Back

ⓘ Kikalio cha Dhahabu
Kikalio cha Dhahabu
                                     

ⓘ Kikalio cha Dhahabu

Kikalio cha Dhahabu ni kiti cha enzi cha kifalme cha wafalme wa Ufalme wa Ashanti na ishara kuu ya mamlaka kuu. Kulingana na mapokeo, Okomfo Anokye, Kuhani mkuu na mmoja wa waanzilishi wakuu wa ufalme wa Ashanti, alisababisha kikalio hicho kushuka kutoka mbinguni na kutua kwenye paja la Osei Tutu aliyekuwa mfalme wa kwanza wa Ashanti.

Kikalio cha Dhahabu kinaaminika kuwa na roho ya taifa la Ashanti ndani yake.

                                     

1. Mgogoro wa kihistoria

Vita nyingi zimeibuka juu ya umiliki wa kiti hicho cha kifalme. Mnamo mwaka wa 1900, Sir Frederick Hodgson, Gavana Mwingereza wa Gold Coast, alitaka kukalia Kikalio cha Dhahabu akaamuru kipelekwe mbele yale. Lakini Waasante walikificha. Ufatwaji wa kiti ulisababisha uasi wenye silaha unaojulikana kama Vita ya Kikalio cha Dhahabu, ambayo ilisababisha maeneo ya Ashanti kutwaliwa na Uingereza na kuwa koloni. Lakini Waingereza walishindwa kupata kiti.

Mnamo 1921, wafanyakazi Waafrika kadhaa waliojenga barabara waligundua kikalio cha dhahabu wakavua mapambo kadhaa ya dhahabu. Walikamatwa na Waingereza, kabla ya kuhukumiwa adhabu ya kifo kulingana na mila ya Ashanti. Waingereza waliingilia kati na badala yake wahukumiwa walifukuzwa katika Ghana. Hapo serikali ya kikoloni iliahidi kwamba haitaingilia tena mambo ya kikalio kikatolewa mafichoni.

Mnamo mwaka wa 1935 kikalio kilitumika katika sherehe ya kumtawaza Osei Tutu Agyeman Prempeh II.

                                     

2. Muonekano na ufundi

Kikalio cha Dhahabu ni kiti kilichopindika sm 46 juu chenye nafasi ya upana wa sentimita 61 kwa 30. Uso wake wote umepambwa kwa dhahabu, na umetundikwa na kengele kumwonya mfalme juu ya hatari inayokuja. Haikuonekana na watu wengi, ilhali ni mfalme tu, malkia, na washauri wanaoaminika wanajua maficho yake.

Mifano yake yametengenezwa kwa ajili ya machifu na kwenye mazishi yao inapakwa damu ya wanyama. Kikalio cha dhahabu ni moja ya ishara kuu za Asante leo kwa sababu bado inaonyesha mfululizo wa kifalme na mamlaka.

                                     

3. Viungo vya nje

  • West African Kingdom: Asante. BBC World Service.
  • Picture of Golden Stool
  • African Stools. Hamill Gallery of Tribal Art, catalogue of exhibition, March 1-May 26, 2001.
                                     
  • wa Waashanti anakalia hadi leo jumba lake mjini. Ndipo kilipo kikalio cha dhahabu cha Asantehene ambacho kinaaminiwa kimeteremshwa kutoka mbinguni. Mwaka
  • Waashanti mfalme wa Kumasi au: Kumasihene Osei Kofi Tutu I alipokea kikalio cha dhahabu kama alama ya kuteuliwa na mbinguni lakini hali halisi kiti kilitengenezwa