Back

ⓘ Supamaketi za Uchumi
Supamaketi za Uchumi
                                     

ⓘ Supamaketi za Uchumi

Supamaketi za Uchumi ni mtandao wa supamaketi nchini Kenya ulioanzishwa mwaka wa 1975 na uliorodheshwa katika Soko la Hisa la Nairobi mwaka wa 1992.

                                     

1. Kufungwa na kufunguliwa tena

Uchumi ilifungwa, kwa muda, katika mwezi wa Juni 2006 baada ya miaka 30 ya biashara. Wakati huo kufungwa kwake kulionekana kama msiba mkubwa zaidi uliokumba biashara katika historia ya Kenya. Baadaye serikali ilianzisha mpango wa kuiokoa na hapo basi vituo vitano vya Uchumi vikafunguliwa tena tarehe 15 Julai 2006, vyote vikiwa Nairobi.

                                     

2. Hali ya sasa

Mnamo Januari 2015 Uchumi ilikuwa ikiendesha maduka 37 nchini Kenya. Yaliyowahi kufunguliwa nje ya nchi yamefungwa yote.

Kampuni ina wenye hisa 12.000 hivi baada ya kurudishwa kwa kampuni kwenye soko la hisa la Nairobi.