Back

ⓘ Josie Duffy Rice
Josie Duffy Rice
                                     

ⓘ Josie Duffy Rice

Josie Duffy Rice ni mwandishi habari kutokea nchini Marekani. Mnamo 2019, Alitajwa kama raisi wa The Appeal, shirika la uandishi Habari linalolenga zaidi mfumo wa haki za wahalifu. Duffy Rice pia anaendesha jarida la Marekani kwa jina la Justice in America. Kazi zake zimetajwa mara kadhaa na majarida ya The New York Times, Nylon, na Harpers Bazaar.

                                     

1. Maisha ya awali na elimu

Duffy Rice alizaliwa kama Josie Duffy, binti mkubwa kabisa wa Eugene na Norrene Duffy, alilelewa na kukulia jijini Atlanta. Ana dada mmoja, kwa jina la Rosa Duffy ambaye no mmiliki wa duka la vitabu kwa jina la For keeps. Bini yake kwa jina la Josie Johnson, ni mwanaharakati wa haki za binadamu anayefanya shughuli hiyo akiwa jijiniMinneapolis.

Duffy Rice alipata shahada yake ya kwanza katika Sayansi ya siasa kutoka Chuo Kikuu cha Columbia. Alifanya kazi kama msaidizi mtendaji wa shirika la watetezi wa umma huko Bronx moja kwa moja baaada ya kuhitimu chuo kikuu, ambayo iliathiri uamuzi wake wa kuhudhuria shule ya sheria. Alipokea digrii yake ya sheria maarufu kama Juris Doctor kutoka shyule ya sheria ya Harvard. Duffy Rice alipendelea kuandika kazi za kisheria, na baada ya shule ya sheria alianza kufanya kazi katika nyanja za sera na uanaharakati.

                                     

2. Kazi

Kazi yake amejikita zaidi katika haki za wahalifu kama vile uonevu wa askari polisi na dhamana kwa hela ya papo hapo. Duffy Rice anapinga sana uwepo wa askari polisi pamoja na gharama kuendesha vitengo vya polisi kama njia mojawapo ya kufikia lemgo lake. Alishapata mualiko katika majadiliano maarufu katika kipindi cha The Daily show kujadili suala hili na kuhusu vyombo vinavyoelezea juu ya haki ya wahalifu kama Slate, NPR; na Lte Night with Seth Meyers.

Duffy Rice hapo awali alifanya kazi kama mwanamikakati katika Mradi wa Adhabu ya Haki. Mnamo mwaka 2017 alijiunga na Ushirikiano wa Haki, inayoendasha shirika maarufu kwa jina la The Appeal, tovuti ambayo inalenga sera, siasa, na haki ya wahalifu. Duffy Rice aliteuliwa kama raisi wa shirika la The Appeal mnamo 2019.

Duffy Rice anashirikiana na jarida la habari juu ya nchini Marekani akiwa na wageni waalikwa ambao ni Darnell Moore, Donovan X. Ramsey, Derecka Purnell, na Zak Cheney-Rice. Kipindi kinashughulikia mada za haki ya wahalifu kama vile kiwango kikubwa cha wafungwa nchini Marekani.

Duffy Rice alikuwa mwandishi anayechangia toleo la Septemba 2020 la Vanity Fair iliyohaririwa na Ta-Nehisi Coates.