Back

ⓘ Mdororo Mkuu
Mdororo Mkuu
                                     

ⓘ Mdororo Mkuu

Mdororo Mkuu ulikuwa kipindi ambacho uchumi wa Marekani na sehemu nyingine za dunia ulikuwa mbaya sana. Ulianza na Kuanguka kwa Soko la Hisa la Marekani 1929. Bei za masoko katika Soko la Hisa la Marekani zilianguka kuanzia tarehe 24 Oktoba hadi 29 Oktoba 1929. Watu wengi sana walipoteza kazi zao. Watu wengi wakawa maskini na kutokuwa na makazi. Hii ilimaliza utajiri wa Roaring Twenties. Ile siku ambayo imesemwa kuwa mwanzo wa Mdororo Mkuu inaitwa "Black Tuesday."

Wakati Mdororo Mkuu umeanza, Herbert Hoover ndiye aliyekuwa rais wa Marekani. Watu walipiga kura kwa ajili ya rais mpya hapo 1932. Jina lake lilikuwa Franklin D. Roosevelt. Roosevelt alivyopata serikali akapata kupitisha sheria mpya na mipango ya kusaidia watu ambao walipata kuumizwa na Mdororo Mkuu. Hiyo mipango ilikuwa ikiitwa New Deal.

Mdororo Mkuu ulikuwa mbaya sana, lakini kwa msaada wa kila mmoja, kukawa na afadhali, na kila kitu kikaja kuwa sawa. Kati ya miaka 1939 na 1944 watu wengi wakapata kazi tena kwa sababu ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, na huo Mdororo Mkuu ukawa unaelekea ukingoni na maisha yakawa kawaida na si kama hapo awali.