Back

ⓘ Adili
Adili
                                     

ⓘ Adili

Adili, ni uzoefu wa kutenda kiutu.

Huko Ugiriki katika karne ya 5 K.K. wanafalsafa Plato na hasa Aristotle waliorodhesha maadili mengi yanayotegemea nne za msingi maadili bawaba: busara, haki, nguvu na kiasi. Zaidi ya hayo, walionyesha kwamba haiwezekani kujipatia adili moja tu, bali uadilifu unadai mtu awe na maadili yote. Kwa mfano, haiwezekani kuwa mtu wa haki pasipo busara.

Katika Ukristo, juu ya maadili ya kiutu, mwamini anatakiwa kupokea maadili ya Kimungu yaliyoorodheshwa na mtume Paulo, yaani imani, tumaini na upendo ambayo yanaendana vilevile.