Back

ⓘ Daisy Bates
                                     

ⓘ Daisy Bates

Baba yake ni Hezakiah Gatson na mama yake ni Millie Riley. Alikulia kusini mwa Arkansas, katika mji mdogo wa Huttig, Arkansas. Hezakiah Gatson, alihudumia familia yake kwa kufanya kazi ya kukata mbao,katika kiwanda kidogo Cha kukatia mbao. Mama yake Millie Riley aliuawa wakati Daisy akiwa mdogo sana, na alilelewa na rafiki yake mama yake aliyejulikana kwa jina la Orlee Smith, aliyekuwa shujaa wa Vita ya kwanza ya dunia, na mke wake Susie Smith. Baba yake Hezakiah alimtelekeza, na Daisy hakuweza kumuona tena. kwenye kifo cha mama yake. Bates alikuja kutambua akiwa na miaka nane kuwa mama yake mzazi,alibakwa na kuuawa na wazungu watatu wa kiume, na mwili wake kutupwa kwenye dimbwi la maji, ambapo ilikuja kujulikana baada.

Baada ya kujua kwamba hamna mtu aliyeshitakiwa kwa kifo Cha mama yake, ilimshtua na kumpa hasira baada ya kuona kuwa hamna haki iliyotendeka. baba yake wa kumrithi,Orlee Smith, alimwambia kuwa wauwaji, hawajawahi kupatikana na polisi hawakuonyesha jitihada ya kuwatafuta wauawaji.

Bates alisema hajawahi kusahau hicho. Aliamini kuwa hiyo kumbukumbu inamsaidia kumpa nguvu katika uongozi wa haki za binadamu.

Kabla ya kuambiwa ukweli kuhusu kifo cha mama yake, alikuwa akicheza na Beatrice, msichana wa kizungu aliyekuwa rika moja naye. Walishirikiana fedha kidogo walionayo na kuishi vizuri.

Daisy alikuwa na miaka 17 wakati alipoanza kuwa na uhusiano na Lucius Christopher Bates, aliyekuwa muuza bima, pia aliwahi kufanya kazi ya magazeti katika kusini na magharibi. Lucius alitengana na mke wake wa Kwanza mnamo mwaka 1941 kabla ya kuhamia Little Rock na kuanza Arkansas State Press. Daisy na L.C. Bates walioana mnamo machi 4.1942

Mnamo mwaka 1952, Daisy Bates alichaguliwa kuwa rais wa Arkansas Conference ya NAACP branches.

                                     

1. Heshima na Tuzo

Alitajwa kuwa mwanamke wa mwaka mnamo mwaka 1957 na National Council of Negro Women. Arkansas General Assembly Commendatio ilimzawadia shahada ya Uzamivu ya Sheria katika chuo kikuu Cha Arkansas mnamo mwaka 1984. Shule ya Daisy Bates Elementary School katika Little Rock ilipewa jina hilo kwa heshima yake. Mnamo tarehe 11 April, 2019 serikali ya Asa Hutchinson walisaini katika Sheria mswada wa kumpitisha Daisy Bates na muimbaji Johnny Cash Kama wawakilishi wawili Wa mji wa Arkansas katika majimbo ya marekani National Statuary Hall Collection.