Back

ⓘ Ulumbi
Ulumbi
                                     

ⓘ Ulumbi

Ulumbi, kwa asili ya neno, ni sifa ya matumizi bora ya lugha. Wataalamu mbalimbali wameutumia ulumbi kumaanisha "uhodari wa kutumia lugha ili kufaulisha mawasiliano" au "sifa ya kutumia maneno mengi". Wengine lakini wameutumia sawa na uwingilugha, yaani uwezo wa kutumia lugha mbili au zaidi.

Chini ya kipengele cha kwanza cha ulumbi, yaani uhodari wa kutumia lugha, kuna umahiri na umilisi.

Chini ya kipengele cha pili cha ulumbi, yaani uwezo wa kutumia lugha nyingi, kuna ujozilugha, ubadilishaji msimbo na diglosia.

                                     

1. Marejeo

  • Wamitila, Kyallo 2003," Kamusi ya Fasihi – Istilahi na Nadharia”, Nairobi: Focus Books
  • Massamba, David 2004, "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  • Buliba, Aswani, Kimani Njogu & Alice Mwihaki 2006, "Isimujamii kwa Wanafunzi wa Kiswahili", Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundation
  • TUKI 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam