Back

ⓘ Kilimo
Kilimo
                                     

ⓘ Kilimo

Kilimo ni uzalishaji wa mazao kwenye mashamba.

Kilimo kina maana pana inayojumuisha mifumo ya uzalishaji mimea, ufugaji wa wanyama, na uvuvi wa samaki. Mara nyingi kilimo cha mimea kinaenda sambamba na ufugaji wa wanyama.

Watu hupanda mimea na kuitunza hadi mavuno hasa kwa uzalishaji wa chakula cha binadamu na lishe ya wanyama, lakini pia kwa shabaha ya kupata malighafi mbalimbali zinazotumiwa kwa kutengeneza nguo za watu.

Siku hizi kilimo kinalenga pia nishati ya mimea.

Mtu anayejihusisha na kilimo huitwa mkulima.

                                     

1. Katika uchumi

Kilimo ni mojawapo ya shughuli za mwanadamu ambayo humsaidia kupata mazao kwa ajili ya chakula na mazao mengine kwa ajili ya biashara ambayo inaweza kumuingizia kipato kwa ajili ya maisha yake, pia kipato hicho husaidia katika kukuza uchumi wa nchi yake ili hatimaye itakuwa imejikomboa kiuchumi.

Sekta hiyo ndiyo kiinua uchumi kikubwa kwa mataifa mengi.

Kwa jumla serikali zinatakiwa zitoe kipaumbele kwa sekta ya kilimo ili kuepukana na janga la njaa: mojawapo ya mahitaji makuu ya mwanadamu ni chakula.

Serikali zinatakiwa zizidi kuongeza zana za kilimo ili watu waweze kupata kwa wingi mazao ya biashara na mazao ya chakula.

Pia serikali itoe elimu juu ya kilimo bora kama kitega uchumi ambacho huwasaidia watu kujipatia mazao na kipato cha kwao ili kuendesha maisha yao binafsi.

Wakulima wanatakiwa kupewa mikopo ya pesa, na pia kujishughulisha na kilimo cha umwagiliaji, si tu kutegemea mvua.

                                     

2. Historia

Watu walianza kulima takriban miaka 10.000 iliyopita na kabla ya hapo watu waliwinda tu na kukusanya matunda. Kuna vikundi vidogo ambavyo vinaendelea na maisha haya hadi leo, lakini siku hizi zaidi ya asilimia 99 za binadamu hupata chakula kutokana na kilimo.

Inaaminiwa ya kwamba kilimo kilianza katika sehemu tatu za dunia ambako watu walitambua mimea yenye lishe kubwa na kupanda mbegu zake. Maeneo haya ambako kilimo kilianza ni China, Amerika ya Kaskazini na Mashariki ya Kati.

Wataalamu hawakubaliani kama kilimo cha Afrika kina asili yake huko Mashariki ya Kati au kama ilianzishwa barani peke yake.

                                               

Kachuo

Kachuo ni kitongoji kilichopo katika kijiji cha Nyamatongo kata ya Kamanga wilayani Sengerema mkoani Mwanza. Wakazi wake ni mchanganyiko wa makabila kama vile Wasukuma, Wasumbwa,Wazinza na makabila mengineyo yanayo lizunguka Ziwa NyanzaViktoria. Katika kitongoji hiki wakazi wake wanajishughulisha na shughuli za Uvuvi, Kilimo, Ufugaji na Biashara.

Nyumba ya Mungu
                                               

Nyumba ya Mungu

Nyumba ya Mungu ni bwawa linalozalisha umeme ambalo lipo katika wilaya ya Mwanga, mkoa wa Kilimanjaro. Nyumba ya Mungu ipo kwenye bonde la mto Pangani; maji yake yanatoka katika Kikuletwa na Ruvu. Lambo llitengenezwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, kuzalisha umeme na viwanda vya samaki vilivyo kuwa karibu na pale.

Bustani
                                               

Bustani

Bustani ni eneo lililotengenezwa nje ya nyumba au jengo lingine kwa kupanda miti, majani na maua ili kulipendezesha na kulifurahia wakati wa kupumzika. Pengine bustani linapandwa pia mimea kwa ajili ya mboga au matunda. Tena kuna bustani ya wanyama ambao wanatunzwa ili watu waweze kuwaona kwa urahisi. Bustani zilianzishwa zamani za kale.