. Huduma bila malipo isiyositishwa na isiyosukumwa na chochote kwa Krsna na wafuasi wake ndiyo maana ya maisha katika hali uhuru. Sisi tupo katika Dunia ya kinafsi tukimtumikia Krsna kwa furaha huku tukifahamu vyema kuwa sisi ni roho za kinafsi na tunayo maisha ya milele. Kwa sababu ya kumchukia Krsna na kwa sababu ya mapenzi yetu ya kutaka kuwa na anasa m,bali na Krsnatupo katika Dunia hii ambapo tunapitia mzunguko unaojirudiarudia wa kuzaliwa, magonjwa, uzee na kifo katika miili tuliyopata ya spishi 8.4 za kimaisha, tukihama kutoka mwili mmoja hadi mwingine kulingana na karma yetu na mapenzi yetu.

Lengo la maisha ya binadamu haswa ni kufikiria zaidi ya njia ya kinyama ya kula, kulala, kufanya mapenzi na kulinda na kufuata akili ya juu zaidi ili kuanzisha upya uhusiano na Krsna, Baba yetu wa milele, ambaye kutoka kwake vyote vilitoka, ambaye ndiye mwezeshaji na mwenye kuangamiza. Maandiko yaliyoonyehswa kwetu kama vile Bhagavad-Gita na Srimad Bhagavatam yanafunza kuwa Sambandha Mimi ni nani? Mungu ni nani? Uhusiano kati ya Mungu na mimi ni upi? na Abhideya mchakato wa kuanzisha uhusiano ulipotea na Mungu kupitia michakato 9 ya Bhakti - Huduma ya Maombi na Prayojana - matokeo - kupata upendo wa Mungu. Mchakato rahisi zaidi ni kuimba maha Bhakti "Hare Krsna Hare Krsna Hare - Hare Rama Hare Rama Hare Hare" pamoja na wafuasi wa Mungu. Huku maana ya maisha yakiwa kuanzisha upya uhusiano ulioisha na Mungu anayewapenda watu wote, lengo la uumbaji ni kutumia rasilimali kurudi nyumbani kwa Mungu, Dunia ya milele ya kinafsi inayoitwa Goloka Vrindavana - milki ya Mungu.

                                     

4.4. Mitazamo ya kidini Ujaini

Ujaini ni dini iliyoanza katika Uhindi ya kale, mfumo wake wa kimaadili unakuza nidhamu ya kibinafsi kushinda yote mengine. Kupitia kuyafuata mafundisho ya kujiepusha na anasa zote, ya ujaini, binadamu anapata kutaalamika maarifa kamili. Ujaini unaugawanya ulimwengu katika viumbe vilivyohai na visivyohai. Wakati tu visivyohai vinavyoshikilia vyenye uhai ndipo mateso hutokea. Kwa hivyo, furaha ni matokeo ya utekaji-kibinafsi na uhuru kutoka kwa vitu vya nje. Maana ya maisha basi huweza kusemwa kuwa kutumia mwili unaoonekana kupata utambuzi wa kibinafsi na neema.

Wajaini huamini kwamba kila binadamu anawajibika kwa matendo yake na viumbe wote hai wana roho ya milele, jīva. Wajaini wanaamini nafsi zote ni sawa kwa sababu zote zinamiliki uwezekano wa kufanywa ziwe huru na kufikia Moksha. Mtazamo wa Kijanini wa karma ni kwamba kila hatua, kila neno, kila wazo linazalisha, mbali na yanayoonekana, matokeo yasiyoonekana, na yanayopita fikira kwa nafsi.

Ujaini unajumuisha kushikilia vikali ahimsa au ahinsā, mbinu ya aina ya Kusitisha Vurugu ambayo huzidi kwa mbali ulaji mboga. Wajaini wanakikataa chakula kilichopatikana kwa ukatili usiohitajika. Wengi wana mazoezi ya maisha sawa na ulaji mboga pekee kutokana na vurugu ya mashamba ya maziwa ya kisasa, na wengine huepukana na mboga za mizizi katika maakuli yao ili kulinda maisha ya mimea ambayo wao hula.

                                     

4.5. Mitazamo ya kidini Ubudha wa Mapema

Ubudha ni mafundisho yasiyo na pande mbili, ambapo kichwa, chombo, na hatua yote ni huonekana yakiwa si ya kweli.

Wabudha wanaamini kwamba maisha kwa undani yamejaa mateso au kuchanganyikiwa. Hilo si kumaanisha kwamba hakuna raha maishani, lakini kwamba raha hii haisababishi furaha ya milele. Mateso yanasababishwa na kuvishikilia vitu vinavyonekana na kuguzika au visivyoonekana na visivyokuguzika ambavyo mwishowe husababisha mtu kuzaliwa tena na tena katika mzunguko wa kuwepo. Sutra na tantra za Kibudha haziongei kuhusu "maana ya maisha" au "madhumuni ya maisha", bali huzungumzia kuhusu uwezo wa maisha ya binadamu wa kukomesha mateso kupitia kujiepusha na tamaa na kushikilia dhana fulani. Mateso yanaweza kushindwa kupitia shughuli za binadamu, tu kwa kuondoa sababu ya mateso. Kufikia na kutimiza kutopenda raha ni mchakato wa ngazi nyingi ambazo hatimaye matokeo yake ni hali ya Nirvana. Nirvana inamaanisha uhuru kutoka mateso na kuzaliwa upya.

Ubudha wa Kitheravada kwa jumla unadhaniwa kuwa karibu na mazoezi ya mapema ya Wabudha. Unakuza dhana ya Vibhajjavada Pali, maana ya moja kwa moja "Kufunzwa kwa Uchambuzi", ambao Unasema kwamba lazima ufahamu utokane na uzoefu wa anAyenuia kuupata, uchunguzi makini, na kufikiria badala ya kutumia imani ya kipofu. Hata hivyo, mapokeo ya Kitheravadin pia yanasisitiza kuutilia maanani ushauri wa wenye busara, hasa ikizingatiwa kuwa ushauri huo na tathmini ya uzoefu wa kibinafsi kuwa vipimo viwili ambavyo vinafaa kutumiwa kuyapima mazoea. Lengo la Kitheravadin ni ukombozi au uhuru kutoka mateso, kulingana na Kweli Nne Adimu. Hili linapatikana katika kuipata Nirvana,au kufunguliwa ambao pia husitisha 0}mzunguko unaorudiwa wa kuzaliwa, uzee, maradhi na kifo.

                                     

4.6. Mitazamo ya kidini Ubudha wa Kimahayana

Shule za Ubudha wa Kimahayana zinasita kusisitiza mtazamo wa jadi ambao bado unatekelezwa katika Kitheravada wa kuachiliwa kutoka Mateso Dukkha ta kibinafsi na kufikia Mwamko Nirvana. Katika Mahayana, Budha huonekana kama kiumbe wa milele, asiyebadilika, asiyeeleweka, na ambaye yupo kila mahali. Misingi mikuu ya mafundisho ya Kimahayana imejikita katika uwezekano wa ukombozi kutoka mateso wa viumbe vyote, na kuwepo kwa Budha-asili apitaye fikira, ambaye ni kiini cha Budha wa milele aliopo, lakini aliyejificha na asiyetambulika, katika viumbe wote.

Shule za kifalsafa za Ubudha wa Kimahayana, kama vile Chan / Zen na shule za Utibeti wa vajrayana na Shingon, hufunza wazi kwamba boddhisattva lazima wajiepushe na ukombozi kamili, wajiruhusu wenyewe kuzaliwa tena ulimwenguni hadi viumbe wote wapate kutaalamika. Shule za kiibada kama vile Ubhuda wa Ardhi Takatifu hutafuta msaada wa mabudha wa mbinguni - watu binafsi ambao wametumia maisha yao wakikusanya karma chanya, na kuutumia mkusanyiko huo kuwasaidia wote.

                                     

4.7. Mitazamo ya kidini Kalasinga

Dini yenye Mungu mmoja ya Kalasinga ilianzishwa na Guru Nanak Dev. Neno "Kalasinga" linamaanisha mwanafunzi, kuashiria kwamba wafuasi wataishi maisha yao milele wakijifunza. Mfumo huu wa falsafa ya dini na kueleza imejulikana tangu jadi kama Gurmat maana yake shauri la maguru au Sikh Dharma. Wafuasi wa Kalasinga wametakaswa kuyafuata mafundisho ya maguru wa Sikh kumi, au viongozi wa kutaalamika, na pia maandiko matakatifu yaitwayo Gurū Granth Sāhib yanayojumuisha maandiko mbalimbali yaliyochaguliwa na wanafalsafa wengi kutoka mazingira mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kidini.

Maguru wa Kikalasinga hutuambia kwamba wokovu unaweza kupatikana kwa kuzifuata njia mbalimbali za kiroho, kwa hivyo si Wakalasinga pekee wanaopata wokovu: "Bwana anakaa ndani ya kila moyo, na kila moyo una njia yake yenyewe ya kumfikia." Wakalasinga huamini kwamba watu wote ni muhimu mbele ya Mungu. Wakalasinga hupima maadili yao ya kitabia na ya kiroho na kuyatafuta maarifa, na lengo la kukuza maisha ya amani na usawa, na pia yenye hatua chanya.

Sifa muhimu na tofauti ya Kalasinga ni dhana ya Mungu isiyo ya kumtazama Mungu akiwa na umbo fulani, kiasi kwamba mtu anaweza kumtafsiri Mungu kama Ulimwengu wenyewe upanthei. Kalasinga kwa hivyo inayaona maisha kama fursa ya kumuelewa huyu Mungu na pia kuugundua uungu ambao upo katika kila mmoja. Ingawa ufahamu kamili wa Mungu unazidi ubinadamu, Guru Nanak alielezea Mungu kama asiye eleweka kikamilifu, na kusisitiza kwamba Mungu lazima aonekana kutoka kwa "jicho la ndani", au "moyo", wa binadamu: wanaoamini lazima watafakari ili kuelekea kutaalamika. Nanak alihimiza ufunuo kupitia kutafakari, kwani kutumika kwake kila wakati kunaruhusu kuwepo kwa mawasiliano kati ya Mungu na binadamu.

                                     

4.8. Mitazamo ya kidini Ushinto

Ushinto ni dini iliyoanzia Ujapani. Neno Shinto linamaananisha "njia ya kami", lakini kwa ufasaha zaidi, linaweza kumaanisha "sehemu yenye njia nyingi ambapo kami anachagua njia yake". Njia yenye sehemu nyingi ya kimungu inaashiria kwamba ulimwengu wote ni roho ya kimungu. Msingi wa nia huru kuichagua njia ya mmoja, inamaanisha kwamba maisha ni mchakato wa ubunifu.

Ushinto Unayataka maisha ya kuishi, siyo ya kufa. Ushinto unakitazama kifo kama uchafuzi na inatazama maisha kama eneo ambapo roho ya kimungu inanuia kujitakasa yenyewe kwa kujiendeleza inavyostahili. Ushinto unayataka maisha ya kibinafsi ya kibinadamu kuendelezwa milele duniani kama ushindi wa roho ya kimungu katika kuhifadhi tabia yake ya usawa kwa hali ya juu kabisa. Kuwepo kwa uovu duniani, kama inavyodokezwa na Ushinto, hakupingi hali ya kimungu kwa kuweka juu ya uungu jukumu la kuweza kuyapunguza mateso ya binadamu huku ikikataa kufanya hivyo. Mateso ya maisha ni mateso ya roho ya kimungu katika kuyatafuta mafanikio katika ulimwengu unaolenga usawa.

                                     

4.9. Mitazamo ya kidini Utao

Kosmojenia ya Watao inasisitiza haja ya viumbe wote wenye fahamu na watu wote kurudi kwa mwanzo au kuungana na Umoja wa Ulimwengu kupitia njia ya kujikuza na kujitambua. Wahumini wote wanapaswa kuelewa na kuwiana na mwisho wa kikweli.

Wanaamini yote awali yalikuwa kutoka Taiji na Tao, na maana maishani kwa wahumini ni wao kugundua hali ya muda mfupi ya kuwepo. "Kujiangalia tu kindani ndio kunaoweza basi kutusaidia kupata sababu zetu za undani kabisa za kuishi.jibu rahisi limo humu ndani yetu."

                                     

4.10. Mitazamo ya kidini Ukonfusio

Ukonfusio unatambua hali ya binadamu kulingana na mahitaji ya nidhamu na elimu. Kwa sababu binadamu anaendeshewa na ushawishi mzuri na mbaya, Wakonfiuso huona lengo katika kupata tabia nzuri kupitia uhusiano wa nguvu na kufikiria na pia kukanusha nishati hasi. Msisitizo huu wa maisha ya kawaida unaonekana katika msemo wa mwanachuoni wa Kikonfiuso Tu Wei-Ming, "tunaweza kutambua maana kuu ya maisha katika kuwepo kwa kawaida kwa binadamu."

                                     

4.11. Mitazamo ya kidini Dini mpya

Kuna harakati nyingi mpya za kidini katika Asia ya Mashariki, baadhi yao zikiwa na mamilioni ya wafuasi: Chondogyo, Tenrikyo, Cao Dài, na Seicho-No-ie. Dini mpya kawaida zina maelezo ya kipekee kuhusu maana ya maisha. Kwa mfano, katika Tenrikyo, mtu anatarajiwa kuishi Maisha ya Furaha kwa kushiriki katika mazoea yanayokuza furaha yake binafsi na pia ya watu wengine.

                                     

4.12. Mitazamo ya kidini Uzoroastro

Uzoroastro ni dini na falsafa inayopata jina lake kutoka kwa nabii wake Zoroaster, ambayo labda iliathiri imani za Uyahudi na dini zilitokana na Uyahudi. Wazoroastro wanaamini ulimwengu na Mungu apitaye fikra, Ahura Mazda, ambaye ibada yote inaelekezwa kwake. Kiumbe cha Azhura Mazda ni asha, ukweli na mpango ambao unazozana na kinyume chake, druj, uwongo na machafuko.

Kwa sababu binadamu wana hiari, ni lazima wawe na uwajibikaji kwa maadili wanayoyachagua. Kwa kutumia hiari, watu lazima wawe na jukumu tendaji katika mgogoro wa dunia nzima, wawe na mawazo mema, maneno mema na matendo mema ili kuhakikisha furaha na kuepuka machafuko.

                                     

4.13. Mitazamo ya kidini Uyahudi

Kipengele muhimu zaidi cha Uyahudi ni ibada ya Mungu mmoja anayejua yote, mwenye nguvu kuliko wote, ambaye ni mkarimu kila wakati, anayepita fikra zote, na ambaye aliumba ulimwengu na anautawala. Kulingana na Uyahudi wa awali, Mungu alifanya agano na Waisraeli katika mlima Sinai, alipowapa sheria na amri zake zinazopatikana katika Torati. Katika Uyahudi wa Kirabi, Torati inajumuisha maandishi ya Torati na sheria ya mapokeo ya mdomo iliyoandikwa baadaye kama maandiko matakatifu.

Katika mtazamo wa ulimwengu wa Kiyahudi, maana ya maisha ni kumtumikia Mungu pekee wa kweli na kujiandaa kwa ulimwengu ujao. Fikira za "Olam Haba" Inahusu kujiinua kiroho, ni mtu kutumia "Olam Hazeh" dunia hii kwa kuunganika na Mungu na kujiandaa kwa "Olam Haba" ulimwengu ujao.

                                     

4.14. Mitazamo ya kidini Ukristo

Ingawa Ukristo una mizizi yake katika Uyahudi, na unafanana sana na ontolojia ya Uyahudi, imani kuu ya Ukristo inatokana na mafundisho ya Yesu Kristo yaliyotolewa katika Agano Jipya. Kusudi la maisha kwa Mkristo ni kutafuta wokovu wa Kimungu kupitia neema ya Mungu iliyoletwa na Yesu Yoh 11:26.

Agano Jipya linaongea kuhusu Mungu kutaka uhusiano na binadamu wote katika maisha haya na yale yajao, jambo ambalo linaweza kufanyika tu kama dhambi za mtu zimesamehewa Yoh 3:16-21, 2 Pet 3:9.

Katika mtazamo wa Kikristo, watu waliumbwa katika hali njema kwa mfano wa Mungu, lakini kuanguka kwao dhambi ya asili kulisababisha wanaozaliwa kuirithi dhambi hiyo.

Sadaka ya Yesu Kristo ya upendo, kifo na ufufuko hutoa njia ya kuishinda hali hiyo chafu Rum 6:23.

Njia ya kufanya hivyo inatofautiana kati ya madhehebu mbalimbali ya Wakristo, lakini yote yanategemea imani kwa Yesu, kazi yake msalabani na kufufuka kwake kama msingi wa uhusiano mpya na Mungu. Chini ya mtazamo wa Ukristo, watu wanafanywa waadilifu kupitia imani katika kafara ya Yesu kufa msalabani.

Injili inafundisha kwamba, kupitia imani hiyo, kizuizi ambacho dhambi imeunda kati ya mtu na Mungu kinaondolewa, ili kumruhusu Mungu kuwageuza watu na kuweka ndani yao moyo mpya unaotii mapenzi yake, na uwezo wa kutii hivyo.

Hii ndiyo maana inayoashiriwa na maneno kuzaliwa upya au kuokolewa.

Jambo hili linatofautisha sana Ukristo na dini nyingine ambazo zinadai kwamba waumini ni waadilifu kwake Mungu kwa kushikamana na mwongozo au sheria waliyopewa na Mungu.

Katika "Katekisimu Fupi ya Westminster", swali la kwanza ni: "Ni nini lengo kuu la binadamu?". Jibu ni: "Lengo kuu la binadamu ni kumtukuza Mungu na kufurahi naye milele. Mungu anataka mtu atii sheria ya maadili aliyomwonyesha akisema tumpende Bwana Mungu wetu kwa moyo wetu wote, kwa roho yetu yote, kwa nguvu zetu zote, na kwa akili zetu zote; na majirani wetu kama sisi wenyewe".

Katekisimu ya Baltimore inajibu swali, "Kwa nini Mungu amekuumba?" ikisema "Mungu ameniumba ili nimjue, nimpende na kumtumikia katika dunia hii, na kuwa na heri pamoja naye milele mbinguni."

Mtume Paulo alijibu swali hilo katika hotuba yake kwenye Areopago mjini Athene: "Kutokana na mtu mmoja Mungu alifanya kila taifa la wanadamu, ili waishi duniani kote; akapima nyakati hasa zilizowekwa kwao na mahali ambapo wanapaswa kuishi. Mungu alifanya hivyo ili binadamu amtafute kama kwa kupapasa ili kumpata, ingawa hayupo mbali na kila mmojawetu. Mdo 17:26-27

                                     

4.15. Mitazamo ya kidini Uislamu

Katika Uislamu, lengo kuu la maisha ya binadamu ni kumtumikia Allah kwa Kiarabu sawa na "Mungu" na kukaa na miongozo ya Kimungu iliyofafanuliwa katika Quran na Mapokeo ya Mtume. Maisha ya duniani ni mtihani tu ambao huamua maisha ya mtu baada ya kifo, katika Jannat Mbinguni au katika Jahannum Kuzimu.

Kwa ajili ya radhi ya Mwenyezi Mungu, kupitia Qurani, lazima Waislamu wote waamini katika Mungu, ufunuo wake, malaika wake, wajumbe wake, na katika "Siku ya Kiyama". Quran inaelezea madhumuni ya uumbaji kama ifuatavyo: "Heri yeye ambaye mkononi mwake ana ufalme, yeye ana nguvu juu ya kila kitu, ambaye aliumba mauti na uhai ili apate kuchunguza nani kati yenu ndiye bora katika matendo, na yeye ni mwenyezi, Mwenye kusamehe "Quran67:1-2 na" Mimi tu niliumba malaika na binadamu kuniabudu Mimi "Quran 51:56. Ibada inashuhudia kuwepo kwa umoja wa Mungu katika uongozi wake, majina yake, na sifa yake. maisha ya Duniani ni mtihani; jinsi mtu anavyotenda huamua kama nafsi ya mtu inakwenda Jannat Mbinguni au Jahannam Motoni.

Nguzo Tano za Kiislamu ni wajibu wa kila Muislamu; yaani: Shahadah ungamo la imani; Salah Maombi; Zakah ukarimu; Sawm kufunga wakati wa Ramadhan na Hajj Hija kwenda Makka. Zinatokana na maandiko ya Hadith, hasa ya Sahih Al-Bukhari na Sahih Muslim.

Imani ni tofauti kati ya Kalam. Dhana ya Kisunni ya mwisho wa safari iliyoamuliwa awali ni amri ya Kimungu; aidha, dhana ya Kishia ya nafsi kuwa na mahali pa kwenda kabla ya kifo ni haki ya Kimungu; katika mtazamo wa Kisufi unaoeleweka na wachache Ulimwengu upo tu kwa radhi ya Mungu; Uumbaji ni mchezo mkubwa, ambapo Mwenyezi Mungu ndiye tuzo kuu.

                                     

4.16. Mitazamo ya kidini Imani ya Baháí

Imani ya Bahai inasisitiza umoja wa ubinadamu. Kwa Wabaháí, madhumuni ya maisha ni kukua kiroho na kutoa huduma kwa ubinadamu. Binadamu wanatazamwa kama viumbe wa kiroho kwa undani. Maisha ya watu katika dunia hii tunayoishi hutoa fursa zilizopanuliwa za kukua, kukuza sifa na fadhila za Kimungu, na manabii walitumwa na Mungu kuwezesha hili.

                                     

5. Katika sanaa

Siri ya maisha na maana yake ni jambo linalorudiwa mara nyingi katika utamaduni maarufu, unaoonyeshwa katika burudani ya vyombo vya habari na aina mbalimbali za sanaa.

Katika mfululizo maarufu wa vitabu vya kuchekesha vya Douglas Adams kwa jina "The Hitchhikers Guide to the Galaxy", Jibu la Swali Kuu la Maisha, Ulimwengu, na Yote lina ufumbuzi wa kinambari wa 42, ambayo ilipatikana baada ya muda wa zaidi ya miaka milioni saba na nusu kupitia tarakilishi yenye nguvu kubwa kwa jina "Deep Thought". Baada ya kunganyika kwingi kutoka wazao wa waumbaji wake, "Deep Thought" anaelezea kuwa tatizo ni kuwa hawajui Swali Kuu, na ingewabidi kujenga kompyuta yenye nguvu zaidi ili kulibainisha. Kompyuta inaonyeshwa kuwa Dunia, ambayo, baada ya kuhesabu kwa miaka milioni, inaharibiwa ili kuunda Barabara ya Kiulimwengu dakika tano kabla ya kukamilisha kufanya hesabu. Katika Maisha, Ulimwengu na Kila kitu, inathibitishwa kwa kweli kuwa 42 ndilo Jibu Kuu, na kwamba haiwezekani kwa Jibu Kuu na Swali Kuu kujulikana katika ulimwengu mmoja, kwani zitafutana na kuuchukua ulimwengu, na kubadilishwa na kitu cha maajabu zaidi. Hatimaye, katika matumaini kwamba fahamu yake ina swali, Arthur Dent anajaribu kuliwaza swali, na anapata "unapata nini ukizidisha sita mara tisa?", Pengine ni dhana isiyosahihi, kwani kuwasili kwa "Golgafrinchans" katika Dunia ya kabla ya historia ingeharibu mchakato wa kuhesabu. Hata hivyo, Dent, Fenchurch, na Marvin anayekaribia kufa waliona ujumbe wa mwisho wa Mungu kwa uumbaji wake: "Sisi tunaomba msamaha kwa shida tuliyowaletea".

Katika maana ya maisha ya Monty Python,kuna kugusia kwingi kwa maana ya maisha. Katika "Sehemu ya VI B: Maana ya Maisha" mwanamke anayefanya kazi ya kusafisha anaelezea "Maisha ni mchezo, wakati mwingine unashinda au kushindwa" na baadaye mtu wa kupelekea watu vyakula hotelini anaelezea falsafa yake ya kibinafsi "Dunia ni pahali pazuri. Lazima uende ndani yake, na upende kila mtu, usiwachukie watu. Lazima hujaribu na kumfanya kila mtu awe na furaha, na upeleke amani na ridhaa kokote uendapo. Katika mwisho wa filamu, tunaweza kumuona Michael Palin akipewa bahasha, anaifungua, na kupea watazamaji maana ya maisha: "Basi, si kitu maalumu sana. Uh, jaribu kuwa mzuri kwa watu, epuka kula mafuta, soma kitabu kizuri kila wakati, pata kutembea, na jaribu kuishi pamoja kwa amani na utulivu na watu wa Imani zote na mataifa yote.

Katika kipindi kimoja cha "The Simpsons" kilichoitwa "Homer the Heretic", mfano wa Mungu unakubali kumwambia Homer maana ya maisha, lakini majina ya wahusika wa kipindi yanaanza kuonekana anapoanza kusema ni nini. Mapema katika kipindi hicho, Homer anaanzisha dini yake mwenyewe, ambapo anajaribu kumwabudu Mungu kwa njia yake mwenyewe, baadaye akimwwambia Moe kwamba dini hiyo haina kuzimu na haina kupiga magoti. Hata hivyo, Homer anaiacha kwa haraka dini yake ya anasa na ubinafsi baada ya nyumba yake kunusurika kuchomeka, akitafsiri moto kama ishara ya kulipiza kisasi kwa kimungu, na kuita "O Mwenye Nguvu za Kuumiza, nionyeshe nani wa kuumiza, naye ataumizwa." Ned anamfariji Homer kuwa moto haukuwa kisasi cha Mungu na Lovejoy anaelezea kwamba Mungu alikuwa "akifanya kazi katika mioyo ya marafiki na majirani wako walipokuja kukusaidia."

Mwishoni mwa "The Matrix Revolutions", Smith anahitimsha kwamba "madhumuni ya maisha ni kuisha" na anakusudia kuharakisha lengo hilo. The Matrix series. Mfululizo wa filamu wa "The Matrix" pia unatoa wazo la "wanaoishi katika ukweli uliobuniwa" na swali linalohusika na wazo hilo ikiwa kuwepo huko kunafaa kutazamwa kama kusiokuwa na maana, katika njia inayoweza kulinganishwa na Hadithi fupi yenye mafunzo ya pango ya Plato na jinsi baadhi ya mifumo ya imani hutazama ukweli, kama Ubuddha au Uaginostiki.

                                     

6.1. Viungo vya nje Jumla

 • Meaning of life” Archived Januari 4, 2010 at the Wayback Machine.
 • Why Life Extension - or Why Live at All?
 • Meaningsoflife.tv – Video discussions on the ultimate meaning of life with various religious and philosophical leaders.
 • Meaningsoflife.com
 • Frequently Asked Questions about the Meaning of Life Archived Septemba 27, 2007 at the Wayback Machine.
                                     

6.2. Viungo vya nje Kisayansi

 • The Big Question: Why are we here? – by Richard Dawkins
 • Meaning and Happiness – Research on meaning and happiness from the perspective of Positive psychology.
                                     

6.3. Viungo vya nje Kifalsafa

 • The Origin of Human Nature, A Zen Buddhist Looks a Evolution Archived Januari 13, 2009 at the Wayback Machine. by Albert Low
 • The Logic of Existential Meaning Archived Julai 9, 2007 at the Wayback Machine.
 • A Guide for the Godless: The Secular Path to Meaning Archived Julai 6, 2011 at the Wayback Machine.
 • An Objective Philosophy: Why We Exist? Archived Mei 14, 2008 at the Wayback Machine. – by Martin G. Walker.
 • Hedonism & Meaning of life Archived Juni 26, 2008 at the Wayback Machine.
 • "The Meaning of Life" in the Stanford Encyclopedia of Philosophy
 • Einsteins credo
                                     

6.4. Viungo vya nje Kiroho

 • A Guide for the Perplexed excerpt included – by E. F. Schumacher
 • Handbook for Mankind Archived Desemba 16, 2008 at the Wayback Machine. – by Buddhadasa Bhikkhu
 • Answers to Lifes questions – by The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints
 • The Meaning of Life from a Jewish perspective – by Rabbi Noah Weinberg
 • Human Life Archived Desemba 5, 2009 at the Wayback Machine. – by K. Sri Dhammananda
 • Human life on earth - A Spiritual Perspective Archived Septemba 13, 2017 at the Wayback Machine. – by New age