Back

ⓘ Uchumi
                                               

Orodha ya benki nchini Kenya

Hii ni orodha ya mashuhuri benki za biashara nchini Kenya Banki zilizo na leseni za biashara Equity Bank Barclays Bank Kenya Diamond Trust Bank Giro Commercial Bank Family Bank Kenya Commercial Bank Citibank ABC Bank Kenya Habib Bank Bank of India Guardian Bank Prime Bank Kenya Bank of Africa Paramount Universal Bank United Bank for Africa Housing Finance Company of Kenya First Community Bank Habib Bank AG Zurich Consolidated Bank of Kenya CfC Stanbic Bank Trans National Bank Kenya Credit Bank Bank of Baroda Equatorial Commercial Bank Development Bank of Kenya Jamii Bora Bank National Bank ...

                                               

Ekinokokasi

Ekinokokasi ni maradhi yenye kusababishwa na kimelea parasiti. Hiadatidi ni sisti za kiluwiluwi cha tegu" Taaenia echinococcus” masalia ya tishu za kiinitete Watu wanaumia aina mbili kuu ekinokokasi ya sisti na ekinokokasi alveolasi. Zaidi kuna aina mbili zingine zisizojulikana kama hizo ekinokokasi yenye sisti nyingi na ekinokokasi yenye sisti moja. Maradhi haya mara nyingi yanaanzia bila dalili huenda yanamudu muda wa mwaka katika hali hiyo. Dalili zilizopo zinategemea mahali panapo kuwa na sisti pamoja na ukubwa wao. Maradhi alveolasi kwa kawaida yanaumiza ini kwanza lakini yanaweza kus ...

                                               

Aramex

Aramex au kwa kiarabu ni kampuni ya kimataifa ya maswala ya usafirishaji na uwekaji katika ghala wa bidhaa, usafirishaji kwa njia ya ndege na usafirishaji wa mizigo ndani ya nchi mbalimbali. Kampuni hii ilianzishwa mwaka 1982 na makao yake makuu yako Amman, Jordan. Aramex pia inatoa huduma za reja kama vile usambazaji wa barua.

                                               

Liza Essers

Baada ya kupata shahada ya biashara na uchumi, Essers alifanya kazi kama mshauri mipango na mikakati katika kampuni ya global professional services company ambapo aliweza kuinua sekta ya biashara na mapato nchini Afrika kusini. Mapema mwaka 2008 mawazo ya kuuuzwa kwa kampuni ya Goodman Gallery, Essers alikuwa pia ni mshauri katika masuala ya sanaa na filamu, pia alikuwa ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya filamu ya South African film. Filamu ya kwanza kushinda tuzo ilishinda mwAka 2006 ilokuwa ikizungumiza maisha ya kisanii ya William Kentridge na Marlene Dumas.

                                               

Isabelle Axelsson

Isabelle Axelsson ni mwanaharakati wa hali ya hewa kutoka Stockholm, Uswidi. Axelsson amekuwa mwanaharakati na mratibu wa Fridays for Future Sweden tangu Desemba 2018. Mwisho wa Januari 2020, alihudhuria Mkutano wa Uchumi Ulimwenguni World Economic Forum huko Davos pamoja na wanaharakati wengine wa hali ya hewa, ambao ni Greta Thunberg, Luisa Neubauer, Loukina Tille na Vanessa Nakate. Alikuwa mchangiaji wa kitabu kilichoitwa Gemeinsam für die Zukunft - Fridays For Future und Scientists For Future: Vom Stockholmer Schulstreik zur weltweiten Klimabewegung. Katika kitabu hicho, alichangia mae ...

Uchumi
                                     

ⓘ Uchumi

Uchumi ni jumla ya shughuli zote za binadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji yao. Ni hasa uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa bidhaa pamoja na kutolewa kwa huduma kwa njia mbalimbali.

Uchumi mara nyingi hutazamwa kwenye ngazi za kijiji, eneo, taifa au dunia.

Sayansi ya Uchumi kwa Kiingereza economics ni tawi la elimu inayochunguza masharti ya uchumi kufaulu au kushindwa.

                                     

1. Sekta za uchumi

Uchumi wa jadi katika nchi nyingi ulikuwa hasa kilimo cha kujikimu pamoja na biashara ya kubadilishana bidhaa kadhaa zenye thamani kubwa. Kwa mfano, tangu kale migodi ya Zimbabwe ilichimba dhahabu iliyopelekwa baadaye hadi Asia na kando ya Mediteranea.

Katika uchumi wa kisasa mara nyingi sekta tatu hutofautishwa:

  • Sekta ya msingi: kutoa na kuzaa malighafi pamoja na mazao katika mazingira asilia. Mifano ni kilimo, uchimbaji wa madini, uvuvi au kuvuna ubao.
  • Sekta ya pili: shughuli za kubadilisha malighafi hizi kuwa bidhaa. Madini ya chuma hubadilishwa kuwa feleji; feleji hutumiwa na viwanda kutengeneza vyuma vya ujenzi, magari, vifaa vya nyumbani. Viwanda vya nguo hutumia pamba kutoka mashambani na kuibadilisha kuwa uzi halafu kitambaa na nguo.
  • Sekta ya tatu: biashara au usambazaji wa bidhaa hizi kwa wateja pamoja na kuwatolea huduma. Mifano ni maduka yanayouza bidhaa zilizotengenezwa viwandani. Mingine ni huduma kama benki, hoteli, sinema na usafiri.
  • Wataalamu wengine hutaja sekta ya nne: shughuli za kusambaza habari na pia utafiti wa teknolojia mpya unaoendelea kuwa muhimu katika nchi zinazoendelea. Wengine huingiza pia elimu kazi za shule na vyuo katika sekta hii ya uchumi.
                                     

2. Viungo vya Nje

  • Majarida kuhusu uchumi mtandaoni Archived Julai 10, 2013 at the Wayback Machine.
  • Vitabu kuhusu uchumi toka Wikibooks
  • Mafunzo ya uchumi huria na bure kutoka MIT