Back

ⓘ Kamusi elezo
Kamusi elezo
                                     

ⓘ Kamusi elezo

Kamusi elezo ni kitabu kinachokusudiwa kukusanya ujuzi wa binadamu kadiri iwezekanavyo kulingana na wingi wa kurasa zake.

Siku hizi, Wikipedia ni kamusi elezo kubwa zaidi duniani lakini si kitabu cha karatasi, ni mkusanyo wa habari kwa umbo dijitali katika intaneti. Zamani kabla ya kuja kwa Wikipedia Encyclopedia Britannica ilikuwa kati ya kamusi elezo kubwa zaidi iliyokuwa ikitolewa kama vitabu vilivyochapishwa.

                                     

1. Historia

Katika historia yalikuwepo majaribio mbalimbali ya kukusanya ujuzi wote wa dunia. Mfano bora wa kale ni kamusi ya Yongle kutoka China iliyotungwa na wataalamu 2000 katika karne ya 14 na kuandikwa kwa mkono katika vitabu 1100.

Lakini kamusi elezo au ensaiklopedia zimekuwa na athari kubwa sana tangu Johannes Gutenberg na kupatikana kwa uchapaji wa vitabu ulioshusha kabisa bei ya vitabu kwa watu wengi.

Ensaiklopedia ya kwanza ya kisasa iliyokuwa na athira kubwa sana ilikuwa "Encyclopédie ou Dictionnaire raisonné des sciences, des arts et des métiers" iliyokusanywa na Denis Diderot pamoja na Jean Baptiste le Rond d’Alembert pamoja na waandishi zaidi ya 130 katika karne ya 18 huko Ufaransa. Kamusi elezo hii ikawa moja kati ya vyanzo vya harakati ya Zama za Mwangaza.

                                     
 • Wikipedia ni kamusi elezo huru ya lugha nyingi katika mtandao wa wavuti. Inalenga kukusanya elimu nyingi iwezekanavyo na kuisambaza kwa njia ya intaneti
 • au Old Catholic Encyclopedia au Original Catholic Encyclopedia, ni kamusi elezo ya Kiingereza kutoka Marekani ambayo inafafanua vidahizo kuhusu Kanisa
 • Kiingereza - Kiswahili Kamusi elezo ing. encyclopedia inayolenga kukusanya maelezo ya mambo ambayo yanatajwa kwa maneno. Wikipedia ni kamusi elezo ya kwanza kwa
 • Encyclopædia Britannica ni kamusi elezo kubwa na moja kati ya kamusi elezo iliyo - maarufu zaidi. Inaandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Kamusi elezo hii huchapishwa
 • Vikipedia, Daneshname - ye Azad maana yake Wikipedia, Kamusi Elezo Huru ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kiajemi. Toleo la Wikipedia
 • Kiesperanto: Vikipedio en Esperanto, au esperantlingva Vikipedio ni toleo la kamusi elezo huru ya Wikipedia kwa lugha ya Kiesperanto. Wikipedia hii, ilianzishwa
 • Wikipedia ya Kihaiti ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kihaiti. Ni moja kati ya Wikipedia chache sana za lugha ya aina ya Krioli. Wikipedia
 • Wikipedia ya Kihungaria Kihungaria: Magyar Wikipédia ni toleo la kamusi elezo huru ya Wikipedia kwa lugha ya Kihungaria Magyar. Wikipedia hii, ilianzishwa
 • Wikipedia ya Kipoland Kipoland: Wikipedia polskojęzyczna ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kipoland. Wikipedia ya Kipoland, ni toleo la
 • Wikipedia ya Kidenmark ni toleo la kamusi elezo huru ya Wikipedia kwa lugha ya Kidenmark. Wikipedia hii, iliazishwa mnamo tar. 1 Februari katika mwaka
 • Википедија на српском језику Vikipedija na srpskom jeziku ni toleo la kamusi elezo la Wikipedia kwa lugha ya Kiserbia. Ilianzishwa mnamo tar. 16 Februari