Back

ⓘ Kito (madini)
Kito (madini)
                                     

ⓘ Kito (madini)

Kito ni madini adimu na ngumu zinazopendeza kwa sababu ya uangavu na rangi yake. Vito mbalimbali vinapendwa na watu na kutumiwa kama mapambo. Kito chenye ugumu na thamani kubwa ni almasi.

Mara nyingi vinakatwa, kusuguliwa na kungarishwa kwa namna mbalimbali na kutumiwa pamoja na metali adili kama dhahabu au fedha kuwa mapambo kama pete, hereni, mkufu au bizimu.

Mifano ya vito ni

  • almasi
  • tanzanaiti
  • zumaridi
  • feruzi
  • yakuti

Lulu na korali hutajwa wakati mwingine pia kama kito ingawa si minerali asilia lakini dutu inayotengenezwa na wanyama.