Back

ⓘ Isimujamii
                                     

ⓘ Isimujamii

Isimujamii ni tawi la isimu ambalo huchunguza uhusiano kati ya lugha na jamii.

Aidha inajihusisha na athira yeyote ya jamii kama vile desturi za watu, matazamio, na muktadha, katika nyanja za lugha namna inavyotumika.

Chini ya taaluma hiyo, kuna matawi mengi yanayoshughulikia uchanganuzi wa vipengele fulani vya uhusiano kati ya lugha na jamii, k.m.

  • vipengele mbalimbali vya mawasiliano kupitia maoni ya msemaji tawi hilo pia huitwa isimu amali
  • matumizi ya lugha baina ya jamii za watu tofauti, kama lugha mawasiliano, pijini na krioli
  • matumizi ya lugha tofauti wakati mmoja, kama katika wingilugha, ubadilishaji msimbo na diglosia
  • uhusiano kati ya lugha na siasa katika upangaji lugha na sera za lugha
  • matumizi ya aina tofauti za lugha na mazingira yake, kama lahaja, rejista na mtindo
  • uhusiano kati ya lugha na utamaduni
                                     

1. Marejeo

  • Massamba, David 2004, "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  • Buliba, Aswani, Kimani Njogu & Alice Mwihaki 2006, "Isimujamii kwa Wanafunzi wa Kiswahili", Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundation
  • TUKI 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

macha kutokka sauti ana kubali maelezo haya kwani ni vitu viwili vinavyoambatana