Back

ⓘ Usafiri
                                               

Magic Bus

Magic Bus Ni brandi ya basi ambayo Shirika la Stagecoach hutumia kwa mabasi yake nchini Ufalme wa Muungano, ambayo kwa kawaida huhudumu chini ya ushindani mkali kutoka kwa wahudumu wengine. Jina hili lilitumika kwa mara ya kwanza mjini Glasgow, Scotland miaka ya 1980 wakati Routemaster zilizokuwa za Usafiri wa London zilikuwa zikitumika lakini huduma hiyo hatimaye iliuzwa kwa Kelvin Central Buses mnamo 1994. Leo hii mabasi mengi ya Magic Bus ni mabasi ya zamani ya deka mbili. Mabasi mengine ya aina ya tri-axle ya deka mbili yaliyonunuliwa kutoka maeneo ya Uhudumu wa Stagecoach ya Kenya na ...

                                               

Kampuni ya Green Bus Lines

Green Bus Lines ilikuwa kampuni ya mabasi katika jiji la New York,Marekani.Ilisimamiwa na hivi majuzi kabisa na Bw.Jerome Cooper na ikaendesha biashara zake katika mitaa ya Queens na pia kuwa na mabasi ya kuenda hadi Manhattan bila kusimama.Ilifanya hivi hadi 9 Januari 2006,ndipo Kampuni ya MTA ilichukua njia maalum za Green Bus Lines. Kampuni hii ilianzishwa 3 Aprili 1925 ili kuwasilisha huduma ya mabasi katika mitaa. Mabasi yake yalikuwa yakipitia njia nyingi maalum za Manhattan katika mwaka 1933,lakini mamlaka za kutumia njia hizi zikapewa Shirika la Comprehensive Omnibus katika mwaka w ...

Usafiri
                                     

ⓘ Usafiri

Usafiri ni uhamisho wa watu au vitu na bidhaa kutoka mahali pamoja kwenda mahali pengine.

Usafiri unakuja pamoja na muundombinu kama njia za usafiri, vyombo vya usafiri na wahusika wake kama makampuni, shirika na abiria.

                                     

1. Njia za usafiri

Njia za usafiri hutofautishwa kufuatana na aina yake kama ni:

  • usafiri wa hewani kwa kutumia vyomboanga na viwanja vya ndege
  • usafiri wa nchi kavu kwa kutumia barabara au reli
  • usafiri wa majini kwa kutumia bahari, maziwa, mito na mifereji
  • usafiri wa mabomba ambayo husafirisha maji, gesi na mafuta.
                                     

2. Vyombo vya usafiri

Vyombo vya usafiri hulingana na njia zinazotumika.

Usafiri wa nchi kavu hutumia motokaa, treni, baisikeli au pikipiki.

Usafiri wa majini hutumia meli, boti, jahazi na mengine.

Usafiri wa hewani hutumia ndege, helikopta au ndegeputo.

                                     

3. Faida ya usafiri

  • Husaidia kufikisha haraka habari zilizo kwenye majarida n.k.
  • Pia husaidia katika maendeleo ya nchi kimapato
  • Husaidia biashara za masafa marefu kuendelea.
  • Husaidia katika kufikisha haraka vyakula au matunda yanayooza mapema.
  • Huwezesha mahusiano kati ya nchi na nchi.