Back

ⓘ Kipindupindu
Kipindupindu
                                     

ⓘ Kipindupindu

Kipindupindu ni ugonjwa hatari unaosababishwa na bakteria hasa katika utumbo mwembamba. Bakteria hizo ambazo huitwa vibriocholerae huweza kusababisha kuhara sana na kutapika sana pamoja na homa kali.

Maambukizi hutokea hasa kupitia maji au vyakula vilivyochafuliwa na wadudu kama vile nzi. Wadudu hao huweza kuchafua vyakula endapo vyakula hivyo vitaachwa wazi bila kufunikwa na chombo chochote na kuvutia nzi hao kutua juu ya vyakula hivyo na kuacha bakteria zitakazosababisha ugonjwa wa kipindupindu kwa mtu atakayekula chakula kile.

Kiwango cha kuhara na kutapika kinaleta upungufu wa maji na uwiano wa chumvi mwilini. Baada ya dalili hizo kutokea kuna hatari ya kifo kwa asilimia 20 - 70 ya wagonjwa kama hawana tiba.

Tunaweza kujilinda na kipindupindu endapo tukajilinda na vitu vifuatavyo ambavyo ni kunywa maji safi na salama na kula chakula kisichopoa. Bila kusahau kusafisha maeneo yote yanayomzunguka kiumbe hai, hasa binadamu. Yatupasa kufanya usafi katika mikoa yetu yote, hasa majijini ambako kunashutumiwa sana kuwa machafu.

                                     

1. Ambukizo

Kipindupindu husababishwa na bakteria aina ya Vibrio cholerae zinazosababisha kuhara majimaji yenye rangi kama maji ya kupikia mchele. Bakteria hiyo ilitambuliwa mwaka 1854 na Filippo Pacini.

Robert Koch alifaulu mwaka 1883 kufuga bakteria kutokana na utumbo wa watu waliokufa kwa kipindupindu huko Misri.

Kipindupindu hutokea hasa katika nchi pasipo maji safi, hasa ambako maji ya kunywa na majimaji ya choo yanaweza kuchanganyikana. Bakteria ya vibrio cholerae hupatikana hasa katika mavi na maji ya choo na pia katika maji ya bahari, maziwa na mito kama maji machafu huingizwa katika magimba ya maji bila kusafishwa kwanza.

Vilevile samaki na vyakula vingine kutoka maji yenye bakteria vinachafuliwa na vinaweza kusababisha ambukizo. Vilevile vyakula vinavyooshwa kwa maji yaliyochafuliwa na bakteria ya kipindupindu.

Katika mazingira yenye maji ya bomba, yaliyopitia karakana ya kusafisha maji machafu, kipindupindu hutokea mara chache tu. Kujulikana kwa njia za kuambukizwa kulikuwa sababu ya kuanzishwa na kugharamiwa kwa teknolojia hizo katika nchi nyingi.

                                     

2. Matibabu

1. Mgonjwa hunyweshwa maji mengi, kwa sababu mwili wake hupoteza maji mengi anapougua maradhi haya.

2. Dawa zinazojulikana kufanya kazi ni kama cotrimoxazole, erythromycin, doxycycline, chloramphenicol, na furazolidone. 3. Chanjo za kuzuia Kipindipindu hutolewa katika baadhi za nchi.

                                     

3. Kuepukana na Kipindupindu

Kinga ni kama ifuatavyo:

 • Tumia choo kila mara – usiende haja karibu au ndani ya chanzo cha maji.
 • wakati wowote kunawa mikono kabla ya kutayarisha au kula chakula, kusafisha vyombo kama sahani, vikombe n.k.
 • kunawa mikono kabisa kwa sabuni – kiganja, upande wa nyuma wa mkono, katikati ya vidole na kucha kwa sekunde. Baada ya haja na kabla ya kula.
 • mikono inayoshika wagonjwa au nguo zao inapaswa kunaniwa kwa sabuni
 • kuwa na akiba ya maji yaliyochemshwa pasipo na maji safi ya bomba
 • vifaa vyote vinavyotumiwa na wagonjwa vinapaswa kuchemshwa kwa maji ya moto
 • kupika chakula vizuri maana halijoto juu ya 75 °C hadi 85 mlimani inaua bakteria;
 • Tumia maji yaliyotibiwa pekee hasa ikiwa ya kunywa; yachemshe au utie matone 5 ya klorini kwa kila galoni 1 au utumie dawa ya kutakasa maji. Yaache maji yatulie kwa dakika 30 kabla ya kunywa.
 • maji ya choo yanayotokamana na wagonjwa wa kipindupindu yanapasa kupitia mashimo ya choo yaliyohifadhiwa vizuri ili kuzuia usambazaji wa bakteria
 • kumenya matunda yote
 • kufunika chakula maana nzi wanapitisha bakteria kwa miguu yao
 • mashimo ya choo yanapaswa kutiwa dawa za kuua bakteria kwa kutumia klorini


                                     

4. Historia

Mnamo miaka 1816-1826 kulikuwa na janga la kwanza la kipindupindu mkoani Bengal, nchini India. Waingereza 10.000 na Wahindi walikufa.

Janga la pili la kipindupindu lilikuwa mnamo 1829-1851 kilipoenea nchini Urusi, Hungaria, Ujerumani na Uingereza. Zaidi ya watu 55.000 walikufa katika Uingereza pekee. Mwaka 1831, watu 150.000 walikufa kutokana na janga hili nchini Misri.

Mwaka 1849, kipindupindu kilizuka tena kwa mara ya pili mjini Paris. Mjini London watu 14.137 walikufa.

Miaka ya 1961-1970: kulikuwa na janga lingine la kipindupindu nchini Indonesia. Ilianzia Afrika Kaskazini na kuenea hadi nchi ya Italia. Katika miaka ya 1970, watu waliathirika kidogo nchini Ujapani.

Mnamo 1991-1994 kulikuwa na janga lingine huko Amerika Kusini, lililosababishwa na meli iliyomwaga maji machafu. Nchini Peru watu takriban 10.000 waliuawa.

Mwaka 2000, wagonjwa 14.000 waliripotiwa kuugua kipindupindu. Takriban 87% waliripotiwa kutoka bara la Afrika.

Julai - Desemba 2007: ukame wa maji salama kwa ajili ya kunywa nchini Irak ulisababisha tena janga la kipindupindu. Watu 22 walifariki.

Mnamo Agosti 2007 jimboni Orissa, India, zaidi ya watu 2.000 walilazwa hospitalini.

Machi - Aprili 2008: watu 2.490 walilazwa hospitalini nchini Vietnam kutokana na janga la kipindupindu.

                                     

5. Waathirika maarufu

 • Pedro V, Mfalme wa Ureno
 • Mary Abigail Fillmore, mtoto wa rais wa Marekani Millard Fillmore
 • James K. Polk, rais wa kumi na moja wa Marekani
 • Alexandre Dumas mzee, mwandishi wa Kifaransa aliyeandika kitabu "The Three Musketeers"
 • Nicolas Léonard Sadi Carnot
 • George Bradshaw
 • Juan de Veramendi
 • John Blake Dillon
 • Charles X wa Ufaransa
                                     
 • Chanjo ya kipindupindu ni chanjo madhubuti katika kuzuia kipindupindu Zinatenda vizuri 85 muda wa miezi sita wa kwanza na 50 - 60 muda wa mwaka wa kwanza
 • aligundua kirusi kinachosababisha kifua kikuu, na mwaka wa 1883 kirusi kinachosababisha kipindupindu Mwaka wa 1905 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.
 • ya familia yake akahudumia waliopatwa na kipindupindu na makahaba. Hatimaye alihudumia tena wenye kipindupindu nayo ikampata na kumuua. Anaheshimiwa na
 • Ulaya. Anajulikana hasa kwa riwaya zake, kwa mfano Upendo wakati wa Kipindupindu kwa Kihispania El amor en los tiempos del cólera iliyotolewa mwaka
 • ya magonjwa na maradhi mabaya. Kinga ni bora kuliko tiba. Chanjo ya kipindupindu Chanjo ya ukambi How vaccines work British Society for Immunology en
 • ya mafukara aliowatembelea na kuwaombea. Hatimaye alijitoa mhanga ili kipindupindu mjini kikome ikawa hivyo. Alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenye heri
 • vimechafuliwa na kinyesi. Maji haya yanaweza kusababisha magonjwa kama kipindupindu na homa ya matumbo. Maji ni muhimu kwa maisha ya binadamu na viumbe hai
 • mazingira kwani tukiyachafua tutapata magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu na mengine mengi. Mazingira ni vitu vyote vinavyotuzunguka sisi wanadamu
 • nyongo nyeusi Nadharia ya miasma, iliyosema kwamba magonjwa kama vile kipindupindu au Tauni Nyeusi yalisababishwa na miasma, aina hatari ya hewa mbaya
 • Mauaji ya Rwanda. Watu wengi waliumwa na kufa kwa sababu ya kuharisha, kipindupindu na malaria. Ukosefu wa chakula, maji na mahitaji ya maisha ulisababisha