Back

ⓘ Uwanja wa Nyayo
Uwanja wa Nyayo
                                     

ⓘ Uwanja wa Nyayo

Uwanja wa kitaifa wa Nyayo ni uwanja wa azma tofauti mjini Nairobi, Kenya. Iko karibu na kituo cha mji. Uwanja huu unaweza kushikilia watu elfu thelathini na ulijengwa mwaka wa 1983. Hivi sasa hutumiwa zaidi kwa mechi ya kandanda. Klabu maarufu ya AFC Leopards huchezea mechi zao mengi za kinyumbani huko. Uwanja huu pia hutumika kwa Riadha na sherehe mbalimbali. Vifaa vingine katika uwanja wa nyayo ni pamoja na Gym na mita hamsini ya pahali pa kuogelea. Kukamilika kwa uwanja wa nyayo ulipatia Kenya nafasi ya kuwekwa katika jamii ya Mataifa yalioalikwa kushindania kuandaa michezo ya nne ya Pan African games mwaka wa 1987. Kenya ilinyakua nafasi hii na kuipa sifa kimataifa. Hivi uwanja wa kitaifa wa nyayo ulisababisha kujengwa kwa uwanja wa kimataifa wa Moi. Uwanja wa nyayo ulibadilishwa jina na kuwa uwanja wa kitaifa wa coca cola, baada ya kampuni hii ya kimataifa kushinda haki za kuipa jina mwezi wa februari 2009. Mpango huo alikuwa wa thamani ya dola milioni 1.5, na kampuni hii ya coca cola ingeweza kuipa jina, na kuirekebisha kwa miaka mitatu. Miezi mitatu tu baadaye, Coca Cola ilijiondoa kutoka kwenye mkataba, kwa sababu serikali ya Kenya ilitaka jina ya uwanja uwe uwanja wa kimataifa wa nyayo coca cola. Makao makuu ya Shirikisho la Soka Kenya na Athletics Kenya, iko uwanja mkuu wa Nyayo. Yafuatayo ni orodha kina ya miundombinu katika uwanja;

                                     

1. a) Uwanja Mkuu.

Miundo mikuu

 • Uwanja wa kandanda ni wa kiwango iliyokubaliwa na FIFA
 • Floodlights.
 • kituo cha vyombo vya habari kilicho na mtandao.
 • Inakalisha watu 30.000.
 • Vyumba viwili vya kifahari vya mapumziko, na ofisi.
 • Sherehe kama vile siku ya likizo ya kitaifa, mikutano, na hafla za kidini hufanyiwa huko.
                                     

2. c) Indoor Gymnasium.

Miundo mikuu

 • Mbinu za kisasa za kuhesabu alama.
 • Uwanja kuu iliyo ndani ya jengo - Ndipo ligi ya kitaifa ya mpira wa kikapu inpoendeleza hafla zake.
 • Mpira wa kikapu, dondi, Badminton, Martial arts na ustawi wa utendaji.
 • Uwanja ulioko ndani na ambayo imefunikwa.
 • Inaweza kushikilia watu 2500.
 • Chumba cha kukulia.
                                     

3. Viunganish vya nje

 • Photos Archived Oktoba 22, 2007 at the Wayback Machine. saa fussballtempel.net
 • Photo saa worldstadiums.com
 • Michezo Stadia Management Board - mwili stadiums chache zinazotawala nchini Kenya

Majiranukta kwenye ramani: 1°18′15.1″S 36°49′28.1″E