Back

ⓘ Simona Marchini
                                     

ⓘ Simona Marchini

Simona Marchini ni mwigizaji, mtangazaji wa redio na runinga, muongozaji wa jukwaa, mchekeshaji na anajihusisha na sanaa nchini Italia.

                                     

1. Maisha na Kipaji chake

Alizaliwa na mfanyabiashara anayeitwa Alvaro, alihitimu shahada yake ya fasihi katika chuo kikuu cha La Sapienza.

Anapenda sanaa, tangu mwaka 1966 aliongoza nyumba kadhaa za sanaa, moja ya nyumba ya sanaa aliyoiongoza ni "Nuova Pesa" na aliongoza nyumba hiyo kati ya mwaka 1985 na 1995.

Baada ya kuwa mwigizaji na muongozaji hodari, mwaka 1980 alianza uchekeshaji katika maonyesho tofauti kwenye runinga RAI A tutto gag na alionekana katika baadhi ya filamu za uchekeshaji, televisheni na vipindi vya redio.

                                     

2. Maisha yake binafsi

Aliwahi kuolewa na mwanamume kutoka familia tukufu Calabria, na 1970 mpaka 1980 Marchini aliolewa na mchezaji wa mpira Franco Cordova.

Marchini pia ni balozi wa UNICEF Goodwill Ambassador.