Back

ⓘ Maria (Kipindi cha televisheni)
                                     

ⓘ Maria (Kipindi cha televisheni)

Maria ni kipindi cha televisheni nchini Kenya ya hadithi ya mapenzi iliyoelekezwa na Julian S. Mwanzele inayomshirikisha Yasmin Said kama mwigizaji mkuu, pamoja na Brian Ogana na Bridget Shighadi katika kipindi chao cha kwanza kwenye televisheni. Kilionyeshwa kwa mara ya kwanza Oktoba 10, 2019 na onyesho la mwisho likafanyika Machi 18, 2021, baada ya jumla ya maonyesho 374. Kipindi hiki kilionyeshwa katika runinga ya Citizen TV kila siku ya wiki saa 7:30 usiku saa za Afrika Mashariki na pia katika chaneli ya Viusasa.

Hadithi hii ya mapenzi inaangazia wahusika watatu wakuu kwenye kipindi - Maria, binti wa kupanga mwenye mvuto; Luwi, kifungua mimba wa aila kwasi ya Hausa na Sofia, mkewe Luwi ambaye lengo lake ni kupokonya mali ya familia ya wakwe zake.

                                     

1. Muhtasari

Tamthiliya hii inaangazia maisha ya mhusika mkuu Maria Yasmin Said pamoja na yanayomkuta jijini Nairobi. Hakuweza kuwaona wazazi wake wa kumzaa, wote ambao waliaga dunia yeye akiwa angali mchanga, hivyo basi, akalelewa na mama mlezi Naomi ambaye pia akaaga dunia baadaye. Maria anakuja kuwa binti wa kupanga kwenye familia ya William Hausa, tajiri mmoja aliyejuana na babake tangu zamani. Kule, anamkuta Luwi ambaye licha ya uanandoa wake na Sofia, anapatwa na hisia za mapenzi juu ya Maria. Maria pia baadaye anagundua kwamba anazo hisia zizo hizo kwa Luwi, na wote wawili nanakuja kuwa wapenzi. Matukio mengi yanafanyika kama vile Sofia kuigiza uchizi kwa minajili ya kufanikisha mpango wake. Anapojifanya kuwa sawa hatimaye, anaomba talaka yake, jambo linalompa Luwi uhuru wa kumchumbia Maria. Huba hilo lenye kina kirefu linayeyuka ghafla, pindi tu Maria anapogundua kuwa William Hausa ndiye muuaji wa babake na mali zote anazo ni za babake, yakiwemo maovu mengine, yote ambayo aliyasitiri moyoni mwake na hakumruhusu yeyote ayajue. Vile vile, inagundulika kuwa Victor siye mwanawe mzee William wa kumzaa, ya kwamba yeye ni ndugu wa kambo wa Sofia pamoja na Luwi. Anaifurusha aila yake nyumbani kwao na kisha baadaye kuchizika. Mzee William, pamoja na mshauri wake Mejja wanakula njama ya kumfanya Sandra atiwe mbaroni. Sandra, ambaye daima alizama kwenye mapenzi na William asisikie lolote wala chochote, anaahidi kulipiza kisasi baada ya usaliti alioshuhudia. Mzee William anashuhudia ajali mbaya inayomfanya kiwete abadi. Kumwona katika hali hiyo, Maria, aliyekuwa na mpango wa kumfungulia mashtaka William, anamhurumia na kuufutilia mbali wazo hilo la awali. Anaukubali uchumba wa Luwi kwa mara nyingine tena kisha wao wawili wanapanga harusi yao. Kwa bahati mbaya, Sofia anapigwa risasi siku hiyo ya harusi na Brenda ambaye lengo lake lilikuwa ni Maria. Silas anamchumbia Vanessa huku Maggie akihuzunika kwa sababu hata yeye anazo hisia za mapenzi juu yake Silas. Mzee William pia anakamatwa na askari siku hiyo kwa makosa mengi aliyoyafanya hapo nyumaye. Anaaukubali agizo hilo kiurahisi. Miezi michache imepita na waarusi wale wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza. Tunawaona Luwi na Maria wakiifurahia fungate yao na kutembelea mbuga ya wanyama. Wote wanasemezana mapenzi yao huku wakitarajia maisha mema baadaye.

                                     

2.1. Wahusika na waigizaji Waigizaji wakuu

 • Sheila Ndanu kama Madam Victoria Hausa au Vickie
 • Brian Martins Ogana kama Luwi Hausa
 • Dennis Musyoka kama Boss William Hausa
 • Wanjiku Stephens kama Vanessa Hausa
 • Bridget Shighadi kama Sofia
 • Ronald Ndubi kama Victor
 • Yasmin Said kama Maria Tino
                                     

2.2. Wahusika na waigizaji Waigizaji wasaidizi

 • Brian Kibochi kama Bondi
 • Tina Njambi kama Lorna
 • Tindo Mwanzele kama Mwambe
 • Nyakundi Isaboke kama Silas
 • Jane Mulanda kama Dogo
 • Abdalla Ali kama Jayden
 • Sarah Malaki kama Mama Chapo
 • Aisha Hussein kama Gloria
 • Anthony Ashioya kama Tekno
 • Maureen Wangare kama Brenda
 • Musa Ore kama Father Ezekiel
 • Suzie Malaki kama Rufina
 • Robert Budi kama Trevor
 • Blessing Lungaho kama Meja
 • Linda Alexette kama Tobi
 • Botul Abdalla kama Marianne
 • Timothy Musyoka kama Ben
 • Terry Ombaka kama Naomi
 • Carol Kipsuto kama Sandra
 • Christopher Kamau kama Daniel
 • Edwin Buni kama Koros
 • Quincy Ando kama Thomas
 • Joseph Kiplabatt kama Collo
 • Umar Hussein kama Pupa
 • Belinda Joana kama Kobi
 • Grace Obuya kama Sister Teresa
 • Periz Wambui kama Salome
 • Teddy Brown kama Fali
 • Beatrice Dorea kama Maggie
 • Alice Mari kama Kanini
 • Edna Nguka kama Delilah