Back

ⓘ Kipanya-misitu
                                     

ⓘ Kipanya-misitu

Vipanya-misitu ni wanyama wagugunaji wa jenasi Hylomyscus katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae ambao wanatokea katika misitu na maeneo yenye midambi ya Afrika kusini kwa Sahara.

                                     

1. Maelezo

Vipanya hawa wana masikio makubwa yenye mviringo na mkia mrefu na mwembamba. Urefu wa mwili ni mm 55-120, urefu wa mkia ni mm 75-175 na uzito ni g 6-42. Manyoya yao ni laini na kahawia hadi kahawianyekundu mgongoni na kijivu iliofifia tumboni.

Hukiakia usiku na wanaishi kwenye miti. Hula matunda, mbegu na wadudu.

                                     

2. Spishi

 • Hylomyscus endorobae, Kipanya-misitu Miguu-midogo Small-footed wood mouse – Kenya
 • Hylomyscus vulcanorum, Kipanya-misitu wa Volkano Volcano wood mouse – Burundi, Rwanda, Uganda
 • Hylomyscus stella, Kipanya-misitu wa Stella wood mouse – Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda
 • Hylomyscus walterverheyeni Walter Verheyens mouse
 • Hylomyscus thornesmithae Mother Ellens wood mouse
 • Hylomyscus mpungamachagorum, Kipanya-misitu wa Mahale wood mouse
 • Hylomyscus aeta, Kipanya-milia wa Uganda Beaded wood mouse – Burundi, Uganda
 • Hylomyscus simus Flat-nosed wood mouse
 • Hylomyscus alleni Allens wood mouse
 • Hylomyscus pygmaeus Pygmy wood mouse
 • Hylomyscus parvus Little wood mouse
 • Hylomyscus carillus Angolan wood mouse
 • Hylomyscus baeri Baers wood mouse
 • Hylomyscus heinrichorum Heinrichs wood mouse
 • Hylomyscus anselli, Kipanya-misitu wa Ansell Ansells wood mouse – Tanzania
 • Hylomyscus Pamfi wood mouse
 • Hylomyscus stanleyi, Kipanya-misitu wa Stanley Stanleys wood mouse
 • Hylomyscus grandis Mount Oku wood mouse
 • Hylomyscus kerbispeterhansi, Kipanya-misitu wa Ml. Elgon Kerbis Peterhanss wood mouse – Kenya, Uganda
 • Hylomyscus arcimontensis, Kipanya-misitu wa Tao la Mashariki Arc Mountain wood mouse – Tanzania
 • Hylomyscus denniae, Kipanya-misitu wa Ruwenzori Montane wood mouse – Uganda