Back

ⓘ Elimu
                                               

Elimu nchini Cote dIvoire

Elimu nchini Côte dIvoire inaendelea kukabiliwa na changamoto nyingi. Kiwango cha wanaojua kusoma na kuandika kwa watu wazima bado kipo chini: mnamo 2000, ilikadiriwa kwamba 48.7% ya jumla ya wakazi wanajua kusoma na kuandika. Watoto waliowengi kati ya miaka 6 na 10 hawajaandikishwa shule. Idadi kubwa ya wanafunzi wa elimu ya sekondari ni wanaume. Mwishoni mwa elimu ya sekondari, wanafunzi wanakaa na kufanya mtihani wa mwisho. Nchi ina vyuo vikuu mjini Abidjan na huko Bouaké.

                                               

Elimu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Elimu ya umma katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ni bure, na elimu ni kiada kuanzia umri kati ya miaka 6 hadi 14. Vifo vinavyotokana na UKIMWI - vimechukua nafasi kubwa sana kwa walimu, hilo limepelekea kufungwa kwa shule za msingi zaidi ya 100 kati ya mwaka 1996 na 1998. Mwaka wa 1991, idadi kamili ya waliojiandikisha kwa ajili ya elimu ya msingi ilikuwa asilimia 56.9. Mwaka wa 2000, idadi kamili ya watoto wenye umri kati ya 6 hadi 11 walioandikishwa kwa ajili ya elimu ya msingi ilikuwa asilimia 43 pekee. Ripoti ya idadi ya mahudhurio kwa ajili ya elimu ya msingi haikupatikana katika Jamhur ...

                                               

Ganimedi (Mshtarii)

Ganimedi ni mwezi mkubwa zaidi wa Mshtarii ambayo ni sayari ya tano kutoka kwa Jua na sayari kubwa katika mfumo wa Jua. Ni pia mwezi mkubwa katika mfumo wa Jua.

                                               

Philippa Hobbs

Philippa Hobbs ni mwanahistoria na msanii na mkusanyaji wa amali za kihistoria wa Afrika Kusini. Alimaliza elimu yake kutika shule ya Mtakatifu Andrea mwaka 1972. Alisomea sanaa katika chuo cha sanaa cha Johannesburg kabla ya kumaliza shahada ya uzamili ya uchapishaji katika chuo kikuu cha sanaa Philadelphia. Aliendeleza elimu yake katika chuo kikuu cha Afrika kusini na Technikon Witwatersrand.

                                               

Doreen Sibanda

Doreen Sibanda ni mzaliwa wa Uingereza na msanii wa Zimbabwe, pia ni msimamizi wa sanaa nchini Zimbambwe. Ni mkurugenzi mtendaji wa jumba la sanaa la Taifa la Zimbambwe tangu mwaka 2004.

                                               

Ennica Mukomberanwa

Ennica Mukomberanwa ni msanii wa sanaa za uchongaji nchini Zimbabwe. Ni binti wa Grace Mukomberanwa na Nicholas Mukomberanwa. Alifunzwa na kizazi cha kwanza cha wachonga sanamu. Kazi zake zinaonyeshwa katika nyumba za maonyesho duniani kote. Ni kizazi cha tatu cha wachonga Sanaa Zimbabwe. Mnamo mwaka 2004 alizawadiwa tuzo ambayo ilimruhusu kusafiri kwenda Stockholm, Copenhagen, Scotland, na Kanada. Ni mwanafamilia katika familia ya wasanii wachongaji na wazazi wake walikuwa ndio washauri wake wakuu katika masuala ya sanaa. Ni dada wa wachonga sanaa Anderson, Netsai, Taguma, Tendai Mukomber ...

Elimu
                                     

ⓘ Elimu

Elimu kwa maana pana ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi. Katika dhana ya kiufundi, elimu ni njia ambayo hutumiwa makusudi na jamii kupitisha maarifa, ujuzi na maadili kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine.

Walimu katika taasisi za elimu huratibisha elimu ya wanafunzi wao kupitia masomo kama vile ya kuandika, kusoma, kuhesabu hisabati, sayansi na historia. Mbinu hii wakati mwingine huitwa masomo haswa tunaporejelea somo la aina fulani, kwa kawaida mbinu hii hutumiwa na maprofesa katika taasisi za masomo ya juu.

Kuna elimu maalumu kwa wale wanaohitaji ujuzi wa kitaaluma, kama vile wanaohitaji kuwa marubani. Juu ya hayo, kuna nafasi nyingi za elimu katika viwango vingine visivyo rasmi kama vile majumba ya ukumbusho, maktaba pamoja na mtandao na tajriba za maisha.

Haki ya kusoma imeweza kuelezwa kuwa haki ya msingi ya binadamu katika kifungu cha pili cha itifaki ya kwanza ya maagano ya haki za binadamu barani Ulaya kuanzia mwaka wa 1952 ambapo wanachama wote wanashurutishwa kuhakikisha elimu kwa wote. Katika kiwango cha kimataifa, Mapatano ya Umoja wa Mataifa ya haki za kiuchumi, za kijamii na za kiutamaduni katika mwaka wa 1966 yanahakikisha haki hii katika kifungu cha 13.

                                     

1. Mifumo ya elimu rasmi

Elimu ni dhana inayorejelea namna ambayo wanafunzi wanaweza kujifunza kitu:

 • Mwongozo hurejelea urahisishaji wa somo na hulenga kutambua shabaha zilizobuniwa na mwalimu au mbinu zingine za kufunza.
 • Kujifunza hurejelea masomo yenye mtazamo unaolenga kuwapa wanafunzi elimu, ujuzi na uwezo unaoweza kutumika punde tu wakamilishapo kipindi cha masomo.
 • Kufunza hurejelea matendo halisi ya mwalimu yanayonuia kupasha elimu kwa wanafunzi.
                                     

2. Elimu ya msingi

Masomo ya msingi huchukua kati ya miaka 5-7 ya kwanza ya elimu rasmi. Kwa jumla elimu ya juu hujumulisha miaka 6-8 ya masomo kuanzia mwaka wa tano au sita, lakini hutofautiana baina na kati ya nchi. Asilimia 70 ya watoto waliotimu umri wa kujiunga na shule hujiandikisha katika masomo ya msingi kote ulimwenguni na viwango hivi vinaongezeka. Chini ya Elimu kwa mipango yote inaendeshwa na UNESCO, nchi nyingi wana nia ya kufanikisha zima uandikishaji katika elimu ya msingi ifikapo mwaka 2015, na katika nchi nyingi, ni lazima kwa watoto kupata elimu ya msingi.Chini ya mpango wa elimu kwa wote ulioanzishwa na Shirika la Elimu, Sayansi na utamaduni la Umoja Wa Mataifa UNESCO, nchi nyingi zimejitolea.

                                     

3. Elimu ya sekondari shule za upili

Katika mifumo ya kisasa ya elimu ulimwenguni, elimu ya shule za upili au sekondari huchukua kipindi cha pili cha elimu rasmi ambayo hutokea wakati wa ujana wa wanafunzi. Mfumo huu hutofautian na masomo ya msingi ambayo ni ya lazima, ni ya jumla na yanayofanana.

Yale ya shule za upili ni teule na ya hiari. Shule hizi hujulikana kama sekondari, shule za upili, shule za kati, vyuo au shule za ujuzi wa kitaalamu kulingana na kipindi au mfumo unaofuatwa. Maana ya dhana hizi hutofautiana kutoka mfumo mmoja hadi mwingine. Mpaka kamili kati ya elimu ya msingi na ya upili hutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine. Tofauti hizi zipo hata katika nchi lakini kwa kijumla hutokea kati ya mwaka wa saba na wa kumi wa kusoma.

Elimu ya sekondari hutokea katika umri wa ujana. Nchini Marekani na Kanada elimu ya msingi na sekondari kwa pamoja hurejelewa kama elimu ya K-12 na katika nchini ya Nyuzilandi, elimu hii hurejelewa kama elimu ya miaka 1-13. Azma ya elimu ya sekondari ni kutoa maarifa ya kawaida, kutayarisha wanafunzi kwa elimu ya juu au kuwafunza watu kazi moja kwa moja.

Elimu ya sekondari iliibuka nchini Marekani mwaka wa 1910 na ilisababishwa na kuwepo kwa biashara kubwa na maendeleo ya kiteknolojia viwandani. Ili kuafikia mahitaji ya kazi, shule za upili zilijengwa na mtaala uliolenga maarifa ya kazi za ofisi na za sulubu ukazinduliwa. Hii ilibainika kuwa njia ya manufaa kwa mwajiri kwani uimarishaji wa huduma za kibinadamu uliwafanya waajiriwa kuwa madhubuti kazini na kushusha gharama kwa waajiri huku waajiriwa wakinufaika na mishahara minono ikilinganishwa na waliokuwa na elimu ya msingi pekee.

Barani Ulaya, shule za sarufi au akademia zilikuwepo hata katika miaka ya 1500. Shule za umma au zile za kulipa karo au hata shule za ufadhili na wakfu zina historia ndefu zaidi.

Tunapaswa kujitahidi katika kuhamasisha elimu ya sekondari kwani huwezesha kufikia chuo kikuu.                                     

4. Elimu ya juu

Elimu ya juu, yaani ile ya baada ya shule ya upili au elimu ya awamu ya tatu, si ya lazima. Elimu hii kwa kawaida hujumulisha viwango vya shahada pamoja na elimu ya ujuzi wa kitaalamu.

Kwa jumla elimu ya juu hutolewa na vyuo na vyuo vikuu na huambatana na kutolewa kwa vyeti, stashahada za diploma na shahada za digrii kitaaluma.

Masomo ya juu hujumuisha elimu, utafiti na huduma za jamii na katika uwanja wa elimu, hujumulisha viwango vya shahada ya kwanza na nyingine za juu. Elimu ya juu aghalabu huhusu kufuzu katika kiwango cha shahada ya kwanza, ya uzamili na ya uzamifu.

Idadi kubwa ya watu katika nchi zilizoendelea hadi kufikia asilimia 50 wameweza kupata elimu ya juu wakati fulani maishani mwao. Kwa hiyo, elimu ya juu ni muhimu kwa uchumi wa taifa, ni kiwanda cha pekee ambacho huzalisha wafanyakazi walioelimika.

Katika nchi maskini serikali zinatakiwa kuongeza mikopo kwa wanafunzi wa vyuoni ili waweze kupata elimu hiyo na kusonga mbele, kwa kuwa elimu ni ufunguo wa maisha.

                                     

5. Elimu ya watu wazima

Elimu ya ngumbaru au ya watu wazima imekuwa kawaida katika nchi nyingi. Elimu hii huchukua maumbo mengi yakiwemo elimu rasmi darasani, elimu ya binafsi na masomo ya mtandao. Idadi fulani ya kozi za kazi maalum kama vile elimu ya mifugo, masuala ya madawa, uwekezaji, uhasibu na kozi nyinginezo kwa sasa hupatikana mtandaoni.

                                     

6. Elimu mbadala

Elimu mbadala, ambayo pia hujulikana kama elimu isiyo rasmi, ni dhana yenye maana pana na inayoweza kutumiwa kurejelea aina zote za elimu zilizo nje ya elimu ya kawaida kwa watu wote na viwango vyote vya elimu.

Hujumuisha si tu mitindo ya elimu inayokusudiwa wanafunzi wenye mahitaji ya pekee lakini pia mitindo inayolenga hadhira ya jumla na kutumia mitindo na falsafa badala ya elimu.

Elimu mbadala mara nyingi huwa matokeo ya mabadiliko katika elimu yaliyotokea katika misingi mbalimbali ya falsafa ambayo kwa kawaida ni tofauti na elimu ya jadi ya lazima. Mabadiliko mengine yana misingi ya kisasa, kiutafiti au kifalsafa, ilhali mengine ni miungano isiyo rasmi kati ya walimu na wanafunzi wasioridhika na masuala fulani ya elimu hiyo ya jadi.

Elimu mbadala hii ambayo ni pamoja na shule za tabia, shule badala, shule zinazojitegemea na masomo ya nyumbani hutofautiana pakubwa, lakini zote hutilia maanani umuhimu wa idadi ndogo ya wanafunzi darasani na mahusiano ya karibu kati ya wanafunzi na walimu. Vilevile husababisha hali ya umoja.                                     

7. Elimu ya asili

Kuongezwa kwa ruwaza za elimu ya asili mbinu na maudhui yake ndani ya elimu badala katika eneo la mfumo wa elimu rasmi na elimu isiyo rasmi kumewakilisha kipengele muhimu kilichochangia ufanisi wa mfumo wa elimu asili kwa wanajamii asili walioamua kufuata njia hii; hii ikiwa ni pamoja na wanafunzi na walimu.

Kuingizwa kwa mbinu za asili kama vile kujua, kusoma, kuelekeza, kufunza na kusoma kama njia nzuri ya kuhakikisha kuwa wanafunzi/wanagenzi na walimu/waelekezi wanaweza kufaidika kutokana na elimu kwa njia ya kiasili iliyokuza, kutumia na kuendeleaza uhamasishaji wa tamaduni za kiasili.

Kwa wanafunzi au wagenzi na walimu au waelekezi, kuwekwa pamoja kwa mbinu hizi mara nyingi huongeza fanaka, matarajio na matokeo ya elimu. Hili huafikiwa kwa kutoa elimu inayooana na taswira zao za asili, mazoea na mitiazamo yao ya ulimwengu. Kwa wanafunzi na walimu wasio wa asili, elimu ya aina hii ina athari ya kuongeza ufahamu wa tamaduni zao za kibinafsi na mazoea ya jumla ya umma na watu wanaowazunguka, hivyo basi kukuza heshima na kuthamini tamaduni za wanajamii hizo.

Katika elimu na mafunzo, kujumuishwa kwa maarifa ya kiasili, tamaduni, maono, mitazamo na dhana katika mitaala, vifaa vya kuelekeza na vitabu vya kozi vina athari kubwa kama ile ya kujumuisha mbinu za asili katika elimu ambayo hunufaisha walimu na wanafunzi katika usambamba wa masomo, kufaulu na matokeo ya masomo hayo. Ambayo hunufaisha walimu na wanafunzi katika usambamba wa masomo, kufaulu na matokeo ya masomo hayo. Walimu na wanafunzi wa kisasa wana heshima, hamasa na maridhio kwa jamii na watu wa kienyeji kutokana na elimu husishi wanayopata.

Mfano mkuu unaoonyesha mbinu na maudhui ya asili yanaweza kukuza matokeo yaliyotajwa hapo juu undhihirika katika elimu ya juu nchini Kanada. Kwa sababu ya sheria fulani, dhamira ya kuongeza mafanikio kwa wanafunzi wa elimu asili na kukuza maadili ya jamii ya kitamanduni, kuingizwa kwa mbinu na maudhui ya asili katika elimu huonwa kuwa jukumu na wajibu wa serikali na taasisi za elimu zenye mamlaka.

                                     

8. Mitaala

Somo la taaluma ni tawi la elimu ambalo hufunzwa kirasmi katika vyuo vikuu ama kupitia njia zingine kama hizo. Kwa kawaida, kila somo huwa na masomo mengine ama matawi na mipaka ya kuyabainisha mara nyingi huwa si dhahiri na mara nyingine husababisha utata. Mifano ya masomo ya kitaaluma yenye upana ni kama vile sayansi asilia, hesabu, sayansi ya komputa, sayansi za jamii, sayansi za binadamu na sayansi za matumizi.

                                     

9. Mitindo ya kujifunza

Kuna utafiti uliofanywa kuhusu mitindo ya kusoma katika miongo miwili iliyopita. Dunn na Dunn walilenga kutambua vichangamshi husishi vinavyofanya masomo yavutie na namna ya kutawala mazingira ya shule. Baadaye Joseph RenzulLi alipendekeza mikAkati tofautitofauti ya kufunza. Howard Gardner alitambua talanta ama vipaji vya mtu binafsi katika nadharia zake za akili nyingi. Kwa misingi ya kazi za C. G. Jung" Kielezi Aina cha Myers Briggs” na" kitenga tabia cha Keisresy” vililenga kuelewa jinsi nafsi za watu huathiri uhusiano wa mtu binafsi na zinavyoathiri maelewano ya watu katika mazingira ya kujifunza. Kazi za David Kolib na Anthony Gregorc" jinsi ya kusawiri” ” hufuata mfano kama huu lakini uliorahisishwa.

Kwa wakati huu, kugawika kwa elimu katika mitindo tofautitofauti hukubalika na wengi. Huenda ikawa kuwa mitindo ya kujifunza ndiyo ya kawaida:

 • Masomo husishi: Kusoma kwa misingi ya kutumia mikono na vitendo husishi.
 • Kuona: Masomo yenye misingi ya kutazama kwa makini na kuona kile kinachosomwa.
 • Kusikiza: Kusoma kwa misingi ya kusikiliza maelezo/habari.

Imedaiwa kuwa kulingana na mtindo wa kujifunza unaopendelewa, mbinu tofautitofauti za kufunza huwa na matokeo ya viwango tofauti. Umuhimu wa nadharia hii ni kuwa kunakofaa, inapaswa kutumia mbinu mbalimbali za kufunza zinazojumulisha mitindo yote mitatu ya kufunza ili wanafunzi tofautitofauti wapate fursa ya kujifunza kwa njia inayowafaa. Guy Claxton ametilia shaka mitindo ya kujifunza kama vile VAK kwani kwa kiasi fulani mitindo hii ina mazoea ya kupachika watoto majina hivyo basi kuwazuia kujifunza.

                                     

10. Kujifunza

Kujifunza ni kutaka kujua juu ya jambo fulani ambalo hukulijua kabla. Hata jambo zuri kuhusu kujifunza ni kwamba hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kukiweka mbali nawe kitu hicho ambacho umejifunza.

Walimu wanapaswa kuelewa somo vilivyo ili kuwasilisha umuhimu wake kwa wanafunzi. Shabaha hapa ni kuunda misingi ya ujuzi kamili ambayo wanafunzi wanaweza kutumia kujijenga zaidi kwani wamewekwa wazi kwa matukio mbalimbali ya maisha. Walimu wazuri huweza kutafsiri habari kama hukadiria vizuri, hutumia mazoea na hekima hadi kwa elimu husika ambayo mwanafunzi anaweza kuelewa, kuhifadhi na kupititishia wengine.

Utafiti kutoka Marekani unatoa maoni kuwa ubora wa walimu ndio kigezo kinachoathiri mafanikio ya wanafunzi, na kuwa nchi zinazopata alama za juu katika mtihani au majaribio ya kimataifa zimeweka sera chungu nzima zinazohakikisha kuwa walimu wanaoajiriwa ndio bora.

                                     

11. Teknolojia

Teknolojia ni kigezo muhimu katika elimu. Tarakilishi na simu za rununu zinatumiwa katika nchi zilizoendelea kuimarisha elimu iliyothibitishwa na kukuza njia mpya za elimu kama vile elimu ya mtandao masomo ya mbali. Wanafunzi hupata fursa ya kuchagua wanachotaka kusoma.

Kuenea kwa tarakilishi pia kunamaanisha kuongezeka kwa programu za kompyuta na kuongeza habari mtandaoni. Teknolojia hutoa vifaa muhimu vinavohitaji ujuzi mpya na uelewa wa wanafunzi zikiwemo njia nyingi za mawasiliano, na huleta njia mpya za kuhusisha wanafunzi kama vile mazingira ya kujifunza.

Teknolojia inatumiwa si tu katika wajibu wa kutawala katika elimu bali pia katika kuwaelekeza wanafunzi. Matumizi ya teknolojia kama vile virusha maandishi power point na ubao mweupe hutumiwa kunasa akili za wanafunzi darasani. Teknolojia vilevile hutumiwa kuwatahini wanafunzi. Mfano mzuri ni mfumo wa kuvutia hadhira ARS,ambao huruhusu majibu ya mitihani moja kwa moja pamoja na majadiliano darasani.

Teknolojia pia imekuwa mojawapo wa maktaba katika elimu ambamo vitabu, ripoti za utafiti, tansifu n.k. huchapishwa. Tovuti zinazochapishwa vitabu, ripoti na tansifu zimekuwa za manufaa kwa wasomi. Zinawapa uwezo wa kupata vitabu maalum kwa ujumbe fulani tofauti na maktaba za kizama ambazo humlazimu mtu kusoma kwa urefu na upana kupata ule ujumbe. Tofuati hizi hufuata mpangilio, nyingine zikiruhusu watumizi kupakua vitabu bila malipo, nyingine zina malipo ya muda, ilhali nyingine hulazimu mtu kununua kile kitabu anachokihitaji.

Teknolojia za habari na mawasiliano ICT ni "seti ya vifaa na rasilimali mbalimbali zinazotumiwa kuwasiliana, kuunda, kueneza na kuongoza habari." Teknolojia hizi ni pamoja na kompyuta, mtandao, teknolojia za kusambaza habari redio na televisheni na simu kuongea na pia kwa ujumbe wa maandishi. Kuna mvuto unaoongezeka kuhusu namna tarakilishi na mtandao vinavyoweza kuimarisha elimu katika viwango vyote, yaani mseto wa elimu rasmi na ile isiyo rasmi.

Teknolojia za habari na mawasiliano za awali, kama vile redio na televisheni, zimetumiwa kwa zaidi ya miaka 40 kwa elimu wazi na ile ya mbali, hata hivyo kupiga chapa ndiyo njia nafuu zaidi, inapatikana kwa urahisi, na hivyo basi ni mbinu iliyotawala katika nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea.

Matumizi ya tarakilishi na mtandao ikiwa vinatumika bado ni changa katika nchi zinazoendelea, na hii ni kwa sababu miundo msingi ni michache na ghali. Kwa kawaida teknolojia kadhaa hutumiwa kwa pamoja bali si mbinu pekee ya kupokelewa. Kwa mfano, Kothmel Community Radio Internet hutumia matangazo ya redio na kompyuta pamoja na teknolojia ya mtandao, na hivyo hurahisisha kugawa habari na kutoa nafasi za elimu katika kijiji fulani Sri Lanka.

Chuo Kikuu cha Uingereza UKOU kilichoanzishwa mwaka wa 1969 kama taasisi ya elimu ya kwanza ulimwenguni kujitolea kutoa elimu ya wazi na ya mbali, bado hutegemea vifaa vilivyopigwa chapa na kuongezea redio, runinga na kompyuta. Vivyo hivyo, Chuo Kikuu cha Indira Gandhi nchini India huweka pamoja matumizi ya chapa, sauti zilizorekodiwa, video, redio, televisheni na teknolojia ya vielezo vya kusikiza mkutano.

Dhana ya" masomo yanayosaidiwa na kompyuta” CAL limetumiwa kwa wingi kuelezea teknolojia katika masomo.                                     

12. Nadharia ya elimu

Nadharia ya elimu ni nadharia ya azma, matumizi na ufafanuzi wa elimu na kusoma. Historia yake inatokana na wataalamu wa elimu kutoka Ugiriki kuanzia karne ya 18. Katika karne ya 20 mbinu za kusoma zimetumia nadharia katika kufunza, kutathmini na katika sheria za elimu ambazo hupatikana katika vitengo mbalimbali kama ifuatavyo:

                                     

13. Uchumi

Sababu zimetolewa kuwa kiasi cha juu cha elimu ni muhimu kwa nchi ili kuwezesha ukuaji haraka wa uchumi. Uchunguzi unaotegemea nadharia huunga mkono nadharia za kutabiri kuwa nchi maskini zinapaswa kukua haraka kuliko nchi tajiri kwani nchi hizi zinaweza kutumia teknolojia mpya kabisa ambayo imeshajaribiwa na nchi tajiri.

Hata hivyo, kuhamisha teknolojia kunahitaji viongozi wenye maarifa na wahandisi wenye uwezo wa kutumia mashine mpya ama mazoezi ya uzalishaji yaliyokopwa ili kuziba mpaka kwa miigo. Hivyo basi, uwezo wa nchi wa kujifunza kutoka kwa nchi kiongozi ni jukumu la wafanyakazi wa nchi hiyo.

Utafiti wa hivi karibuni wa vitambulishi vya kujumuisha ukuaji wa kiuchumi umesisitiza umuhimu wa vyuo asili vya uchumi na majukumu ya ujuzi tambuzi.

Katika kiwango cha mtu binafsi, kuna maandishi yenye uhusiano na kazi ya Jacob Mincer, ya jinsi mapato yanahusiana na elimu na rasilimali ya mtu binafsi. Kazi hii imetia motisha idadi kubwa ya utafiti lakini pia inaelekea kuleta mabishano kwa kiasi fulani. Ubishi mkubwa unahusu jinsi ya kufasiri matokeo ya kusoma.

Wataalamu wa uchumi Samwel Bowels na Herbert Ginits walitoa maoni kwamba kulikuwa na ubishi asili katika elimu nchini Marekani kati ya shabaha ya demokrasia shirikishi yenye usawa na faida ya mapato ya kibepari yaliyodokeza hali ya kutokuwa na usawa.

                                     

14. Historia ya elimu

Historia ya elimu ilianza miaka mingi iliyopita, kwa kuwa elimu kama sayansi haiwezi kutengwa na utamaduni wowote wa elimu iliyokuwepo awali. Wakubwa waliwafunza wadogo wao juu ya jamii kwa kutumia maarifa na ujuzi waliohitaji kufahamu na mwishowe kupitisha.

Mabadiliko ya utamaduni na binadamu kama spishi yalitegemea mazoea ya kupitisha elimu. Katika jamii ambazo hazikujua kusoma, hili liliafikiwa kupitia mdomo na kuiga. Kusimuliana hadithi kuliendelezwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Lugha ya mazungumzo iliendelea na kuwa ishara na herufi. Kina na upana wa elimu au maarifa ulioweza kuhifadhiwa na kupitishwa uliongezeka zaidi na zaidi. Wakati ambapo tamaduni zilianza kupanua elimu zaidi ya ujuzi wa kawaida wa mawasiliano, biashara, ukusanyaji chakula, tunu na desturi za kidini na kadhalika, mwishowe elimu rasmi na masomo vilifuatia. Kisomo kwa maana hii kilikuwa kimeshaanza nchini Misri kati ya 3000 na 500 KK.

Siku hizi aina fulani ya elimu ni jambo la lazima kwa watu wote katika nchi nyingi. Kwa sababu ya ongezeko la watu na kuenea kwa elimu ya lazima, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO limepiga hesabu ya kwamba miaka 30 ijayo, watu wengi zaidi ulimwenguni watapata elimu rasmi katika historia ya binadamu.

                                     

15. Falsafa ya elimu

Falsafa ya elimu ni utafiti wa kifalsafa juu ya kusudi, utaratibu na ubora wa elimu kwa kuchunguza ufafanuzi, malengo na maana ya elimu kwa jumla au ya mtazamo mmojawapo juu yake.

Falsafa ya elimu kwa kawaida huonwa kama tawi la falsafa na la elimu.

Falsafa ya elimu mara nyingi hubaki ndani ya falsafa na elimu, ilhali ni falsafa matumizi, iliyotokana na nyanja za zamani za falsafa na njia kisia, taswira na tafiti, mbinu na mtaala, nadharia, kwa kutaja tu chache.

                                     

16. Saikolojia ya elimu

Saikolojia ya elimu ni uchunguzi wa jinsi watu hujifunza katika mandhari ya elimu, ufaafu wa maingiliano ya elimu, saikolojia ya kufunza na saikolojia jamii za shule. Ingawa maneno" saikolojia ya kielimu” na" saikolojia ya shule" mara nyingi hutumiwa kwa kubadilishana, watafiti na wananadharia wanaweza kutambuliwa kama wanasaikolojia wa elimu, ilhali weledi wanaopatikana shuleni au mandhari yanayoana na shule hujulikana kama wanasaikolojia wa shule. Saikolojia ya elimu inajishughulisha na utaratibu wa kutoa elimu kwa watu na umma kwa jumla na umma mdogo, kama vile watoto wenye vipaji na wale wenye ulemavu.

Saikolojia ya elimu inaweza kueleweka kwa sehemu kupitia masomo mengine. Saikolojia ya elimu vilevile huarifiwa na saikolojia, ikileta uhusiano baina ya utabibu na biolojia. Saikolojia ya elimu pia huarifu masafa mapana ya masomo maalum yakiwemo mpango wa mafunzo. Teknolojia ya elimu, mtaala uliokuzwa, masomo yaliyopangwa, masomo maalumu, sayansi tambuzi na sayansi masomo. Katika vyuo vikuu, idara za elimu ya saikolojia zimehifadhiwa katika vitivo vya elimu. Hii ni kwa sababu ya uwezekano wa ukosefu wa uwakilishaji wa maudhui ya saikolojia ya elimu katika utangulizi wa vitabu vya saikolojia.

                                     

17. Sosholojia ya elimu

Sosholojia ya elimu ni somo linalohusu jinsi taasisi za kijamii na kani huathiri michakato na matokeo ya elimu, na kinyume chake. Kwa wengi, elimu hueleweka kama mbinu ya kushinda vizuizi, kufanikisha usawa na kupata amani na hadhi kwa wote Sargent 1994. Wanafunzi wanaweza kutiwa motisha na hamu ya maendeleo na uboreshaji. Elimu hutambuliwa kama mahali ambapo watoto huweza kujikuza kulingana na mahitaji yao ya pekee. Jukumu la elimu linaweza kuwa ni kukuza mtu binafsi hadi kilele. Uelewa wa shabaha na mbinu za michakato ya utangamano wa kielimu hutofautiana kulingana na dhana ya sosholojia iliyotumika.

                                     

18. Maendeleo ya elimu

Katika nchi zinazoendelea idadi na uzito wa shida zilizoko kwa kawaida ni kubwa. Watu wa vijijini wakati mwingine huwa hawana habari kuhusu umuhimu wa elimu. Hata hivyo, nchi nyingine zina wizara ya elimu na katika masomo mengi, kama vile kujifunza lugha za kigeni, kiwango cha elimu kimo juu kuliko katika nchi zilizoendelea. Kwa mfano, katika nchi zinazoendelea ni kawaida kupata wanafunzi wakizungumza lugha nyingi za kigeni kwa usanifu mkubwa, ilhali jambo hili ni nadra katika nchi zilizoendelea ambapo idadi kubwa ya watu huzungumza lugha moja.

Vilevile kuna shinikizo la kiuchumi kutoka kwa wazazi ambao hupendelea watoto wao wapate pesa kwa muda mfupi kuliko faida za elimu ya muda mrefu. Utafiti wa hivi karibuni kuhusu ajira ya watoto na umasikini zimependekeza kuwa familia zilizokumbwa na umasikini zinapofikia kiwango fulani cha kukidhi mahitaji yao ya kimsingi, wazazi huwarejesha watoto wao shuleni. Hii imethibitshwa kuwa kweli mara tu kizingiti kinapovukwa. Hata kama uwezekano wa thamani ya kiuchumi ya ajira ya watoto inaongezeka baada yao kurudishwa shuleni.

Ukosefu wa vyuo vikuu bora na kiwango cha chini cha kukubalika katika vyuo hivi ni dhahiri katika nchi zilizo na idadi kubwa ya watu. Baadhi za nchi zina mitaala mikuu inayoweza kubadilika kwa urahisi, inayofanana na yenye miundo zaidi.

 • Kutokana na utandawazi shinikizo kwa wanafunzi katika shughuli za mtaala zimeongezeka
 • Kuondolewa kwa asili mia fulani ya wanfunzi kwa ajili ya uboreshaji wa masomo kwa kawaida hufanywa shuleni baada ya daraja la kumi

India inakuza teknolojia na mtandao. India ilizindua EDUSAT, elimu ya setilaiti ambayo inaweza kuwafikia wengi kwa gharama ya chini. Kuna pia mpango ulioanzishwa na shirika la OLPC, kundi lililotokana na maabara ya MIT lililoungwa mkono na mashirika makuu ili kukuza kompyuta ya kupakata ambayo ingeghalimu $100, ili kuwezesha kuwasilisha elimu ya programu ya kompyuta. Kompyuta hizi zimesambaa kote kufikia mwaka wa 2009. Kompyuta hizi zinauzwa au kutolewa kama msaada. Hii itawezesha nchi zinazoendelea kuwapa watoto wao elimu kwa kutumia mitambo.

Barani Afrika, shirika la NEPAD limezindua programu ya masomo ya mtandao inayotoa vifaa vya kompyuta na masomo ya mtandao kwa shule zote za msingi na upili kwa kipindi cha miaka kumi. Vikundi vya binafsi kama vile Wamormoni, wanajikakamua kuwapa watu fursa ya kupokea elimu katika nchi zinazoendelea kupitia miradi kama vile Perpetual Educational Fund. Mradi wa maendeleo kimataifa inayofahamika kama nabuur.com, com iliyoanza kwa msaada wa rais wa Marekani Bill Clinton, hutumia mtandao kuwezesha ushirikiano wa watu binafsi kuzungumzia maswala ya maendeleo ya jamii.

                                     

18.1. Maendeleo ya elimu Umataifishaji

Elimu inaendelea kuwa jambo la kimataifa. Si vifaa vyake tu vinavyoendelea kuathiriwa na mazingira ya kimataifa yenye ukwasi bali pia mabadiliko ya wanafunzi katika viwango vyote yanayochangia kuendesha jukumu hili muhimu. Kwa mfano kule Uropa, programu ya Socratis Erusmus imechechemua mabadilishano kati ya vyuo vikuu vya Uropa. Vile vile, Shirika la Soros hutoa fursa nyingi kwa wanafunzi kutoka Asia ya kati na Uropa mashariki. Wasomi wengi hudai kwamba ingawa mfumo fulani unaweza kuzingatiwa kuwa bora au mbaya kuliko mwingine, kuzoea aina tofauti ya elimu mara nyingi huonwa kuwa elementi muhimu ya kuzoea masomo ya kimataifa.

                                     

19. Dini na elimu

Elimu katika dini ya Uislamu ni muhimu kwa wake na waume, haswa kwa watoto wadogo. Kinyume na dhana ya kawaida, kutafuta aina zote za maarifa, yawe ya kitaaluma, ya kidini au ya kidunia yanaruhusiwa kwa watu wa umri wowote. Hata hivyo, masomo ya umri mdogo huonwa kuipa akili fursa ya kumakinika bila kuathiriwa na shida na majukumu ya maisha ya utu uzima.

                                     

20. Tazama pia

 • Teknolojia ya kuelekeza
 • Elimu ya umma
 • Jamii inayotumia masomo ya mtandao
 • Shule
 • Elimu ya juu
 • Masomo ya mtaala
 • Elimu ya mbali
 • Ufundishaji
 • Chuo Kikuu
 • Jamii inayosoma
 • Kujifunza
 • Uainishaji wa malengo ya elimu
 • Elimu ya ziada
 • Elimu ya lugha
 • Elimu ya amani
 • Elimu ya katuni
 • Elimu ya sheria
 • Elimu linganishi
 • Historia ya elimu
 • Mbinu mwafaka ya elimu
 • Elimu mbadala
 • Elimu ya majaribio
 • Elimu ya kale
 • Udanganyifu katika elimu
 • Sayansi ya kusoma
 • Elimu ya kushirikiana
 • Elimu ya watu wazima
 • Elimu ya makazi
 • Shule ya siku zijazo
 • Elimu ya kiufundi
 • Elimu ya jinsia moja
 • Mabadiliko ya elimu
 • Falsafa ya elimu
 • Utafiti wa elimu
 • Elimu ya matibabu
 • Elimu ya biashara
 • Elimu ya mtandao
 • Elimu ya kukua
 • Kisomo cha nyumbani
 • Elimu ya kielezo
 • Mtaala
 • Sosholojia ya elimu
 • Elimu ya kuhitimu
 • Mwalimu
 • Elimu ya teknolojia
 • Elimu ya maishani
 • Faharasa ya maneno yenye uhusiano na elimu
 • Elimu ya vipaji
 • Orodha ya walimu
 • Elimu kwa mahitaji maalum
 • Elimu ya kweli na sawa
 • Kusoma kwa kufundisha LdL
                                     

21. Viungo vya nje

 • Elimu kwa wote – Uwanja wa Kujifunza kwa Urahisi
 • Historia ya elimu Archived Oktoba 12, 2017 at the Wayback Machine.
 • Mifano mbalimbali ya teknolojia inavyoimarisha elimu Afrika
 • Elimu kwa teknolojia ya simu, video na mtandao
 • OECD takwimu za elimu
 • UNESCO Taasisi ya Takwimu: International kulinganishwa mifumo ya takwimu za elimu Archived Mei 15, 2007 at the Wayback Machine.
 • Education katika Open Directory Project
 • Educational Resources Archived Aprili 10, 2005 at the Wayback Machine. kutoka UCB Libraries GovPubs
                                     
 • Elimu nchini Kenya imekuwa ikizingatia mfumo wa 8 - 4 - 4 tangu mwishoni mwa miaka ya 1980, ikiwa ni miaka minane ya elimu ya msingi, ikifuatiwa na miaka minne
 • Elimu katika Afrika ilianza kama chombo cha kuandaa vijana wake kuchukua nafasi yao katika jamii ya Afrika. Uzoefu wa elimu ya Kiafrika ilianzishwa hasa
 • Elimu ya sekondari shule za upili katika mifumo ya kisasa ya elimu ulimwenguni, huchukua kipindi cha pili cha elimu rasmi ambayo hutokea wakati wa ujana
 • Elimu ya juu, yaani ile ya baada ya shule ya upili au elimu ya awamu ya tatu, si ya lazima. Elimu hii kwa kawaida hujumulisha viwango vya shahada pamoja
 • Wizara ya Elimu Sayansi, Teknolojia na Ufundi Tanzania kwa Kiingereza: Ministry of Education, Science, Technology and Vocational Training kifupi ni
 • Masomo ya msingi huchukua kati ya miaka 5 hadi 8 ya kwanza ya elimu rasmi. Kwa jumla elimu ya juu hujumulisha miaka 6 - 8 ya masomo kuanzia mwaka wa tano
 • Elimu nchini Tanzania hutolewa na sekta zote mbili, yaani, sekta za serikali na binafsi. Muundo wake kiujumla ni kama ifuatavyo: Miaka 2 elimu ya vidudu cheke - chea
 • serikali zinazoitwa Wizara ya Elimu au Wizara ya Elimu ya Umma Wizara ya kwanza kabisa inafikiriwa kuwa Tume ya Taifa ya Elimu pl. Komisja Edukacji Narodowej
 • Elimu mbadala, ambayo pia hujulikana kama elimu isiyo rasmi, ni dhana yenye maana pana na inayoweza kutumiwa kurejelea aina zote za elimu zilizo nje ya
 • Falsafa ya elimu ni utafiti wa kifalsafa juu ya kusudi, utaratibu na ubora wa elimu kwa kuchunguza ufafanuzi, malengo na maana ya elimu kwa jumla au
 • Elimu kama kipaji cha Roho Mtakatifu ni utayari wa Mkristo kuangaziwa na Roho Mtakatifu kuhusu mambo ya duniani ili kuelewa kasoro zake. Hivyo haitegemei
 • Sosholojia ya elimu ni sayansi inayohusu uhusiano ya elimu na jamii. Kwa upana zaidi, elimu ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama
                                               

Beth Diane Armstrong

Beth Diane Armstrong ni msanii wa sanaa za uchongaji, huku ujuzi wake, wa kiwango kikubwa cha usimamiaji wa miradi mikubwa imemruhusu kuchukua jukumu na sehemu ya wanaume wengi wa Afrika ya Kusini. Kwa miaka ya mwisho amefanya kazi za sanaa nyingi ikiwemo uchongaji, uchapishaji, video, kupiga picha na kuchora.

Julia Rosa Clark
                                               

Julia Rosa Clark

Julia Rosa Clark ni msanii na muelimishaji wa Afrika Kusini Anajulikana zaidi kwa aina yake ya sanaa za rangi za picha ya makaratasi

                                               

Fatou Camara

’’Camara’’’ ni mtoto wa kike wa ’’Modou Lamin Camara’’’ na ’’Fatou Njie’’’. Alisomea elimu ya msingi katika shule ya Msingi ya Walemavu wa Ngozi ’Albion Primary School’’na baadae elimu ya kati katika ’Gambia High School’’.

                                               

Barolong Seboni

Mzaliwa wa Kanye, Botswana, Botswana, alipokea Shahada yake kutoka University of Botswana na shahada yake ya uzamili kutoka chuo kikuu cha University of Wisconsin – Madison.Ametafsiri methali za Botswana kwa Kiingereza. Alikuwa pia na safu katika "Mlinzi wa Botswana" na amefanya kazi katika vyombo vingine ikiwa ni pamoja na redio.

Gifty Anti
                                               

Gifty Anti

Gifty Anti ni mwandishi wa habari na mtangazaji mzaliwa wa Ghana. Yeye ndiye mwendeshaji mwenyeji wa kipindi kinachozungumzia Standpoint Archived Mei 26, 2021 at the Wayback Machine. masuala yanayoathiri wanawake kwenye kituo cha GTV Televisheni ya Ghana. Anajulikana kwa kutetea haki za wanawake. Amepata elimu yake Alma mater Mfantsiman shule ya wasichana ya Secondari na Chuo cha "Ghana Institute of Journalism".

                                               

Chuo Kikuu cha Bagamoyo

Chuo Kikuu cha Bagamoyo ni chuo kikuu cha binafsi nchini Tanzania. kilianzishwa na Tanzania Legal Education Trust pamoja na kituo cha kutetea haki za binadamu Tanzania, chuo hiki kinapatikana katika mkoa wa Dar es Salaam na kampasi kuu ipo eneo la Kiromo, Bagamoyo.

                                               

Rema Namakula

Rema alizaliwa katika hospitali ya Lubaga, tarehe 24 Aprili 1991, kwa marehemu Hamida Nabbosa na marehemu Mukiibi Ssemakula. Yeye ndiye mzaliwa wa mwisho katika familia yake. Alisoma Shule ya Msingi Kitante. Alisoma pia Shule ya Sekondari ya Saint Balikudembe kwa masomo yote ya O-Level na A-Level. Baadaye, alijiunga Chuo Kikuu cha Kyambogo ambayo hakuwahi kumaliza na anasema ana mpango wa kufanya hivyo baadaye.

                                               

Doris Jean Austin

Doris Jean Austin alizaliwa mwaka 1949 katika jimbo la Alabama, nchini Marekani, alilelewa na mama na bibi yake. Austin alihamia katika mji wa New Jersey akiwa na umri wa miaka sita na kusoma katika shule ya Lincolin High School, alianza kuvutiwa katika uandishi wa vitabu na mwalimu wake wa somo la Kiingereza alokuwa akijulikana kama Ercell Webb, Austin alilelewa katika nyumba ya Wasabato, alifariki mwaka 1994

                                               

Tamara Winfrey Harris

Winfrey Harris ni muandishi wa vitabu na kitabu chake cha kwanza ni The Sisters Are Alright: Changing the Broken Narrative of Black Women in America kilichochapishwa mwezi Mei mwaka 2015 na kushinda tuzo ya Phyllis Wheatley Award pamoja na tuzo ya Living Now Award pamoja na IPPY Award. kitabu chake cha pili ni Dear Black Girl: Letters From Your Sisters on Stepping Into Your Power, kilicho pangwa kutoka mwaka 2021 mwezi Machi