Back

ⓘ Kipanya manyoya-mororo
Kipanya manyoya-mororo
                                     

ⓘ Kipanya manyoya-mororo

Vipanya manyoya-mororo ni wanyama wagugunaji wa jenasi Praomys katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae wanaotokea katika misitu minyevu ya Afrika kusini kwa Sahara.

                                     

1. Maelezo

Panya hawa wana manyoya mororo ambayo yanaweza mafupi au marefu. Pua ni ndefu na masikio ni makubwa na ya mviringo. Urefu wa mwili ni mm 90-140, urefu wa mkia ni mm 110-170 na uzito ni g 12-70. Rangi yao ni njano, hudhurungi, kahawianyekundu au kijivu mgongoni na nyeupe au njano tumboni.

Wanapatikana katika misitu minyevu na hukiakia usiku. Hutumia sehemu ya wakati wao katika miti na hujenga viota kwa majani pia mitini au ardhini, pengine katika vishimo. Hula matunda, mbegu na sehemu kijani za mimea, na wadudu pia.

                                     

2. Spishi

 • Praomys rostratus Forest soft-furred mouse
 • Praomys jacksoni, Kipanya Manyoya-mororo wa Jackson Jacksons soft-furred mouse – Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda
 • Praomys delectorum, Kipanya Manyoya-mororo Taanusi Delectable soft-furred mouse – Kenya, Tanzania
 • Praomys derooi Deroos mouse
 • Praomys coetzeei Coetzees soft-furred mouse
 • Praomys verschureni Verschurens swamp mouse
 • Praomys minor Least soft-furred mouse
 • Praomys tullbergi Tullbergs soft-furred mouse
 • Praomys daltoni Daltons mouse
 • Praomys obscurus Gotel Mountain soft-furred mouse
 • Praomys hartwigi Hartwigs soft-furred mouse
 • Praomys misonnei, Kipanya Manyoya-mororo wa Misonne Misonnes soft-furred mouse – Kenya, Uganda
 • Praomys mutoni Mutons soft-furred mouse
 • Praomys petteri Petters soft-furred mouse
 • Praomys degraaffi, Kipanya Manyoya-mororo wa De Graaff De Graaffs soft-furred mouse – Burundi, Rwanda, Uganda
 • Praomys morio Cameroon soft-furred mouse
 • Praomys lukolelae Lukolela swamp mouse