Back

ⓘ Lord Tariq na Peter Gunz
Lord Tariq na Peter Gunz
                                     

ⓘ Lord Tariq na Peter Gunz

Lord Tariq na Peter Gunz lilikuwa kundi la marapa wawili kutoka nchini Marekani, ambao ni Sean "Lord Tariq" Hamilton na "Peter Gunz" Pankey. Mnamo mwaka wa 1996 washkaji hao walipata kuuza sura katika albamu ya Six ya kundi la Whodini katika wimbo wao wa "Cant Get Enough", na pia wakawasaidia kuandika nyimbo zingine mbili za katika albamu hiyo.

Kunako mwaka wa 1998, walipata kutoa single zao mbili na kubahatika kuingiza moja katika platinamu - "Deja Vu Uptown Baby" kibao ambacho kilishika nafasi ya 9 katika chati za Billboard Hot 100 Bora na kibao kilitoka katika albamu yao moja tu ya Make It Reign.

Albamu hiyo ilishirikisha marapa wakubwa kabisa kama vile Big Pun, Fat Joe, Sticky Fingaz, Kurupt na Camron. Lakini kundi halikutoa kibao kingine tangu hapo na badala yake wakatawanyika baada ya muda mfupi. Mtoto wa Peter Gunz, Cory Gunz naye pia ni rapa.

Lord Tariq ana albamu ya kujitegemea iitwayo The Barcode, ambayo imemshirikisha Peter Gunz na mtoto wake Cory Gunz. Lord Tariq pia alishawahi kushirikiana na Jay-Z na Shaquille ONeal mnamo mwaka wa 1998 katika wimbo uitwao "Analyze This". Remix ya wimbo huo baadaye iliondolewa mistari ya Shaqs na badala yake ikawekwa ya Nas.

                                     
  • Reign ni jina la albamu ya kwanza ya marapa wawili wa Kimarekani, Lord Tariq na Peter Gunz Album ilitolewa mnamo mwaka wa 1998 kupitia studio ya Columbia
  • wakimshirikisha Da Brat na Xscape - 4: 40 My All Stay Awhile Basi Basi Def Mix akimshirikisha Lord Tariq na Peter Gunz - 4: 44 Thank God I Found