Back

ⓘ Mnyama
Mnyama
                                     

ⓘ Mnyama

Wanyama ni viumbehai wasio mmea, kuvu, bakteria, protista au arkea. vile tunaweza kusema wanyama ni viumbehai wanaotegemea chakula kutoka sehemu nyingine: wao hawana uwezo wa kujitengenezea chakula chao wenyewe kupitia usanisinuru lakini kutoka kwa viumbehai vingine ama wanyama wengine au mimea.

Kufuatana na aina ya chakula tunatofautisha hasa wanaokula mimea wanaoitwa walamani au walamea kwa Kiingereza: herbivorous na wanaokula nyama wanaoitwa walanyama au wagwizi ing. carnivorous. Kuna pia walavyote ing. omnivorous wanaoweza kula kila kitu, ama mimea ama wanyama wengine ing. omnivorous.

Wanyama wanahitaji oksijeni kwa kupumua.

Wanyama walio wengi hutembea yaani hubadilisha mahali wanapokaa, kwa hiyo wanahitaji milango ya maarifa.

Sayansi inayochunguza wanyama huitwa zuolojia, ambayo ni tawi la biolojia.

Aina za wanyama ni nyingi sana. Mara nyingi aina zao zinatofautishwa kama ni wanyama wenye seli nyingi metazoa au seli moja protozoa tu.

Kuna wanyama wanaoishi peke yao, katika vikundi na jamii. Mfano wa wanyama wanaoishi peke yao ni kifaru au nyoka. Wanajumuika kwa tendo la kuzaa pekee. Mfano wa wanyama wa jumuiya ni simba wanaokaa na kuwinda pamoja. Ushirikiano unasaidia kupata chakula bora. Mfano wa wanyama katika jamii ni nyuki na wadudu wengine.

Upande wa mwili hata binadamu ni mnyama na kimaumbile anahesabiwa kati ya mamalia.

Binadamu hutofautisha mara nyingi

 • Wanyama wa kufugwa au Mifugo
 • Wanyama wa pori au wanyamapori
 • Wanyama-kipenzi

ingawa lugha hii hutumiwa tu kwa wanyama wakubwa zaidi, kwa kawaida wenye uti wa mgongo kwa Kilatini: Chordata.

                                     
 • Mondo, kizongo au suzi Leptailurus serval ni mnyama mbuai wa nusufamilia Felinae katika familia Felidae. Mondo katika Hifadhi ya Serengeti Taswira Makinda
 • Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru Lama ni mnyama wa kufugwa wa spishi Lama glama katika familia Camelidae, anayeishi Amerika Kusini. Lama ametumiwa kwa
 • 2700 na 4500 kg. Hivyo kiboko inashindana na kifaru juu ya cheo cha kuwa mnyama mzito wa pili kwenye nchi kavu baada ya tembo. Akikimbia hufikia mwendo
 • mwili inayoweza kumtambulisha zaidi mtu au mnyama Kwa kawaida uso hupatikana sehemu ya mbele ya kichwa cha mnyama au wanadamu ingawa si wanyama wote wanaoona
 • Kanu - miyombo Kanu - mondo Kanu madoa - makubwa kusi Wikimedia Commons ina media kuhusu: Kanu mnyama Lioncrusher s Domain Animal Diversity Web: Genus Genetta
 • ya vitu viwili vinavyohusiana. Kimsingi inamaanisha: kile ambacho mtu, mnyama au mmea hupenda kufanya kama kwa silika. Lakini binadamu anaweza kujijengea
 • Mdudu mkubwa dudu pia kwa lugha ya mitaani ni aina ya mnyama mdogo asiye vertebrata, yaani mnyama bila uti wa mgongo. Wanyama waitwao wadudu wana miguu
 • pia wana mwili. Tofauti kubwa iliyopo kati ya viumbehai hao, yaani mtu na mnyama upande wa uwezo wa akili na utendaji pengine inaelezwa na dini, falsafa
 • Ndege ni neno ambalo kwa Kiswahili linaweza kumaanisha: Ndege mnyama ni aina wa wanyama ambao kwa kawaida wanaweza kuruka. Ndege uanahewa au eropleni
 • Shingo ni sehemu ya mwili wa mnyama au binadamu inayounganisha kichwa na kifua.