Back

ⓘ Haki
Haki
                                     

ⓘ Haki

Haki ndiyo utaratibu unaotakiwa katika mafungamano.

Kwa Kigiriki inaitwa dikaiosyne, kutokana na neno asili dike yaani anayeelekeza na kwa hiyo pia mwongozo, utaratibu. Tofauti na nomos, yaani sheria inayoongoza wanyama pia, dike inahitajiwa na binadamu ili kuishi kwa utaratibu. Ni kinyume cha bie, ukatili, nguvu inayoangamiza. Dikaios mwenye kujali haki, ni mtu anayemtendea kila mmoja haki yake. Dikaia zoe ni maisha ya kiutu yanayopingana na hybris kiburi na ushenzi.

Kwa Kilatini kutokana na neno jus, haki, linapatikana neno justus, mwenye kujali haki, na hatimaye justitia, iliyo adili la msingi la utu linalotufanya tumpatie mwingine anachostahili.

Maana ya haki inatofautiana Kwa kila utamaduni. Katika maana ya kwanza kabisa ambayo ilitafsiriwa na mwanafalsafa wa Ugiriki, Plato kwenye kazi yake Jamhuri. Kutokana na historia dhana mbalimbali zimegunduliwa.