Back

ⓘ Jamii:Historia ya Kanisa
                                               

Abersi

Abersi alikuwa Mkristo wa karne ya 2 aliyepata kuwa askofu wa Hieropoli, Frigia, katika Uturuki ya leo. Alifariki gerezani alipofungwa katika dhuluma ya kaisari Marko Aurelio. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Oktoba.

                                               

Church Missionary Society (CMS)

Church Missionary Society ni shirika la umisionari la Kanisa Anglikana lililoanzishwa mwaka 1799 huko London.

                                               

Cluny

Abasia ya Cluny, ilikuwa monasteri ya Wabenedikto, maarufu kwa kuongoza urekebisho wa utawa na wa Kanisa lote kuanzia karne ya 10. Ilijengwa kwa mtindo wa Kiroma katika eneo la Burgundy, leo mkoa wa Saône-et-Loire, Ufaransa. Mwanzilishi wake, William I wa Aquitania, mwaka 910 alimteua Berno wa Cluny awe abati wa kwanza, chini ya Papa Sergius III tu. Hivyo alionyesha njia ya kukwepa watawala wasiendelee kuingilia vyeo vya Kanisa kwa malengo yao ya kisiasa na ya kiuchumi badala ya yale yaliyokusudiwa ya kidini. Monasteri nyingine nyingi zilifuata njia hiyo na kivyo kuinua hali ya kiroho ya u ...

                                               

Dola la Papa

Dola la Papa lilikuwa nchi huru chini ya himaya ya Papa kuanzia miaka ya 700 hadi 1870. Chanzo chake ni uvamizi wa makabila ya Wagermanik uliobomoa Dola la Roma upande wa magharibi wa Bahari ya Kati. Wenyeji, wengi wao wakiwa Wakristo Wakatoliki, walimkimbilia Papa kama kiongozi wao atakayeweza kuwasaidia katika matatizo. Baadaye Wafaranki walikubali kumuachia Papa mamlaka ya kisiasa juu ya maeneo mbalimbali nje ya Roma. Polepole maeneo yaliongezwa hata kufikia mikoa 3 na nusu ya Italia ya leo: Lazio, Umbria, Marche na sehemu ya Emilia-Romagna. Dola lilikoma tarehe 20 Septemba 1870, jeshi ...

                                               

Farakano la Donato

Farakano la Donato lilitokea katika Kanisa la mkoa wa Afrika wa Dola la Roma hasa kati ya Waberberi wa Algeria na Tunisia za leo. Farakano hilo lilikuwa na nguvu hasa katika karne ya 4 na ya 5. Mizizi yake ni dhuluma za dola hilo dhidi ya Wakristo waliostawi mapema katika eneo hilo, hasa zile za kikatili zaidi zilizoagizwa na Kaisari Diokletiani. Farakano lilipewa jina la askofu Donato Mkuu aliyeshika msimamo mkali kuhusu kuwasamehe walioasi ili kuokoa uhai wao.

                                               

Farakano la Kanisa la Magharibi

Farakano la Kanisa la Magharibi lilitokea ndani ya Kanisa Katoliki katika miaka 1378-1418. Makardinali wenye jukumu la kumchagua Papa walichagua wawili, mmoja baada ya mwingine, na hivyo kusababisha isieleweke yupi ana haki ya kuongoza. Siasa ilijiingiza na kudumisha fujo kubwa, ingawa si kuhusu mafundisho ya imani, mpaka Mtaguso wa Konstanz 1414–1418 ulipotoa suluhisho. Hata hivyo ilibaki athari mbaya juu ya mamlaka ya Mapapa waliofuata.

Acta Sanctorum
                                               

Acta Sanctorum

Acta Sanctorum ni kamusi elezo ya Watakatifu wa Kanisa Katoliki inayofuata tarehe ya sikukuu yao. Ni vitabu vikubwa 68 vilivyoandikwa huko Ubelgiji kwa kuzingatia ukweli wa historia kati ya karne ya 16 na karne ya 20 na kuchapwa kuanzia mwaka 1643 hadi 1940.

Huneriki
                                               

Huneriki

Huneriki alikuwa mtoto wa kwanza wa Genseriki, mfalme wa Wavandali na Waalani kwa karibu miaka 50 ambaye aliinua makabila haya madogo kuwa ufalme imara katika Afrika Kaskazini uliotikisa Dola la Roma Magharibi katika karne ya 5 hata kuteka jiji hilo kwa muda mnamo Juni 455. Huneriki hakuendeleza mipango mikubwa ya baba yake lakini, baada ya muda, alizidi kudhulumu kikatili Wakatoliki wa Afrika Kaskazini hivi kwamba Waarabu Waislamu walipoiteka Ukristo ulikoma haraka.