Back

ⓘ Somo la Uchumi
Somo la Uchumi
                                     

ⓘ Somo la Uchumi

Somo la uchumi ni sayansi ya kijamii ambayo hutafiti uzalishaji, usambazaji, na matumizi ya bidhaa na huduma.

Neno uchumi linatokana na kitenzi "kuchuma". Jina la Kiingereza economy linatokana na neno la Kigiriki cha Kale oikonomia lenye maana ya "usimamizi wa kaya, utawala", kwa hiyo "sheria za nyumba kaya". Aina za masomo ya kiuchumi ya kisasa zilizotokana na somo pana la uchumi wa kisiasa katika miaka ya mwisho ya karne ya 19, kutokana na matamanio ya kuchukua mwelekeo jarabati unaofaa zaidi sayansi za kiasilia.

Ufafanuzi unaojumuisha mengi ya masomo ya kiuchumi ya kisasa ni ule wa Lionel Robbins katika insha yake:" Insha Juu ya Asili na Umuhimu wa Uchumi wa Kisayansi." Uhaba unamaanisha kuwa rasilimali zinazopatikana hazitoshi kutosheleza matamanio na mahitaji yote. Ikiwa hakuna uhaba na kuna matumizi badala ya rasilimali zinazopatikana, basi hakuna shida ya kiuchumi. Hivyo somo lililofafanuliwa linahusu utafiti wa chaguzi kama vile zinavyobadilishwa na vishawishi na rasilimali.

Somo la kiuchumi linalenga kufafanua vile uchumi hufanya kazi na vile viungo vya kiuchumi hufanya kazi pamoja. Uchambuzi wa kiuchumi huhusisha sehemu zote za jamii, katika biashara, fedha na serikali, na hata katika uhalifu, elimu,familia, afya, sheria, siasa, dini, taasisi za kijamii, vita, na sayansi. Hoja inayoendelea kukua ya somo la kiuchumi katika sayansi ya kijamii imeelezwa kuwa ubeberu wa kiuchumi.

Tofauti za kawaida huelezwa baina ya jinsi mbalimbali za somo la kiuchumi: baina ya uchumi chanya kueleza" kile kilichoko” na uchumi unaozidi kuongezeka kueleza" kile kinachostahili kuwa” au baina ya uchumi nadharia na uchumi wa utenzi au baina ya uchumi uliotanda ulio" halisi” unaojihusisha na" uwiano wa fikira-ubinafsi-msawazo” na uchumi usio asilia" badilishi” zaidi unaoshughulika na" uwiano wa taasisi-historia-muundo wa kijamii". Hata hivyo tofauti ya kimsingi ya kiada baina ya" uchumi wa kiwango cha chini” microeconomics, ambao unaotafiti tabia ya kiuchumi ya viungo pamoja na watu binafsi na makampuni na" uchumi wa kiwango cha juu” macroeconomics, ambao hushughulikia maswala ya ukosefu wa ajira, mfumuko wa bei, sera ya fedha na hazina kwa uchumi wote.

Fedha za umma ni sehemu ya uchumi ambayo hushughulika na ubuni wa bajeti ya mapato na matumizi ya kitengo cha sekta ya umma, kwa kawaida serikali. Mada hii hushughulikia maswala kama vile malipo ya ushuru ni nani hasa analipa ushuru fulani, uchambuzi wa gharama-faida wa mipango ya serikali, athari juu ya ufanisi wa kiuchumi na ugavi wa mapato katika aina tofauti za matumizi na ushuru, na siasa za kifedha. Jambo hili la mwisho, ambalo ni kipengele cha nadharia ya chaguo ya umma, hubuni tabia ya sekta ya umma kama mfano wa uchumi wa kiwango cha chini, unaohusisha maingiliano ya wapiga kura wanaojali maslahi yao wenyewe, wanasiasa, na wafanyakazi wa serikali au mashirika mengine.

Wingi wa uchumi ni wa manufaa, kwani hutafuta kueleza na kutabiri matukio ya kiuchumi. Uchumi wa kuamua thamani normative economics hujihusisha na kubaini lililo zuri au baya kiuchumi.

Uchumi wa ustawi ni tawi la uchumi wa kuamua thamani unaotumia ustadi wa uchumi wa kiwango cha chini ili kubainisha kwa wakati huo ufanisi wa ugavi katika uchumi na ugavi wa mapato unaohusishwa nao. Huwa unajaribu kupima ustawi wa jamii kwa kuchunguza shughuli za kiuchumi za watu wanaobuni jamii.

                                     

1. Uchumi wa kiwango cha juu

Uchumi wa kiwango cha juu huchunguza uchumi mzima ilikueleza mikusanyiko mipana na mwingiliano wao" kutoka juu hadi chini,” yaani, kwa kutumia aina iliyorahisishwa ya nadharia ya msawazo wa ujumla. Mikusanyiko kama hiyo ni pamoja na mapato na mazao ya kitaifa, kiwango cha ukosefu wa ajira, na mfumuko wa bei na mikusanyiko midogo kama jumla ya matumizi na matumizi ya uwekezaji na vipengele vyake. Somo hili hutafiti pia athari za sera ya hazina na sera ya kifedha.

Tangu angalau miaka ya 1960, uchumi wa kiwango cha juu umekuwa na ujumuishaji zaidi na hivyo kuwa na sekta za aina ya uchumi wa kiwango cha chini, ikiwemo uwiano wa akili wa washikadau, utumiaji wa ufanisi wa habari ya soko, na ushindani usio kamilifu. Jambo hili huzungumzia wasiwasi wa muda mrefu juu ya ukosefu wa uthabiti katika maendeleo ya mada hiyo hiyo.

Uchambuzi wa uchumi wa kiwango cha juu huzingatia vipengele vinavyoathiri kiwango cha muda mrefu na ukuaji wa mapato ya kitaifa. Vipengele kama hivyo ni pamoja na ukusanyaji wa mtaji, mabadiliko ya kiteknolojia na ukuaji idadi ya wafanyakazi.

                                     

1.1. Uchumi wa kiwango cha juu Ukuaji

Uchumi wa ukuaji hutafiti vipengele vinavyoeleza ukuaji wa kiuchumi – ongezeko la pembejeo kwa kila mkazo wa nchi katika muda mrefu. Vipengele hivyo hutumika kueleza tofauti katika kiwango cha mapato kwa mtu baina ya nchi, hasa kwa nini baadhi ya nchi hukua kwa kasi kuliko zingine, na ikiwa nchi hukutana katika viwango sawa vya ukuaji.

Vipengele vilivyochunguzwa zaidi ni pamoja na viwango cha uwekezaji, ukuaji wa idadi ya watu, na mabadiliko ya kiteknolojia. Vipengele hivi huwakilishwa katika namna ya nadharia au ujarabati kama ilivyo katika miundo ya urasimimpya na ukuaji wa kindani na katika ukuaji wa uhasibu.

                                     

1.2. Uchumi wa kiwango cha juu Mzunguko wa Biashara

Uchumi wa unyogofu ndio ulikuwa kichocheo cha ubuni wa" uchumi wa kiwango cha juu” kama kitengo tofauti cha somo la uchumi. Wakati wa Unyogofu Mkuu wa miaka ya 1930, John Maynard Keynes aliandika kitabu kiitwacho The General Theory of Employment, Interest and Money ambacho kiliorodhesha nadharia muhumu za uchumi wa Keneshia. Keynes alishikilia kuwa mahitaji ya jumla kwa bidhaa yanaweza kutotosha katika nyakati za kurudi nyuma katika ukuaji wa kiuchumi, huku matokeo yake yakiwa ni ukosefu wa ajira wa kiwango cha juu sana na ukosefu wa mapato yaliyokisiwa.

Kwa hiyo alitetea kuwekwa kwa sera tendaji na sekta ya umma, kukiwemo kuwekwa kwa sera ya hazina na benki kuu na kuwekwa kwa sera ya kifedha na serikali ili kuimarisha mapato katika muda wa mzunguko wa biashara. Kwa hivyo, hitimisho muhimu la uchumi wa Keneshia ni kuwa, katika hali fulani, hakuna ustadi wa moja kwa moja unaosogeza mapato na ajira kuelekea viwango vya uwepo wa ajira kwa wafanyakazi wote. Muundo wa John Hicks wa IS/LM umekuwa ndiyo tafsiri yenye ushawishi mkuu zaidi wa Nadharia ya Kiujumla.

Jinsi miaka imeendelea kupita, ndivyo kueleweka kwa mzunguko wa biashara kumegawika katika matawi mbalimbali ya mawazo, yanayohusika na au kutofautiana na Ukeneshia. Muhtasari wa urasimimpya huashiria mapatano ya uchumi wa Keneshia na ule wa urasimimpya, huku ukisema kuwa Ukeneshia unafaa katika muda mfupi, huku uchumi ukifuata nadharia ya urasimimpya katika muda mrefu.

Mfumo wa Mpya wa urasimi hukosoa maoni ya Keneshia juu ya mzunguko wa kibiashara. Unahitimisha kuwa dhana ya Friedman ya mapato ya kudumu juu ya matumizi," mageuzi ya matarajio yaendayo na mawazo" yaliyoongozwa na Robert Lucas, na nadharia ya mzunguko halisi wa biashara.

Kwa kinyume, mfumo Mpya wa Keneshia hushikilia matarajio ya kimawazo, ingawa hushikilia aina mbalimbali za kuanguka kwa masoko. Ukeneshia Mpya hasa hushikilia kuwa bei na marupurupu" havibadiliki”, kumaanisha kuwa havibadiliki moja kwa moja kulingana na hali ya kiuchumi.

Kwa hivyo, urasimi mpya hushikilia kuwa bei na marupurupu hufikia ajira kwa kila mtu moja kwa moja, huku Wakeneshia wapya huona ajira kwa watu wote ikifikiwa tu baada ya muda mrefu, na hivyo kuhitaji sera za serikali na benki kuu kwa sababu" muda mrefu” haupo mbali sana.                                     

1.3. Uchumi wa kiwango cha juu Mfumuko wa bei na sera ya kifedha

Pesa ni njia ya malipo ya mwisho ya bidhaa katika mingi ya mifumo ya bei na kitengo cha akaunti ambacho hutumika kwa kawaida kwa kuweka bei. Hujumuisha sarafu ambazo zinashukiliwa na umma usio benki na amana ambazo zinaweza kulipwa na pesa. Mfumo huu umeelezwa kuwa mkataba wa kijamii, kama lugha, inayofaa mmoja kwa sababu inawafaa wengine.

Kama chombo cha ubadilishanaji, pesa huwezesha biashara. Kazi yake ya kiuchumi inaweza kutofautishwa na ubadilishanaji wa bidhaa ubadilishanaji ambao hauhusishi pesa. Huku kukiwa na aina tofauti za bidhaa zilizozalishwa na wazalishaji maalum, ubadilishanaji wa bidhaa unaweza kuhitaji bahati mara dufu ambayo ni ngumu kupata kulingana na vitu vya kubadilisha, kwa mfano tufaha na kitabu. Pesa inaweza kupunguza gharama ya ubadilishanaji kwa sababu ya kukubalika kwake kwa urahisi. Hivyo, huwa ni nafuu zaidi kwa muuzaji kukubali pesa katika ubadilishanaji, kuliko mazao ambayo mnunuzi huzalisha.

Katika kiwango cha uchumi, nadharia na ushahidi vinalingana sawa na uhusiano wa manufaa unaotoka kwa jumla ya usambazaji wa pesa kelekea kwa bei ya siku hiyo na jumla ya mapato na kiwango cha bei ya kawaida. Kwa sababu hii, usimamizi wa usambazaji wa pesa ni kipengele muhimu cha sera ya kifedha.

                                     

1.4. Uchumi wa kiwango cha juu Sera ya hazina na uratibishaji

Uhasibu wa kitaifa ni mbinu ya kujumlisha mkusanyiko wa shughuli za kibiashara katika taifa. Akaunti za taifa ni mifumo ya uhasibu ya ncha mbili za kuweka hesabu ambayo hutoa hatua za kiundani zilizo na maelezo bayana kama hayo. Akaunti hizi ni pamoja na akaunti za kitaifa za mapato na bidhaa NIPA, ambazo hutoa makadirio ya thamani ya pesa ya mazao na mapato kwa mwaka au robo.

NIPA huruhusu kufuatilia kwa utendakazi wa uchumi na vipengele vyake kupitia kwa mizunguko ya kibiashara au katika vipindi virefu zaidi. Takwimu za bei zinaweza kuruhusu kutofautisha kwa bei ya siku kutoka kwa bei halisi, yaani, kurekebisha jumla ya pesa kwa mabadiliko ya bei kupitia vipindi vya nyakati. Akaunti za kitaifa hujumuisha pia kipimo cha mitaji ya hisa, utajiri wa taifa, na mtiririko wa mtaji wa kimataifa.

                                     

2. Uchumi wa kimataifa

Biashara ya kimataifa hutafiti vigezo vya mtiririko wa bidhaa-na-huduma kupitia mipaka ya kimataifa. Hushughulika pia ukubwa na usambazaji wa faida kutoka kwa biashara. Utendakazi wa sera hujumuisha kukisiwa kwa kubadilika kwa viwango vya ushuru na sehemu ya haki ya kibiashara. Fedha ya kimataifa ni kitengo cha uchumi wa kiwango cha juu kinachodadisi mtiririko wa mtaji kupitia mipaka ya kimataifa, na athari za mabadiliko katika viwango vya ubadilishaji. Kuongezeka biashara ya bidhaa, huduma na mtaji baina ya nchi ni athari kuu ya utandawazi wa leo.

Kitengo tofauti cha uchumi wa ustawi huchunguza vipengele vya uchumi vilivyo katika mchakato wa ustawi katika nchi zilizo na mapato ya chini huku kikizingatia kwa ubadilishaji wa mifumo, ufukara, na ukuaji wa uchumi. Mielekeo katika uchumi wa ustawi mara nyingi hujumuisha vipengele vya kijamii na vya kisiasa.

Mifumo ya kiuchumi ni tawi la uchumi linalotafiti mbinu na taasisi ambazo jamii hutumia kubaini umiliki, usimamizi, na ugavi wa rasilimali za kiuchumi. Mfumo wa kiuchumi wa jamii ni kitengo cha utafiti.

Katika mifumo ya kisasa katika nchi tofauti za upindi wa uratibishaji ni mifumo ya kisoshialisti na kikapitalisti, ambako wingi wa uzalishaji hutokea katika mashirika yanayosimamiwa na serikali na yale ya kibinafsi mtawalia. Baina ya makundi haya mawili kunao chumi zilizochanganyika. Jambo linalotokea katika makundi haya yote ni mwingiliano vishawishi vya kiuchumi na kisiasa, ambavyo huelezwa kwa upana kuwa uchumi wa kisiasa. Mifumo linganifu ya kiuchumi hutafiti utendakazi na tabia ya chumi au mifumo tofauti.                                     

3. Uchumi katika utekelezi

Uchumi wa sasa uliotanda, kama kitengo rasmi cha mifano cha hisabati, unaweza pia kuitwa uchumi wa kihisabati. Uchumi huu hutegemea vifaa vya masomo ya kihisabati ya calculus, linear algebra, takwimu, nadharia ya bahati, na sayansi ya kompyuta. Wanauchumi wa kitaalamu hutarajiwa kujua vifaa hivi, ingawa wanauchumi wote huwa na utaalamu, na baadhi yao huwa wataalamu wa uchumikihisabati na mbinu za kihisabati huku wengine wakiwa wataalamu katika vitengo vingine ambavyo havina hesabu nyingi.

Wanauchumi wa mfumo wa heterodox hutilia hisabati msisitizo mchache, na baadhi ya wanauchumi wa kihistoria, wakiwemo Adam Smith na Joseph Schumpeter, hawajakuwa wanahisabati. Mawazo ya kiuchumi huhusisha ujuzi wa akili kuhusu dhana za kiuchumi, na wanauchumi hujaribu kuchambua hadi pale wanagundua matokeo ambayo hayakutarajiwa.

                                     

3.1. Uchumi katika utekelezi Nadharia

Nadharia ya uchumi iliyotanda hutegemea mifumo ya kiuchumi ya kihisabati ambayo haitegemei uzoevu, ambayo hutumia dhana kadha wa kadha. Nadharia huendelea mbele na wazo la vipengele vingine vikibaki vilivyo, ambalo humaanisha kumudu vipengele vingine jinsi vilivyo ila kile kimoja kinachozingatiwa. Katika kubuni nadharia, lengo ni kupata zile ambazo kwa uchache ni rahisi kwa matakwa ya habari, sahihi zaidi katika utabiri wake, na za faida kubwa katika uzalishaji wa utafiti zaidi kuliko nadharia zilizokuwepo awali.

Katika uchumi wa kiwango cha chini, dhana kuu ni pamoja na ugavi na mahitaji, upembezoni, nadharia ya chaguo la kutokana na mawazo, gharama ya fursa, vikwazo vya kibajeti, utumiaji na nadharia ya kampuni. Mifumo ya mapema ya uchumi wa kiwango cha juu ilizinhatia kubuni uhusiano baina ya vipengele jumuishi, lakini kwa vile uhusiano ulionekana kubadilika katika wakati wanauchumi walishurutishwa kutumia wakfu za kiwango cha chini kama msingi wa mifumo yao.

Dhana za uchumi wa kiwango cha chini ambazo zimekwishatajwa huwa na nafasi muhimu katika mifumo ya uchumi wa kiwango cha juu – kwa mfano, katika nadharia ya kifedha, nadharia ya viwango ya pesa hutabiri kuwa kuongezeka katika usambazaji wa pesa huongeza mfumuko wa bei, na mfumuko wa bei hufikiriwa kushawishika na matarajio ya kifikira. Katika uchumi wa ustawi, ukuaji wa polepole katika mataifa yanayostawi unetabiriwa mara nyingine kwa sababu ya kupungua kwa mapato ya pembezoni kutoka kwa uwekezaji na mtaji, na hali hii imeonekana katika mataifa manne ya Kiasia yajulikanayo kama Four Asian Tigers. Mara nyingine dhana ya kiuchumi huwa tu ni ya kueleza jinsi ya kitu na wala si ya kihisabati.

Maonyesho ya kubainisha fikira za kiuchumi mara nyingi hutumia michoro ya pande mbili ili kuonyesha husiano za kinadharia. Katika kiwango cha juu cha ujumuishaji, maandishi ya Paul Samuelson Foundations of Economic Analysis 1947 yalitumia mbinu za kihisabati kueleza nadharia, hasa jinsi ya kuweka kwa kiwango cha juu zaidi uhusiano wa kitabia wa vipengele tekelezi ili kufikia msawazo. Kitabu hicho kilizingatia kuchunguza kundi la taarifa lijulikanalo kama semi za kinadharia zenye maana katika utekelezi katika uchumi, ambazo ni semi za kinadharia ambazo zinaweza kupingwa na takwimu za ujarabati.

                                     

3.2. Uchumi katika utekelezi Utafiti wa ujarabati

Nadharia za kiuchumi mara nyingi huchunguzwa kijarabati, sanasana kwa kutumia uchumukihisabati kutumia takwimu za kiuchumi. Majaribio ya kuthibitiwa yanayopatikana sanasana katika sayansi za kiasili ni magumu na hayapatikana sana katika somo la kiuchumi,na badala yake takwimu za upana hutafitiwa kwa kufanyiwa uchunguzi; aina hii ya uchunguzi huonekana na wengi kuwa rahisi kuliko ile ya majaribio ya kuthibitiwa, na mahitimisho huwa kwa kawaida yasiyo na uhakika kamili. Idadi ya sheria zilizovumbuliwa na somo la kiuchumi ni ya chini ikilinganishwa na ile ya sayansi asilia.

Mbinu za kutumia takwimu kama vile uchambuzi wa kurudi nyuma ni za kawaida. Watekelezaji hutumia mbinu kama hizo kukisia ukubwa, umuhimu wa kiuchumi, na umuhimu wa takwimu" nguvu za ishara” za mahusiano yaliyokisiwa na kuratibisha kelele kutoka kwa vipengele vingine. Kwa njia hiyo, dhana inaweza kukubaliwa, ingawa kwa jinsi ya makisio na wala si uhakika. Kukubalika hutegemea dhana zinazoweza kuwekewa uongo ambazo zilimudu majaribio. Utumiaji wa mbinu zinazokubalika kwa kawaida hauna haja ya kutoa hitimisho la mwisho. Au hata makubaliano juu ya swala fulani, ikiwa lilikuwa na majaribio tofauti, takwimu tofauti, na imani za awali.

Ukosoaji unaolenga viwango vya kitaalamu na ukosefu wa kufanana katika matokeo huwa ni masharti zaidi dhidi ya uonevu, upotovu, na ujumuisha wa kiwango cha juu mno, ingawa wingi wa utafiti wa kiuchumi umekosolewa kwa ukosefu wa kufanana katika matokeo, na nakala za kifahari zimekosolewa kwa kutowezesha urudiaji wa matokeo yaliyofanana kwa kutoa nambari za kificho na takwimu. Kama ilivyo katika nadharia, matumizi ya takwimu za majaribio huwa yamefunguka yenyewe kwa uchambuzi wa kukosolewa, ingawa ufafanuzi muhimu wa nakala juu ya uchumi katika jedwali za kifahari kama vile American Economic Review umepungua kwa kiwango kikubwa katika miaka 40 iliyopita. Jambo hili limehusishwa na motisha ya majedwali ya kutaka kuongeza nukuu ili kuorodheshwa katika nafasi nzuri kwenye Fahirisi ya Nukuu za Sayansi ya Kijamii - Social Science Citation Index SSCI.

Katika uchumi tekelezi, mifumo ya pembejeo na mapato itumiayo mbinu za utaratibishaji wa kunyooka linear programming ni ya kawaida mno. Viwango vikubwa vya takwimu hupitishwa katika mipangilio ya kompyuta ili kuchambua matokeo ya sera fulani; IMPLAN ni mfano mmoja maarufu.

Uchumi wa majaribio umeimarisha utumiaji wa majaribio ya kuthibitiwa ya kisayansi. Hali hii imepunguza tofauti ya kutoka jadi baina ya uchumi na sayansi asili wa kukubalia majaribio ya vipengele vilivyofikiriwa hapo awali kuwa dhana. Katika visa kadhaa majaribio haya yamegundua kuwa dhana huwa si sahihi hasa; kwa mfano mchezo wa hatima ulionyesha kuwa watu hukataa matoleo ambayo hayatoshani.

Katika uchumi wa kitabia, wanasaikolojia Daniel Kahneman na Amos Tversky wameshinda Matuzo ya Nobel ya kiuchumi kwa kazi ya uvumbuzi wa kijarabati wa uonevu wa kimawazo na jibu lililo karibu zaidi na jibu halisi heuristics. Majaribio ya ujarabati yanayofanana na hayo hufanywa katika somo la uchumi wa kiubongo neuroeconomics. Mfano mwingine ni wazo la chaguzi za kibinafsi dhidi ya mfumo ambao huchunguza chaguzi binafsi, za kutaka ustawi wa wengine na za ushirikiano. Ustadi huu umesababisha wengine kusema kuwa uchumi ni" sayansi halisi.".

                                     

3.3. Uchumi katika utekelezi Nadharia ya bahati

Nadharia ya bahati ni tawi la hisabati tekelezi ambalo hutafiti mwingiliano wa mbinu baina ya vipengele tekelezi. Katika mbinu za bahati, vipengele tekelezi huchagua mbinu ambazo zitaongeza mapato yao, ukilinganisha na mbini ambazo vipengele vingine huchagua. Nadhari hii hutoa mfumo rasmi wa mwelekeo kwa hali za kijamii ambapo wafanya maamuzi huingiliana na watendaji wengine.

Nadharia ya bahati hujumuishwa mielekeo ya kuongeza yaliyobuniwa ili kutafiti soko kama vile mfumo wa ugavi na mahitaji. Somo hili lilitokana na kitabu cha urasimi cha 1944 kiitwacho Theory of Games and Economic Behavior kilichoandikwa na John von Neumann na Oskar Morgenstern. Somo hili limepata utekelezi wa kiwango kikubwa kiasi katika sehemu nyingi nje ya uchumi vile inavyofikiriwa, ambayo ni pamoja na ubuni wa ustadi wa kinyuklia, maadili, sayanzi ya kisiasa na nadharia ya mageuzi.

                                     

3.4. Uchumi katika utekelezi Taaluma

Kufanywa taaluma kwa uchumi, jinsi inavyoonekana katika ongezeko la masomo ya daraja ya pili ya vyuo vikuu katika somo hilo, kumeelezwa kuwa" badiliko kuu katika somo la uchumi tangu miaka ya 1900". Idadi kubwa ya vyuo vikuu vya kutajika na taasisi nyingi huwa na somo kuu, kitivo, au idara kuu ambapo shahada za kielimu hutolewa katika somo hili, iwe ni kwa masomo ya sanaa huria, biashara, au kwa masomo ya taaluma.

Tuzo la Bank of Sweden Prize in Economic Sciences in Memory of Alfred Nobel kwa usemi, Tuzo la Nobel katika Uchumi ni tuzo ambalo hutolewa kwa mwanauchumi kila mwaka kwa mchango mkuu wa kimawazo katika somo hili. Katika sekta ya kibinafsi, wanauchumi wataalamu huajiriwa kama washauri na katika sekta, inayojumuisha uhifadhi katika benki na maswala ya kifedha. Wanauchumi pia hufanya kazi katika idara na mashirika ya serikali, kama vile Hazina ya kitaifa, Benki Kuu au Afisi ya Takwimu.

                                     

4. Somo la uchumi na masomo mengine

Uchumi ni mojawapo ya sayansi za kijamii baina ya zingine kadhaa na huwa na matawi yanayopakana na masomo mengine, yakiwemo jiografia ya kiuchumi, historia ya kiuchumi, uchaguzi wa umma, uchumi na nisharti, uchumi wa utamaduni, na uchumi wa taasisi.

Sheria na uchumi au utafiti wa kiuchumi wa sheria, ni mwelekeo wa nadharia ya kisheria ambao hutumia mbinu za kiuchumia katika sheria. Somo hili hujumuisha utumizi wa dhana za kiuchumi ili kueleza athari za kanuni za kisheria, kubainisha ni kanuni zipi za kisheria zilizo na ufanisi wa kiuchumi, na kutabiri ni kanuni za kisheria zinazweza kuwa. Makala ya mafundisho yaliyoandikwa na Ronald Coase na kuchapishwa mnamo 1961 yalipendekeza kuwa sheria za umiliki wa mali zilizodhihirishwa vyema hushinda matatizo yanayotokana na vipengele vua nje.

Uchumi wa kiasiasa ni utafiti unaojumuisha masomo mengi kwa kuchanganya uchumi, sheria, na sayansi ya kisiasa ili kueleza jinsi taasisi za kisiasa, mazingira ya kisiasa, ma mfumo wa kiuchumi hushawishiana. Unatafiti maswali kama vile jinsi makundi yanayotawala shughuli za soko, tabia ya kutafuta manufaa ya kibinafsi kwa madhara ya wengine, na vipengele vya nje vinafaa kuathiri sera ya serikali. Wanahistoria wametumia uchumi wa kisiasa kutafiti njia za wakati uliopita ambazo watu na makundi yaliyo na maslahi yanayofanana ya kiuchumi wametumia siasa ili kuleta mabadiliko ambayo yanafaidi maslahi yao.Georgescu-Roegen alianzisha upya dhana ya entropy aliyoihusisha na uchumi na nishati kutoka kwa somo la ubadilishaji wa nishati la thermodynamics, huku akiitofautisha na kile alichoona kuwa msingi wa kiufundi wa uchumi wa urasimimpya unaotokana na fizkia ya Newton. Kazi yake ilichangia kwa kiwango kikubwa kwa somo la uchumi wa kubadilisha nishati kuwa kazi na joto na kwa uchumi wa kiikolojia. Vilevile alifanya kazi ya kimsingi ambayo iliendelea na kuwa uchumi wa mageuzi.                                     

5. Ukosoaji wa somo la kiuchumi

"Sayansi duni” ni jina badala lililo la kudharau litumikalo kwa uchumi na lililobuniwa na mwanahistoria wa enzi ya Victoria Thomas Carlyle katika karne ya 19. Mara nyingi, husemekana kuwa Carlyle aliupatia uchumi jina la utani la" sayansi duni” kama jibu kwa maandishi karne ya 18 ya Reverend Thomas Robert Malthus, ambaye alitabiri kwa hofu kuwa njaa ingetokea, vile matarajio ya ukuaji wa idadi ya watu yangezidi ongezeko la usambazaji wa chakula. Mafundisho ya Malthus hatimaye yalijulikana chini ya mwavuli wa maneno" Dhana Duni ya Malthus". Utabiri wake ulisitishwa na uboreshaji mkubwa ambao haukuwa umetarajiwa katika ufanisi wa uzalishaji wa vyakula katika karne ya 20; ilhali mwisho wa hatari ambao aliutabiri unabaki kuwa uwezekano ambao haukubaliki na wengine, ikiwa uzuli wa binadamu utashindwa kumudu ongezeko la idadi ya watu.

Baadhi ya wanauchumi kama vile John Stuart Mill au Leon Walras, wamedumisha fikira kuwa uzalishaji wa mali haufai kuunganishwa na usambazaji wake. Uzalishaji ni kitengo cha" uchumi tekelezi” huku usambazaji ukiwa ni aina ya" uchumi wa kijamii” na sana huwa ni swala la mamlaka na siasa.

Katika The Wealth of Nations, Adam Smith anazungumzia masuala mengi ambayo kwa sasa ni mada ya mjadala na mabishano. Smith alishambuliwa mara kadhaa makundi ya watu waliojihusisha na siasa ambao hujaribu kutukia ushawishi wao kuishurutisha serikali kufanya vile watakavyo. Katika enzi ya Smith, haya yaliitwa makundi ya wafitini, lakini kwa sasa hujulikana sana kama maslahi maalum, jina ambalo linaweza kujumuisha wafanyakazi wa mabenki, mashirika ya makampuni, makundi yanayotawala kwa wazi shughuli za soko, kikundi kimoja kinachotawala shughuli za soko, vyama vya wafanyakazi na makundi mengine.

Uchumi halisi, kama sayansi ya kijamii, huwa huru kutoka kwa vitendo vya kisiasa vya serikali yoyote au mashirika mengine yanayofanya uamuzi, hata hivyo, wabuni wengi wa sera au watu binafsi walio na vyeo vikubwa sana ambavyo vinaweza kuwa na ushawishi katika maisha ya watu wengine wana sifa ya kutumia bila mpangilio wowote dhana nyingi sana za kiuchumi na maneno matupu kama chombo cha kuhalalisha ajenda na mifumo ya maadili, na huwa hawakomeshi usemi wao kwa maswala yanayohusu majukumu waliyo nayo. wa karibu wa nadharia na utekelezi wa kiuchumi na siasa Madai haya ya nyuma ni ya utata.

Utafiti wa shirika la International Monetary Fund wa mwaka wa 2002 ulizingatia" utabiri wa makubaliano” utabiri wa makundi makubwa ya wanauchumi ambao ulifanywa awali kabla ya kurudi nyuma kwa uchumi kwa mataifa 60 tofauti katika miaka ya 90; katika 97% ya visa wanauchumia hawakutabiri mpunguo kwa mwaka mmoja kabla ya tukio. Katika visa vile vya nadra ambako wanauchumi walitabiri kwa mafanikio kurudi nyuma kwa uchumi, walikadiria makali yake kwa kiwango cha chini mno.

                                     

5.1. Ukosoaji wa somo la kiuchumi Ukosoaji wa dhana

Uchumi umekuwa mada ya ukosoaji hadi hutegemea dhana ambazo hazina uhakika, haziwezi kuthibitishwa na zimerahisishwa visivyofaaa, kwa wakati mwingine kwa sababu dhana hizi hutumia hisabati zinazovutia. Mifano ni pamoja na habari kamilifu, uimarishaji wa faida kwa kiwango cha juu zaidi na chaguzi za kimawazo. Baadhi ya nadharia za kisasa za kiuchumi zimezingatia kuzungumzia matatizo haya kupitia kwa matawi madogo ya somo hili yanayoibuka kama vile uchumi wa taarifa, uchumi wa tabia, na uchumi wa utata, huku Geoffrey Hodgson akitabiri mabadiliko makubwa katika mwelekeo uliotanda wa kiuchumi. Hata hivyo, wanauchumi maarufu wa uchumi uliotanda kama vile Keynesna Joskow, pamoja na wanauchumi wa kiheteredoksi, wametoa maoni kuwa kiwango kikubwa cha uchumi huwa ni cha kidhana na wala si cha kihisabati, na huwa ni vigumu kuweka mifumo na kuurasmisha kwa kutumia mbinu za kihisabati. Katika majadiliano juu ya utafiti wa makundi ya kutawal shughuli za soko, Paul Joskow alionyesha mnamo 1975 kuwa katika utekelezi, wanafunzi wenye bidii wa uchumi halisi, huwa na mazoea ya kutumia" mifumo isiyo rasmi” inayotokana na vipengele vya maelezo ambavyo hutumiwa katika sekta maalum. Joskow aliamini sana kuwa kazi muhimu ya kutafiti makundi yanayotawala shughuli za soko ilifanya kupitia uchunguzi usio rasmi huku mifumo rasmi ilikuwa" ikionyeshwa kwa madaha baada yakazi kumalizika ". Alidai kuwa mifumo rasmi kwa kiasi kikubwa haikuwa na maana katika kazi ya ujarabati, vilevile, na kuwa kipengele muhimu kilicho msingi wa nadharia ya kampuni, tabia, kilipuuzwa.

Licha ya wasiwasi huu, masomo ya daraja ya pili ya vyuo vikuu yameendelea kuwa ya kiufundi na kihisabati. Ingawa nyingi ya kazi ya kimsingi ya utafiti wa kiuchumi katika historia ulihusu dhana na wala si hisabati, kwa sasa huwa ni vigumu zaidi kupata uwezekano wa kuchapisha nakala isiyo ya kihisabati katika jedwali mashuhuri. Kuona ukweli kwa upande wa baadhi ya wanafunzi kuhusu kuzingatia kwa uchumi kwa vitu ambavyo haviwezi kushikika na vya ufundi kumesababisha kuzuka kwa kundi la uchumi wa baada ya hali ya autism, ambao ulianza Ufaransa mnamo 2000.

David Colander, mtetezi wa uchumi tata, amezungumzia vilevile kwa kukosoa mbinu za kihisabati za kiuchumi, ambazo anahusisha na mfumo wa chuo cha MIT kwa uchumi, kinyume cha ule wa Chicago ingawa anasema pia kuwa mfumo wa Chicago hauwezi tena kuitwa ulio na maono ya kiakili. Anaamini kuwa mapendekezo ya sera kutokana na mfumo wa maono ya kiakili ya Chicago yalichangia kushuka kwa uchumi wa maono ya kiakili. Anasema pia kuwa amewahi kukutana na wanauchumi wenza ambao wamekataa katakata kujadiliana kuhusu uchumi wa kusisimua pasipo na mfumo rasmi, na anaamini kuwa mifumo mara nyingine huzuia maono ya mawazo. Hivi karibuni zaidi, hata hivyo, ameandikwa kuwa uchumi wa kiheterodoksi, ambao mara nyingi huchukua zaidi mwelekeo wa maono ya kimawazo, unafaa kushirikiana na wanahisabati na kuwa wa kihisabati zaidi. "Uchumi uliotanda ni mfumo wa kirasmi”, anaandika, na kinachohitajika si kupungua kwa hisabati wala ni kuongezeka kwa viwango vya hisabati. Anaeleza kuwa baadhi ya mada zinazozingatiwa na wanauchumi wa kiheterodoksi, kama vile umuhimu wa taasisi au ukosefu wa uhakika, zinatafitiwa kwa sasa kupitia mifumo ya kihisabati bila kutaja kazi iliyofanya na wanauchumi wa kiheterodoksi. Uchumi mpya wa taasisi, kwa mfano, huchunguza taasisi kihisababti bila kuhusisha sana somo linatokana kwa kiasi kikubwa na kiheterodoksi la uchumi wa taasisi.

Katika hotuba yake ya Tuzo la Nobel ya 1974, Friedrich Hayek, anayejulikana kwa uhusiano wake wa karibu na mfumo wa kiheterodoksi wa uchumi wa Kiaustria, alilaumu kutofaulu kwa sera za ushauri wa kiuchumi kwa maelekeo ya kuiga utaratibu wa kihisabati unaotumika kwa sayansi asilia bila kupambanua au kutumia mbinu za kisayansi. Anatoa hoja kuwa hata matukio ya kiuchumi ambayo yametafitiwa kwa kiwango kikubwa, kama vile ukosefu wa ajir akatika soko, huwa kwa kindani na utata mkubwa kuliko matukio kama hayo katika somo la sayansi asilia ambako mbinu zilibuniwa hapo awali. Vilevile, nadharia na takwimu huwa mara nyingi havidhihiriki na hushughulikwa kulingana na mwelekeo wa mabadiliko yanayohitajika, na wala si ukubwa wake. Kwa upande mmoja kwa sababu ya ukosoaji, uchumi umepatwa na uratibishaji wa hali ya juu na ufafanuzi wa dhana na mbinu tangu miaka ya 1940, ambao baadhi yake imeelekea katika utekelezaji wa mbinu ya kidhana na kimawazo hypothetico-deductive method katika kueleza matokeo ya dunia halisi.

                                     

6. Marejeo

 • Barr, Nicholas 2004 Uchumi wa Welfare State, 4th ed., Oxford University Press
 • Stiglitz, Joseph 2000 Uchumi wa Sekta ya Umma, 3rd ed., Norton Press
                                     

7. Viungo vya nje

Habari za ujumla
 • Uchumi katika Open Directory Project Archived Julai 10, 2013 at the Wayback Machine.
 • Intute: Economics: Orodha ya anwani ya tovuti ya vyuo vikuu vya Uingereza.
 • Uchumi katika Encyclopædia Britannica.
 • Vifaa Kwa Wanauchumi: Mwongozo unaodhaminiwa na Chama cha Kiuchumi cha Marekani ulio na vifaa zaidi ya 2000 vya Tovuti kutoka "Data" to "Neat Stuff,".
 • Nakala za Utafiti katika Somo la Uchumi RePEc
 • Economics katika Open Directory Project
Taasisi na mashirika
 • Economics Departments, Institutes and Research Centers in the World
 • World Trade Organization
 • World Bank Data
 • Organization For Co-operation and Economic Development OECD Statistics
 • United Nations Statistics Division
 • Center for Economic and Policy Research Marekani
Zana za masomo
 • Maktaba ya Uchumi na Uhuru EconLib: Vitabu vya Somo la Uchumi, Makala, Blogi EconLog, Podcasts EconTalk
 • Mifumo ya mawazo: Linganisha mifumo ya kiuchumi mbalimbali juu ya maswala fulani
 • MIT OpenCourseWare: Economics: Makavazi ya zana za masomo kutoka kwa kozi za MIT
 • Sehemu ya Ask The Professor ya EH.Net Economic History Services
 • Zana za masomo za MERLOT: Economics: Hakiki iliyo Marekani ya vifaa vya masomo
 • Mwongozo wa vitabu vya kiada kadha wa kadha katika tovuti Archived Agosti 12, 2013 at the Wayback Machine.
 • Vitabu vya kiada vya kiuchumi katika Wikibooks
 • Zana za kusoma na kufundisha zilizo katika tovuti, hakiki za UK Economics Network, picha, maelezo ya maneno na vifaa vingine
 • Uchumi katika About.com
 • Introduction to Economics: Dibaji fupi ya uchumi wa kimsingi iliyopewa leseni na Creative commons