Back

ⓘ Rejista
                                     

ⓘ Rejista

Rejista ni matumizi ya lugha kulingana na muktadha maalum. Miktadha tofauti husababisha aina mbalimbali za lugha.

Baadhi ya vipengele vya miktadha hiyo ni:

 • Umri
 • Mada
 • Wakati
 • Mazingira
 • Uhusiano baina ya wahusika
 • Cheo
 • Ujuzi wa lugha
 • Tofauti ya kimatamshi
 • Taaluma
 • Kiwango cha elimu
 • Jinsia
 • Lugha anazozijua mtu

Mifano ya rejista za lugha ni:

 • lugha ya dini
 • lugha ya biashara
 • lugha ya sheria
 • lugha ya mazungumzo
 • lugha ya sayansi
 • lugha ya Elimu
                                     

1. Marejeo

 • TUKI 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
 • Buliba, Aswani, Kimani Njogu & Alice Mwihaki 2006, "Isimujamii kwa Wanafunzi wa Kiswahili", Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundation
 • Massamba, David 2004, "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam