Back

ⓘ Jamii:Ugiriki ya Kale
                                               

Pergamon

Pergamon ilikuwa mji wa Ugiriki ya Kale kwenye pwani ya magharibi ya Asia Ndogo katika Uturuki ya leo. Leo hii huko mji wa Bergama takriban kilomita 80 kaskazini ya Izmir. Wakati wa karne ya 3 na ya 2 kabla ya Kristo Pergamon ilikuwa mji mkuu wa milki iliyotawala sehemu kubwa za Asia Ndogo. Watawala wa nasaba ya Attalos walipamba mji kwa mahekalu na taasisi zilizoufanya kitovu cha utamaduni wa Kigiriki. Pergamon ilikuwa na maktaba kubwa ya pili katika dunia ya Mediteranea baada ya maktaba ya Aleksandria: inasemekana maktaba hii ilikuwa na vitabu vya miswada 200.000. Mfano mashuhuri wa utam ...

                                               

Plataia

Plataia au Plataea ulikuwa mji wa Ugiriki ya Kale, ulioko Ugiriki kusini, takriban kilomita 60 upande wa magharibi mwa Athens, kusini mwa Thebes. Plataia ilikuwa mji rafiki wa Athens na katika vita dhidi ya Waajemi jeshi la Plataia lilipigana pamoja na Waathens kama kwenye mapigano ya Marathon mnamo mwaka 490 KK. Mapigano ya Plataia yaliyotokea mnamo 479 KK karibu na mji yaliyeta ushindi wa mwisho wa Wagiriki dhidi ya Uajemi. Plataia iliharibiwa katika Vita ya Peloponnesi na Thebes na Sparta mnamo 427 KK ikajengwa upya mnamo 386 KK na kubomolewa tena 373 KK. Mji wa kisasa wa Plataies umeje ...

                                               

Sanamu ya Kolossos kisiwani Rhodos

Sanamu ya Kolossos kwenye kisiwa cha Rhodos ilikuwa kati ya maajabu saba ya dunia ya kale. Kolossos ilikuwa mnara wa taa mwenye umbo la sanamu ya mtu aliyesimama kwenye mlango wa bandari na kushika moto kama mwenge. Kazi ya sanamu ilikuwa kuelekeza meli bandarini wakati wa usiku. Sanamu ilimwonyesha mungu wa jua Helios. Ilijengwa kwa muda wa miaka 12 ikakamilishwa mnamo 300 KK na kuwa na kimo cha zaidi ya mita 30. Ilikuwa sanamu kubwa kabisa ya dunia ya kale. Kumbukumbu zimehifadhiwa kuwa matumizi ya vifaa yalikuwa pamoja na tani 13 za bronzi na tani 8 za chuma zilizofunika nguzo za matofa ...