Back

ⓘ Jamii:Majina ya ndege kwa Kiswahili
                                               

Barawai

                                               

Bata

Mabata ni ndege wa maji wa familia ya Anatidae wenye madomo mafupi na mapana na miguu yenye ngozi kati ya vidole. Manyoya yao huwa na uwezo bora wa kufukuza maji kwa msaada wa mafuta maalumu. Mabata ndiyo moja ya familia za ndege ambazo spishi zao zina uume, kwa sababu mabata wanapandana majini tu. Mabata huchanganywa pengine na aina kadhaa za ndege wa maji wasiohusiana wenye maumbo yanayofanana, kama wazamaji, vibisi, kukuziwa na shaunge.

                                               

Gawa

                                               

Heroe

Heroe ni ndege wa jenasi Phoenicopterus, jenasi pekee ya familia ya Phoenicopteridae. Ndege hawa hukaa kwa maji ya chumvi kwa makundi makubwa. Wana miguu mirefu na shingo ndefu na nyembamba. Wakiruka angani hunyosha shingo. Urefu wao ni kati ya futi 3 na 5. Hula vijimea na nduvi ndogo ambazo huzikamata na domo lao zungu linalotumika kama chujio. Tago lao ni kifungu cha matope kwa tundu fupi ambalo ndani lake yai moja linatagwa.

                                               

Kwao

Kasuku ni ndege wa familia Psittacidae. Spishi za jenasi nyingine zinaitwa kwao au cherero. Kasuku wengine ni wakubwa, wengine wadogo. Wengi wana rangi kali. Wana mkia mrefu na miguu yao ina vidole viwili vikabilivyo mbele na viwili vikabilivyo nyuma. Domo lao lina nguvu sana na mataya yamepindika kwa pande za kuelekea kama koleo. Kasuku wanatokea kanda zote za tropiki za dunia. Hula mbegu, kokwa, tunda na macho ya maua, pengine wadudu na wanyama wadogo pia. Spishi za" lories” na" lorikeets” hula mbochi na matunda mororo. Kasuku takriban wote hutaga mayai yao tunduni kwa mti.

                                               

Kasuku Mdogo