Back

ⓘ Liberia
Liberia
                                     

ⓘ Liberia

Liberia yaani Nchi ya watu huru kwa Kilatini ni nchi iliyoko Afrika ya Magharibi. Imepakana na nchi za Ivory Coast, Guinea, na Sierra Leone.

Ni mojawapo ya nchi za Afrika ambazo hazikutawaliwa na Wazungu.

                                     

1. Historia

Liberia ni nchi iliyoundwa na makabila 16 ya asili nchini humo na wahamiaji Weusi toka Marekani na Karibi 5%, mbali na machotara wa aina mbalimbali.

Wamarekani Weusi hao walikuwa watumwa waliopata uhuru ambao kwa kushirikiana na chama cha American Colonization Society waliunda taifa hili na kutangaza uhuru wa nchi hiyo tarehe 26 Julai 1847.

Wamarekani Weusi hao waliichukulia nchi hiyo kama nchi ya ahadi kutokana na asili yao kuwa Afrika, ambako ndiko mababu zao walikotokea kabla ya kupelekwa utumwani Marekani.

Hata hivyo, wahamiaji hao waliendelea kujitambulisha kama Wamarekani na hawakujenga mahusiano ya karibu na wenyeji.

Alama za taifa hili na hata muundo wa serikali vilikuwa vikionyesha mahusiano ya karibu kati ya nchi hizo mbili.

Liberia ilikuwa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe kati ya miaka 1989-1996 na 1999-2003.

Hivi karibuni umefanywa kwa mara ya pili uchaguzi kwa amani na kuweza kumchagua George Weah kushika nafasi ya mwanamke wa kwanza kuwa Rais barani Afrika, Ellen Johnson-Sirleaf.

                                     

2. Watu

Lugha rasmi ni Kiingereza, ambacho kinatumiwa na asilimia 15 za wakazi. Lugha za taifa ni 4: Kiingereza cha Kiliberia, Kikpelle, Kimeriko na Krioli.

Upande wa dini, wakazi kwa asilimia 85.5 ni Wakristo, hasa Waprotestanti, halafu Wakatoliki 5.8%. Waislamu ni 12.2%. Wanaoendelea kufuata dini asilia za Kiafrika ni 0.5% tu.

                                     

3. Tazama pia

 • Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
 • Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
 • Demografia ya Afrika
 • Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
 • Orodha ya lugha za Liberia
 • Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
                                     

4. Viungo vya nje

 • Serikali ya Liberia

Liberia travel guide kutoka Wikisafiri

 • Liberia profile from the BBC News.
 • Liberia entry at The World Factbook
 • "Liberia Maps", Perry-Castañeda Library, University of Texas at Austin.
 • Chief of State and Cabinet Members
 • Liberia katika Open Directory Project
 • Wikimedia Atlas of Liberia
 • Liberia Archived Juni 7, 2008 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs.
                                     
 • Kiingereza ya Liberia ni lugha ya pijini nchini Liberia Ingawa idadi ya watu ambao wamejifunza Kiingereza ya Liberia kama lugha yao ya kwanza haijulikani
 • nchini Liberia unakadiriwa kufuatwa na watu karibia asilimia 12.2 ya idadi ya wakazi wote wa nchini humo. Sehemu kubwa ya Waislamu wa Liberia ni wale
 • Historia ya Liberia inahusu eneo la Afrika Magharibi ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Liberia Liberia ni nchi iliyoundwa na makabila 16 ya asili
 • Play media Kikpelle ni lugha ya Kiniger - Kongo nchini Liberia inayozungumzwa na Wakpelle. Lugha ni tofauti na lugha ya Kikpelle inayozungumzwa nchini Guinea
 • Orodha hii inaorodhesha lugha za Liberia Kibandi Kibassa Kidan Kidewoin Kigbii Kiglaro - Twabo Kiglio - Oubi Kigola Kigrebo - Barclayville Kigrebo - Gboloo Kigrebo - Kaskazini
 • Play media Kiloma ni lugha ya Kiniger - Kongo nchini Liberia inayozungumzwa na Waloma. Isichanganywe na lugha ya Kiloma nchini Cote d Ivoire. Mwaka wa 2006
 • Blyden 1832 - 1912 alikuwa mwalimu, mwandishi, balozi na mwanasiasa nchini Liberia Alizaliwa visiwa vya Karibi. Aliandika kuhusu Muungano wa Afrika.
 • Massaquoi - Fahnbulleh 1912 1978 alikuwa kati ya waanzilishi wa elimu ya juu nchini Liberia Akizaliwa katika ukoo wa wafalme wa kikabila akiwa mtoto wa balozi wa
 • ya Liberia ambaye anacheza kama kipa wa klabu ya LISCR FC katika ligi daraja la kwanza huko Liberia na mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Liberia chini
 • ya Kiniger - Kongo nchini Liberia inayozungumzwa na Wagrebo. Mwaka wa 2002 idadi ya wasemaji wa Kigrebo - Kusini nchini Liberia imehesabiwa kuwa watu 61