Back

ⓘ Usanifu majengo
                                               

Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta

Kigezo:Infobox jumba Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta au Kenyatta International Conference Centre ni jengo la ghorofa 30 iliko mjini Nairobi, Kenya. Iko katikta eneo la kati la biashara la Nairobi. Ni ukumbi kwa mikutano, maonyesho na matukio maalumu ndani ya umbali wa kutembea wa hoteli kadhaa za nyota tano. Imekuwa mwenyeji wa mikutano mingi ya kimataifa na semina. Kuna vyumba kadhaa vya mikutano vilivyo na vifaa vizuri na kile kikubwa kabisa kiko na uwezo wa zaidi ya wajumbe 4.000. Iko na vifaa vya kutafsiria lugha sambamba ambavyo vina uwezo wa kutafsiria lugha saba, kituo c ...

Usanifu majengo
                                     

ⓘ Usanifu majengo

Usanifu majengo ni sanaa na sayansi ya kubuni muundo na sura ya majengo. Sanaa na sayansi hii inajumuisha pia mambo kama mipango miji, usanifu wa eneo la kujenga, na hata ubunifu wa samani zitakazotumika ndani ya jengo.

Watu wanaojihusisha na haya huitwa "wasanifu majengo". Wanahitaji elimu ya ujenzi, hesabu, sanaa, teknolojia, elimu jamii na historia. Msanifu wa kwanza anayejulikana kwa jina ni Imhotep wa Misri ya Kale.

Mbinu za usanifu hutegemea teknolojia inayopatikana, hali ya hewa, hali ya jamii, utaratibu wa siasa yake, hali ya uchumi na mengine mengine.

Nchi na tamaduni mbalimbali ziliunda aina tofauti za usanifu majengo.