Back

ⓘ Danièle Boni-Claverie
                                     

ⓘ Danièle Boni-Claverie

Danièle Boni-Claverie ni mwandishi wa habari na mwanasiasa huko Ivory Coast. Alihudumu katika baraza la mawaziri katika nchi hiyo na alikuwa mwanzilishi na raisi wa Jumuiya ya Muungano wa serikali.

Ni binti wa "Alphonse Boni", alizaliwa Tiassalé. Alifanya kazi kama mwandishi wa habari, akiwa mhariri mkuu wa gazeti na kisha mkuu wa Radiodiffusion Television Ivoirienne RTI).

Hapo awali alikuwa mwanachama wa "Democratic Party of Côte dIvoire - African Democratic Rally | Democratic Party ya Côte dIvoire". Boni-Claverie aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano katika serikali iliyokuwa ikiongozwa na Daniel Kablan Duncan kutoka 1993 hadi 1999. Alihudumu kama Waziri wa Wanawake na Familia na Watoto katika serikali ya Gilbert Aké kutoka 2010 hadi 2011.

Alikamatwa mnamo Oktoba 2016 baada ya kushiriki katika maandamano ya kuomba rasimu mpya ya nchi hiyo iondolewe.