Back

ⓘ Jamii:Saikolojia
                                               

Bipolar Disorder

Tatizo la kubadilika kwa hisia, kama kufurahi na kuhuzunika kupita kiasi, ni tatizo la kiakili ambalo husababisha misimu ya huzuni na misimu ya furaha zisizo za kawaida.

                                               

Tatizo la kiakili linalotokana na kiwewe

Tatizo la kiakili linalotokana na kiwewe ni tatizo la akili linaloweza kukua baada ya mtu kupatwa na tukio la kiwewe, kama vile unyanyasaji wa kijinsia, vita, ajali barabarani, au tishio jingine kwa maisha yake. Dalili zinaweza kuwa: mawazo ya wasiwasi, mhemuko, au ndoto zinazohusiana na matukio hayo, huzuni, jaribio la kuepa ishara zinazohusiana na kiwewe, mabadiliko ya jinsi mtu hufikiria na huhisi, na kuongezeka kwa kupamba na-au-kutoroka majibu. Dalili hizo hukaa kwa zaidi ya mwezi baada ya tukio. Watoto wadogo wana uwezekano mdogo wa kuonyesha huzuni, lakini badala yake wanaweza kuony ...

                                               

Akili

Akili ni kipawa kinachowezesha kufikiri, kuelewa, kuwasiliana, kujifunza, kupanga na kutatua matatizo. Ni ufahamu uliomo katika ubongo wa binadamu, unaoweza hata kutofautisha jambo kwa wema na ubaya wake na hatimaye kumuongoza katika kufanya maamuzi. Ingawa akili kwa ujumla hutumiwa kuhusiana na binadamu, baadhi ya wanyama kama sokwe, bonobo, mbwa n.k. na hata mimea huwa na dalili fulani za akili. Dhana kuhusu asili ya akili zinatofautiana. Akili bandia ni akili ya mashine inayopatikana kwa kutumia programu za kompyuta.

                                               

Akili ya binadamu

Akili ya binadamu ni kipawa kinachowezesha kufikiri, kuelewa, kuwasiliana, kujifunza, kupanga na kutatua matatizo. Ni ufahamu uliomo katika ubongo hasa wa binadamu, unaomwezesha hata kutofautisha jambo kwa wema na ubaya wake upande wa maadili na hatimaye kumuongoza katika kufanya maamuzi kwa kutumia hiari yake. Dhana kuhusu asili ya akili ya binadamu zinatofautiana, vilevile na maelezo mengine mengi, kulingana na dini, falsafa na sayansi husika. Jambo mojawapo la msingi ni kuelewa kama akili hiyo ya pekee inategemea tu ubongo uliokua sana katika binadamu kuliko katika spishi nyingine au ku ...

                                               

Anxiety Disorder

Matatizo ya kiakili yanayosababisha wasiwasi kila mara ni kundi la matatizo yenye sifa ya hisia muhimu ya wasiwasi na hofu. Wasiwasi ni mahangaiko kuhusu matukio ya siku zijazo, na hofu ni athari kwa matukio ya sasa. Hisia hizo zinaweza kusababisha dalili mwilini, kama vile mapigo ya haraka ya moyo, tetemeko, utovu wa usingizi, uchovu mwilini, hasira n.k. Kuna aina ya matatizo ya kiakili yanayosababisha wasiwasi kila mara kama vile tatizo la kiakili linalosababisha wasiwasi kila mara, hofu isiyo ya kawaida, tatizo la kiakili linalosababisha wasiwasi kila mara la utengano, hofu isiyo ya kaw ...

                                               

Glosofobia

Glosofobia ni hofu au dukuduku la kuzungumza hadharani. Neno glosofobia linatokana na maneno ya Kigiriki γλῶσσα glōssa, likimaanisha ulimi na φόβος phobos, hofu. Kitendo cha kuongea hadharani, iwe ni mbele ya kundi la watu wasiojulikana au mbele ya kundi la marafiki, ndio sababu inayompa wasiwasi mzungumzaji. Mzungumzaji anaweza kuongea bila matatizo mbele ya kundi la watu asiowajua, lakini akashindwa kuongea mbele ya marafiki au familia na kinyume chake. Baadhi huongea bila matatizo mbele ya kundi dogo na wengine hufanya hivyo mbele ya kundi kubwa.

                                               

Aina za ufahamu

Aina za ufahamu zilizo kuu ni tatu: ufahamu wa kusoma, ufahamu wa kusikiliza na ufahamu wa kuona. Ufahamu wa kusoma: hapa mtu hupata ufahamu wa jambo fulani kwa kusoma magazeti, barua, n.k. Ufahamu wa kusikiliza: mtu hupata ufahamu kwa kusikiliza redio, hadithi, n.k. Ufahamu wa kuona: mtu hupata ufahamu wa jambo kwa kuona mwenyewe tukio.

                                               

Hisia

Hisia ni mihemko ambayo binadamu na wanyama hujisikia moyoni na huathiri mwili pia kupitia ubongo. Kadiri ya saikolojia zinaweza kuwa za pendo, hamu, furaha, au kinyume chake za chuki, woga, hasira, huzuni na nyingine nyingi tu. Zinaitwa pia maono.

Msisimko
                                               

Msisimko

Msisimko ni hali ya mtu kuhisi mshtuko wa ghafla moyoni au mwilini baada ya kuona au kuingiwa na hamu kubwa ya kupata au kufanya jambo fulani. Unaweza kusababishwa na hofu ya ghafla lakini pia na furaha au mshtuko mwingine.

Pendo
                                               

Pendo

Pendo linaweza kutafsiriwa kwa maana mbalimbali, kama vile upendo, mapendo, mapenzi n.k. Hapa linatumika kwa maana ya ono mojawapo la msingi kwa binadamu na wanyama ambalo wanavutiwa na jambo fulani, hata likafuatwa na hamu na hatimaye furaha ikiwa jambo limepatikana kweli. Kati ya haja za msingi za nafsi, mojawapo ni kupenda na kupendwa.

Saikoanalisia
                                               

Saikoanalisia

Saikoanalisia au mkabala wa unafsiya ni tawi la saikolojia, ambalo muasisi wake mkuu ni Mwaustria Sigmund Freud. Mbinu zake zinachunguza kwanza sehemu ya nafsi isiyoelea kwa kawaida, lakini ni chanzo cha mengi katika mwenendo wa binadamu ili kumtibu mwenye matatizo ya nafsi. Tawi hilo liliendelezwa kwa namna mbalimbali na Alfred Adler, Carl Gustav Jung, Erich Fromm, Karen Horney, Harry Stack Sullivan n.k. Freud retained the term psychoanalysis for his own school of thought.

                                               

Tabia

Tabia inaweza kuwa na maana ya vitu viwili vinavyohusiana. Kimsingi inamaanisha: kile ambacho mtu, mnyama au mmea hupenda kufanya kama kwa silika. Lakini binadamu anaweza kujijengea tabia kwa utashi wake.

                                               

Ugonjwa wa mawasiliano

Ugonjwa wa mawasiliano ni ugonjwa unaoathiri uwezo wa mtu wa kuelewa, kuchunguza, au kutumia lugha na kushindwa kutoa hoja ili kushiriki kwa ufanisi katika mazungumzo na wengine. Husababishwa na hitilafu fulanifulani kwenye ubongo. Ugonjwa huu unamfanya mtu ashindwe kuongea mbele ya umati wa watu.