Back

ⓘ Maadili
                                               

Morgunbladid

Morgunbladid ni gazeti linalochapishwa katika nchi ya Iceland,lilianzishwa na Vilhjálmur Finsen & Olaf Björnsson. Toleo la kwanza lilikuwa na kurasa nane tu lilichapishwa tarehe 2 Novemba 1913. Miaka sita baadaye, katika mwaka wa 1919,shirika la Árvakur likanunua kampuni hiyo. Jarida hili lilikuwa na uhusiano wa karibu na chama cha Independence, hasa wakati wa Vita Baridi. Wahariri wake na wanaripoti wake wa bunge waliketi katika mikutano ya bunge mpaka mwaka wa 1983,wakati Mwenyekiti wa Bodi ya Árvakur alikuwa,pia, Mwenyekiti wa chama cha Independence,Geir Hallgrímsson. Kulikuwa na uamuzi ...

                                               

Uzima wa neema

Uzima wa neema au hali ya neema katika teolojia ya Kanisa Katoliki ni uzima wa juu kabisa unaoweza kupatikana ndani ya binadamu hapa duniani kwa neema ya Mungu, kwa stahili za Yesu Kristo na kwa miminiko la Roho Mtakatifu.

                                               

Wema

Wema ni neno lenye kumaanisha kumfanyia mambo mazuri na kumfanya mwingine aweze kufurahi. Tunaweza kuwafanyia wema ndugu zetu, marafiki zetu na watu wengine wengi wanaotuzunguka. Jambo hili ni la thamani sana kwa wengine na hata kwetu wenyewe, kwa sababu mtu unayemfanyia wema unaweza ukakutana naye na akakusaidia pia, lakini kama wewe ulishindwa kumfanyia wema naye pia hatashindwa kukulipizia ubaya. Wema tunaweza kutumia neno hili kwa maana nyingi tofauti wapo watakaotumia kama jina tu kwa sababu zao binafsi na wengine kwao ni kama jambo la kumfanyia mwingine mambo mazuri. Basi pamoja na y ...

Maadili
                                     

ⓘ Maadili

Maadili ni mafundisho yanayotolewa katika nafasi mbalimbali, hasa katika malezi, ili kuelekeza binadamu atende namna ambayo inamjenga yeye na jamii nzima.

Maadili yanayohitajiwa na watu wote kimsingi ni yaleyale, lakini mazingira yanaweza kudai yatekelezwe kwa namna tofauti kiasi.

Pamoja na hayo, watu tangu zamani wametoa maadili namna maalumu kulingana na dini, utamaduni, falsafa n.k.

                                     

1. Mmomonyoko wa maadili

Mmomonyoko wa maadili ni hali ya kukiukwa kwa maadili ya jamii fulani. Mmomonyoko wa maadili umesambaa kwa kasi sana, kwa vijana kuliko wazee, hiyo yote ni kwa sababu ya vyanzo vifuatavyo.

  • Utandawazi: huo ni hali ya mabadiliko katika nyanja mbalimbali za maisha kwa mwanadamu, kama vile siasa, uchumi n.k. ili kuwa na mfanano mmoja. Lakini mabadiliko hayo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa maadili kwani vijana wamekuwa watu wa kujifananisha na maisha ya watu wa nchi nyingine, kwa mfano wanaiga namna ya mavazi. Mavazi mengi ya nyakati hizi ni mavazi ambayo yanaporomosha maadili.
  • Teknolojia: usambaaji wa teknolojia na mawasiliano kurahisishwa kwa kupitia aina mbalimbali za mitandao ya kijamii kumekuwa ni changamoto kwa vijana. Wamekuwa wakitumia muda mwingi kwa kuperuzi mitandaoni na kufuatilia habari za wasanii ambazo haziwahusu kabisa. Lakini pia vijana wameweza kujiingiza kwenye vitendo vya ubakaji, kutokana na picha au video za ngono zinazooneshwa au kupakuliwa kwenye baadhi ya mitandao na kutazamwa na vijana, kwa hiyo teknolojia nayo imechangia kwa kiasi kikubwa kuporomosha maadili ya vijana.
  • Wazazi kutotimiza wajibu wao: wazazi wengi hawafuatilii watoto: huondoka nyumbani asubuhi na kurudi usiku ambapo huwakuta wamelala, lakini hawa watoto wanaweza wakashawishiwa kununua laptop na simujanja, ambapo huweza kuporomosha maadili yao hadi watakapokuwa wakubwa kwa sababu ni kama samaki ambaye hakukunjwa angali mbichi.
  • Makundi ya rika: rika ni watu ambao wana umri mmoja au kukaribiana; mtu wa kundirika anaweza kuwa rafiki, jirani au hata mwanafunzi mwenzako. Makundi hayo kwa wakati huo inabidi yatazamwe kwa jicho la tatu, kwani huongelea zaidi mambo ya ngono, tofauti na zamani ambapo makundi hayo yalikuwa yanashauriana kuhusu upendo, usawa, haki na jinsi ya kujitegemea katika familia zao.

Swali linakuja: njia gani zitumike ili kutatua mmomonyoko wa maadili hasa kwa vijana?

                                               

Bidii

Bidii ni ile hali ya kuonyesha juhudi za dhati katika kufanya jambo fulani, kwa mfano darasani. Bidii ya mtu inaweza ikamfanya afikie malengo makubwa anayotaka na kujiona yeye ni wa juu. Pamoja na yote hayo sisi binadamu huwa tunafanya bidii ili tufikie malengo yetu tunayoyataka. Kwa kawaida tunaweza kuchochea bidii yetu na ya wengine ama kwa hamasa au motisha fulani ama kwa kitisho au adhabu fulani.