Back

ⓘ Leïla Marouane
                                     

ⓘ Leïla Marouane

Leïla Marouane ni Mwandishi wa habari na Mwandishi wa riwaya zilizopokea tuzo mbalimbali katika fasihi ya Kifaransa

                                     

1. Wasifu

Leyla alizaliwa nchini Tunisia mwaka 1960 katika mji wa Djerba, kisha familia yake ilihamia katika mji wa Biskra, familia yake iliishi hapo kwa muda hadi Leila alipofikisha umri wa miaka sita,Leila alihamia nchini Aljeria na baadae Ufaransa mwaka 1991. Alianza kuwa muandishi wa habari akiwa Aljeria akiandika makala na habari za kisiasa katika magazeti,alisoma katika chuo kikuu cha Paris 8 University hadi alipomaliza shahada yake uandishi,Kitabu chake cha La fille de la Casbah katika Kiingereza The Daughter of the Kasbah kilichapishwa na Éditions Julliard mwaka 1996 tangu wakati huo amechapisha vitabu mbalimbali vya riwaya, kitabu chake cha kwanza kutafsiriwa katikia Lugha ya Kiingereza kilitoka mwaka 1998.

Marouane ni muanzilishi wa La Boutique iloanzishwa mwaka 1996, ikiwa ni asasi ilolenga kuendeleza na kukuza sanaa ya uandishi pamoja na kutangaza lugha ya Kifaransa na kingereza.