Back

ⓘ Jamii:Akiolojia
                                               

Antiokia

Antiokia ya Siria ni mji wa Uturuki, kwenye mto Oronte, karibu na Bahari ya Mediteranea na mipaka ya Syria. Ni makao makuu ya wilaya ya Hatay na wakazi wake ni 139.000 2001; ni muhimu sana kwa akiolojia.

                                               

Enzi ya barafu

Enzi ya barafu ni kipindi cha historia ya dunia ambapo halijoto kwenye uso wa dunia ilikuwa duni kwa muda mrefu, yaani miaka elfu kadhaa au zaidi. Kushuka kwa halijoto kwa muda mrefu kunasababisha kukua kwa barafuto kwenye ncha za dunia na milimani.

                                               

Mlima Karmeli

Mlima Karmeli (kwa Kiebrania הר הכרמל, Karem El/Har HaKarmel, "Shamba la mizabibu la Mungu"; kwa Kiarabu |الكرمل/جبل مار إلياس, Kurmul/Jabal Mar Elyas, "Mlima wa Mt. Eliya" unapatikana katika pwani ya Israeli kaskazini ukijitokeza katika Bahari ya Kati. Ni mlima muhimu kwa biolojia, akiolojia na dini mbalimbali na unahesabiwa na UNESCO "urithi wa dunia" upande wa viumbehai. Kadiri ya masalia yaliyopatikana huko, kwa kipindi fulani watu wa aina Homo neanderthalensis na Homo sapiens waliishi pamoja katika eneo hilo.

                                               

Kurene

Kurene ulikuwa mji wa Libya mashariki uliofuata ustaarabu wa Ugiriki wa kale halafu Roma ya kale. Uko karibu na Shahhat ya leo. Ulikuwa wa kale na muhimu kuliko miji mitano ya Kigiriki ya mkoa ambao kutokana na jina lake unaitwa hadi leo Cyrenaica. Mwaka 1982 ulitangazwa na UNESCO kuwa kituo cha Urithi wa Dunia.

                                               

Laetoli

Laetoli ni eneo karibu na Bonde la Oltupai, km 45 kusini kwake, ambapo mwaka 1972 Mary Leakey aligundua nyayo za kale za zamadamu watatu waliotembea kwa miguu miwili. Mwaka 2015 ushirikiano wa watafiti wa Tanzania na wa Italia uliwezesha kugundua nyayo nyingine mbili za msafara huohuo, za mmojawapo zikiwa ndefu sana kuliko nyingine.

                                               

Mbinu ya rediokaboni

Mbinu ya rediokaboni ni njia ya kisayansi ya kutambua umri wa mata ogania. Msingi wa mbinu hii ni uwepo wa kaboni katika kila kiumbe; na kupungua kwa idadi ya isotopi za kaboni aina za 14 C kwa sababu idadi za atomi nururifu inapungua kadiri ya mbunguo nyuklia. Kutokana na asilimia za kaboni nururifu ya 14 C iliyobaki katika mata ogania inawezekana kukadiria umri wake. Mbinu ya rediokaboni ni muhimu hasa kwa fani ya akiolojia. Mbinu hii inamruhusu mtaalamu kujua umri wa ubao, mifupa na mabaki mengine yanayotokana na viumbe wa kale. Hata hivyo mbinu hii inahitaji kuwepo kwa mata ogania, yaa ...

                                               

Michoro ya Kondoa

Michoro ya Kondoa ni kundi la michoro ya miambani katika wilaya ya Kondoa, mkoa wa Dodoma nchini Tanzania. Mapango au nusumapango haya zaidi ya 150 yanapatikana mfululizo kwenye vilima vinavyotazama mtelemko wa Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki. Mfululizo huo una urefu wa kilometa 9 na uko kama kilometa 20 kaskazini kwa Kondoa. Michoro hii inaonyesha picha za watu, wanyama na uwindaji. Hii inatazamwa kutoa ushuhuda wa namna ya maisha ya wachoraji waliokuwa wawindaji hasa. Hakuna mapatano kama michoro hii ilikuwa sehemu ya ibada za kuomba mafanikio katika uwindaji au labda ilikuwa namna y ...

                                               

Michoro ya miambani

Michoro ya miambani ni jina kwa michoro ya aina mbalimbali iliyofanywa na wanadamu kwenye uso wa miamba asilia. Ni aina ya sanaa inayoweza kuwa na umri mkubwa sana. Wataalamu wa akiolojia hutofautisha kati ya Petroglifi ing. petroglyph – zinazotokana na kukata nyufa kwenye uso wa mwamba Piktografi ing. pictograph – zinazotokana na kutumia rangi juu ya mwamba, hasa kwenye michoro ya mapango. Michoro ya aina hii hupatikana katika mabara yote na nchi nyingi. Mfano mashuhuri ni Michoro ya Kondoa nchini Tanzania. Inapatikana kwenye uso wa mwamba unaosimama kama ukuta ama kwenye mtelemko mkali w ...

                                               

Olduvai Gorge

Bonde la Oltupai ni eneo la kiakiolojia linalopatikana katika mkoa wa Arusha nchini Tanzania ambalo ni kati ya yale muhimu zaidi duniani. Hivyo ni kivutio cha watalii wengi wa nchi ya Tanzania kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi. Bonde hilo lipo katika hifadhi ya Ngorongoro na karibu na ile ya Serengeti, ni mahali ambapo zamadamu, viumbe wa kale waliokaribiana na mwili wa binadamu, waliishi tangu miaka milioni 2 hivi iliyopita. Kwa kuwa wataalamu kadhaa walidhani watu wa leo wametokana nao, eneo hilo pengine limeitwa kwa Kiingereza Cradle of Mankind, kitovu cha binadamu, ambao wameishi kati ...

                                               

Yeriko

Yeriko ni mji wa kale sana, ulioanzishwa miaka 9000 hivi KK karibu na mto Yordani. Mwaka 2006 ulikuwa na wakazi 20.400

Homo neanderthalensis
                                               

Homo neanderthalensis

Homo neanderthalensis alikuwa kiumbehai wa jamii ya binadamu. Pengine spishi hii inachukuliwa kama nususpishi. Utafiti wa DNA umeonyesha walifanana na binadamu wa leo kwa asilimia 99.7. Walienea katika Mashariki ya Kati, Ulaya Magharibi na kusini hadi Asia ya Kati. Kabla hawajatoweka miaka 40.000 iliyopita, waliweza kuzaliana na Homo sapiens baada ya huyo kutoka nje ya Afrika na hivi kurithisha sehemu ya jeni zao kwa binadamu wasio wa Kusini kwa Sahara.