Back

ⓘ Kipanyanyasi-milia
Kipanyanyasi-milia
                                     

ⓘ Kipanyanyasi-milia

Panya hawa wana mlia mweusi mgongoni na spishi wengine zina milia na madoa mengine pia. Urefu wa mwili ni mm 90-140, urefu wa mkia ni mm 95-150 na uzito ni g 18-70.

Kwa ujumla huzingatiwa kukiakia wakati wa mchana, lakini angalau spishi kadhaa zinaweza kukiakia usiku. Hula majani, mizizi na mbegu na mara kwa mara wadudu pia.

Kuna wachanga hadi 12 kwa kila mkumbo, lakini 4-5 ni kawaida zaidi. Wanaweza kuwa na mikumbo minne katika kipindi cha chini ya miezi minne. Wastani wa matarajio ya muda wa kuishi ni mfupi sana, porini mara nyingi mwaka mmoja tu, lakini L. striatus aliishi kwa karibu miaka 5 kifungoni.

                                     

1. Spishi

 • Lemniscomys zebra, Kipanyanyasi-milia wa Heuglin Heuglins striped grass mouse – Kenya, Tanzania, Uganda
 • Lemniscomys bellieri Belliers striped grass mouse
 • Lemniscomys barbarus Barbary striped grass mouse
 • Lemniscomys roseveari Rosevears striped grass mouse
 • Lemniscomys mittendorfi Mittendorfs striped grass mouse
 • Lemniscomys hoogstraali Hoogstraals striped grass mouse
 • Lemniscomys griselda Griseldas striped grass mouse
 • Lemniscomys linulus Senegal one-striped grass mouse
 • Lemniscomys rosalia, Kipanyanyasi Mlia-mmoja Single-striped grass mouse – Kenya, Tanzania
 • Lemniscomys macculus, Kipanyanyasi Milia-hudhurungi Buffoon striped grass mouse – Kenya, Uganda
 • Lemniscomys striatus, Kipanyanyasi-milia wa Kawaida Typical striped grass mouse – Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda