Back

ⓘ Kupatwa kwa Jua
Kupatwa kwa Jua
                                     

ⓘ Kupatwa kwa Jua

Kupatwa kwa Jua ni hali ya Jua kutoonekana angani wakati wa mchana kwa muda fulani hata pasipo mawingu. Kunatokea wakati mwezi unapita kati ya Jua na dunia na kufunika Jua. Tokeo lake ni kupungua kwa nuru ya Jua hadi kutoonekana kwa muda wa kufika kwa giza wakati wa mchana. Muda wa kufunikwa kabisa ni dakika chache tu.

Kuna utofauti kati ya" Kupatwa kiasi” ing. partial eclipse na" Kupatwa kikamilifu” ing. total eclipse. Kupatwa kwa Jua hutokea kila mwaka, angalau mara mbili hadi mara tano. Lakini kupatwa kabisa kwa Jua hautokei zaidi kuliko mara mbili kwa mwaka. Huonekana katika sehemu za Dunia pekee, si kote.

                                     

1. Misingi ya kupatwa kwa Jua

Kupatwa kwa Jua kunatokea wakati Mwezi unapita kati ya Jua na Dunia. Hapo Jua, Mwezi na Dunia zinakaa kwenye mstari mmoja mnyoofu. Katika hali hiyo Mwezi hurusha kivuli chake kwenye uso wa Dunia. Kivuli hiki hakifuniki Dunia yote. Ni kama kinu kwenye uso wa Dunia. Nje ya kivuli hiki Jua linaonekana kwa sehemu au bila upungufu.

Hali ya kupatwa kabisa kwa Jua inatazamwa kila mara kwenye mstari mwembamba kwenye uso wa Dunia, tena giza kabisa kwa muda mfupi. Mstari huu ni njia ya kitovu cha kivuli chake kwenye uso wa Dunia. Nje ya njia hii kupatwa kwa Jua kunaonekana kwa sehemu tu. Mbali na njia ya kivuli hiki Jua linaonekana kama kawaida.

                                     

2. Aina za kupatwa kwa Jua

Kuna aina mbalimbali za kupatwa kwa Jua.

 • kupatwa kwa Jua kiasi: Katika eneo kubwa la kivuli cha kando watu huona upungufu wa mwanga; kiasi chake hutegemea umbali wa kitovu cha kivuli. Wakitazama Jua kwa kichujio, kwa mfano kioo kilichopakwa dohani kutoka moshi wa mshumaa, huwa wanaona sehemu ya duara ya Jua imefunikwa.
 • kupatwa kipete: mwezi huonekana mdogo kiasi kuliko Jua. Kwa hiyo duara la mwangaza wa Jua ni kubwa kuliko duara la Mwezi na mwanga wa Jua huonekana kama pete.
 • kupatwa kikamilifu: Jua hupotea kabisa kwa dakika chache. Hali hii yaonekana kwenye ukanda mwembamba duniani pale ambako kitovu cha kivuli kinapita.
                                     

3. Mpito wa sayari

angalia Mpito wa Zuhura Wakati sayari inapita kati ya Jua na Dunia inafunika sehemu ya Jua. Tofauti haionekani kwa macho lakini inaweza kutazamwa kwa kutumia darubini. Kuna sayari mbili zinazoweza kupita mbele ya Jua kwa macho ya mtazamaji duniani, ni Utaridi Mercury na Zuhura Venus.

                                     

4. Viungo vya nje

 • Prof. Druckmüllers eclipse photography site
 • Solar eclipse time sequence
 • Animated maps of past and future solar eclipses Archived Mei 30, 2009 at the Wayback Machine.
 • NASAs Eclipse Home Page Archived 2012-12-05 at Archive.today, Fred Espenak
 • Eclipse Image Gallery at The World at Night Archived Oktoba 15, 2016 at the Wayback Machine.
 • Detailed eclipse explanations and predictions, Hermit Eclipse
 • World Atlas of Solar Eclipse Paths Archived 2012-07-14 at Archive.today, Fred Espenak
 • Animated explanation of the mechanics of a solar eclipse Archived Agosti 21, 2011 at the Wayback Machine., University of Glamorgan
 • Solar eclipse of January 15, 2010, Fred Espenak, NASA
 • Looking Back at an Eclipsed Earth 1999 August 11 from Mir EO-27 - Astronomy Picture of the Day 10 June 2007
 • Search among the 11.898 solar eclipses over five millennium and display interactive maps


                                     

4.1. Viungo vya nje Usalama wa macho wakati wa kuangalia

 • How to Watch a Partial Solar Eclipse Safely Archived Machi 16, 2006 at the Wayback Machine., A. M. MacRobert Sky & Telescope magazine
 • Eye Safety During Solar Eclipses Archived 2012-07-16 at Archive.today, F. Espenak NASA Goddard Space Flight Center
 • UK hospitals assess eye damage after solar eclipse, British Medical Journal, August 21, 1999, p. 319–469
                                     
 • Hali hii ni kinyume cha kupatwa kwa Jua ambako Jua Mwezi na Dunia vinakuwa pia katika mstari lakini hapo Mwezi uko kati ya Jua na Dunia na hivyo ni Mwezi
 • angahewa ni korona inayoonekana tu wakati wa kupatwa kwa Jua Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa Jua lilitokea takriban miaka bilioni 4.57 iliyopita
 • ambako Jua linapita ni mstari wa ekliptiki. Jina ekliptiki linatokana na neno la Kigiriki Εκλειψις ekleipsis linalotaja Kupatwa kwa Jua au Kupatwa kwa Mwezi
 • dunia. Hii inalingana na kupatwa kwa jua kiasi. Ilihali Utaridi iko mbali inaonekana ndogo na kufunika sehemu ndogo ya jua tu kwa mtazamaji duniani. Sayari
 • ya jua kwa Kiingereza transit of Venus unatokea wakati sayari Zuhura Venus inapita katika mstari baina ya jua na dunia. Hii inalingana na kupatwa kwa
 • kikuu cha astronomia kwa Waislamu na Wakristo wa Ulaya kwa miaka 1500 iliyofuata. Aliweza kukadiria na kutabiri kupatwa kwa jua Katika hisabati alianzisha
 • Ba Sing Se kutafuta msaada wa Mfalme wa Duniani kwa shambulio la Taifa la Moto wakati wa kupatwa kwa jua ijayo, wakati ambao wazima moto hawatakuwa na nguvu
 • alizonazo mwenye karakana. Karakana husaidia kwa kuhifadhi gari lisiharibike kwa kunyeshewa, kupatwa na jua kali na pia kuibwa. Kufuli za karakana huweza
 • ukubwa na umbali kati ya Dunia, Jua na Mwezi Kitabu 6: Kuhusu kupatwa kwa Jua na kupatwa kwa Mwezi Vitabu 7 8: Mienendo ya nyota, orodha ya makundinyota